Wizi mkubwa kwa njia ya Mizani kwenye Butcher

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mabilioni na mabilioni ya fedha za wananchi zinaibiwa kila siku na wafanyabiashara kwa njia ya Mizani zisizoweza kupima kile kinachotakiwa kupima. Mara zote Mizani yetu inapima pungufu ya kile mteja anachonunua na kupima zaidi kile mfanyabiasha anachotaka kununua kwa mwananchi.
Hatuwezi kuwa makini kupima makontena ya mchanga wa dhahabu kama tunashindwa kupima kwa usahihi kilo moja ya nyama anayouziwa mwananchi.

Maduka mengi mitaani yanatumia mizani za mawe, beam balance ambazo ama zimechezewa au zimeharibika.

Nyama mchanganyiko ni wizi mkubwa kwa wananchi, kwakuwa mwananchi hajui anauziwa nyama kiasi gani na mifupa kiasi gani. Ukimtuma mtoto mdogo butchani ndo kBisA atauziwa mifupa mingi kuliko nyama.

Sheria ya kupiga marufuku kuuza nyama mchanganyiko itungwe ili mlaji apate uhalisia wa kile anachokinunua kwa kilo. Kama anataka mifupa anunue mifupa, kama anataka nyama anunue nyama na kama anataka mchanganyiko aende akachanganye mwenyewe nyumbani kwake baada ya kununua.
Wafanyabiashara woote Lazima watumie digital mizani katika kuuza na kununua bidhaa.

Hili nalo linahitaji mpaka Rais Magufuli aseme?
 
Mtoa hoja jaribu kudadavua sijui beam zinachezewa sijui nini, mizani wanachezea vitu gani ili nasi tujue. Funguka zaidi tuwabaini hawa wezi.
 
Mtoa hoja jaribu kudadavua sijui beam zinachezewa sijui nini, mizani wanachezea vitu gani ili nasi tujue. Funguka zaidi tuwabaini hawa wezi.
Duuh, katika mizani zinazotumia huwa zina sehemu kuu tatu, upande kushoto unaowekwa jiwe (effort), upande wa kulia unaowekwa bidhaa inayopimwa (effect) na katikati kwenye egemeo (pivot) la kushoto na kulia. Kama Mizani haina mzigo wowote upande wa kushoto na kulia lazima uwe sawa (balance), mzani lazima uonekane unayumba na kuelea (oscillate) kati kwa kati kwa ulinganifu. Sasa unapotaka kupima bidhaa ya kilo moja lazima uweke jiwe la kilo kilo 1 kushoto na kisha uweke (upime) kulia wa mizani bidhaa yenye uzito sawa na jiwe lililoko kushoto had kulia na kushoto kuelee katikati (balance) bila kuelekea ubande wowote.

Kuibiwa mteja kutatokea kwa njia zifuatazo 1. Jiwe lililoko kulia Lina uzito pungufu kuliko kipimo kinacho nunuliwa na mteja, 2. Mfanyabiashara anaweka kitu kinachoongeza uzito upande wa kulia wa mizani kama vile kipande cha sumaku, jiwe au kitu chochote ambacho kitaongeza uzito upande wa bidhaa ili kudanyanya uzito. Kwa upande wa nyama Unaweza kuongezewa mifupa, mafuta, au kitu chochote ambacho utakwenda kukitupa tu ukifika nyumbani.

Dalili kubwa ya kujua kuwa mizani imechezewa ni kumuamuru muuzaji aondoe mawe yote upande wa kushoto ili uone kama mizani ina balance kabla haijawekewa kitu chochote, mawe au bidhaa. Mwenye duka atahakikisha kuwa upande wa kushoto kumewekwa kitu hata kama hakuna kitu kinachopimwa.
 
Mtoa mada umefikiria sahihi kabisa. Nyama mifupa vitenganishwe. Ila tatizo vifaa vya kutegaishia nyama na mifupa.
Vifaa vipo kama vile wanavyonunua misumeno ya umeme siku hizi, mbona kwenye super markets wanaweza?
 
Asante kwa darasa zuri. LAKINI hali hii ipo hata katika vituo vya mafuta nimejaribu kufuatilia kuwabaini wanawezaje kutupunja mafuta wakati mashine inasoma kiasi cha lita na pesa sawa halafu unakuwa mafuta pungufu? Mimi nachokaga kabisa, hivi ipoje hii
 
Mbona kila unachotaka mbona kinapatikana tuu.
Ukija buchani na sio buchani tu hata dukani hakikisha mzani upo balanced ukiwahauna kitu.
Nyama mchanganyiko ni 6000
Stake (hapa hakuna mfupa) 7000.
Chagua 1
Hapa hakuna haja ya kulalamika na kusubiri matamko jiamlie tuu
 
Mtoa hoja jaribu kudadavua sijui beam zinachezewa sijui nini, mizani wanachezea vitu gani ili nasi tujue. Funguka zaidi tuwabaini hawa wezi.
Sehemu ya Mzigo kwenye beam balance huwekwa sumaku yenye uzito kama gramu 180 ivi hivyo nyama inapowekwa inajibalance haraka lakini uzani ule ni Pamoja Na sumaku siyo nyama tu.

Nadhani niishie hapo nisijemwaga mengi Na kuharibu biashara. Kila Kazi INA namna ya kutengeneza black benefit. Sumaku hutaiona maana huwa sehemu anayosimama muuzaji.
 
Hii iko hv mfano bodaboda kaja kaweka mafuta ya 2000 we unaenda na gari unatak mafuta ya elf kumi na 5 pale utakuta ubao unasoma elf 2 aliyotok kuweka kweny bodaboda hata futa ile elf mbili ataanza kuandka kiwango cha hela yako ya mafuta elf 15 hapo kwenye hesabu itasomeka ameweka mafuta ya elf kumi tatu yaan inakua kama umenunua mafuta ya elf mbili then ukanunua ya elf 13 ndo ikatimia elf kumi na 5 so elf mbili anatia mfukoni
Inatakiwa utakapoenda sheli ukikuta mteja katok waambie waanze na sifuri...
 
You are Smart
 
Duuu.... Umenifumbua
 
Lengo la mteja ni kununua nyama sio mifupa, sasa hana uhakika kwenye hiyo nusu kilo aliyouziwa kapata nyama kiasi gani na mifupa kiasi gani, shombo tu, watoto wanaramba mifupa.
 
hoja nzuri mno kuhusu mada hii,ila umefika wakati nasi tusogee mbele ,turuhusu hizi super markets zetu kama Game or shoprite ziwe zinauza nyama ambayo imeshapimwa na kufungwa vizuri na itakuwa inaonyesha uzito wake na bei yake,hii itasaidia kuongeza ushindani na kuwafanya hawa wafanya biashara ya mabucha nao kuboresha huduma zao.
 
Mkuu, naomba ufafanue zaidi hapo, ninapoingia filling station, nikakuta kwenye dispenser inasoma 2000, kwamba mteja aliyetoka ndo aliwekewa mafuta ya pesa hiyo, mimi nikitaka aweke ya 15000 na nikaona pale kwenye display ameandika 15000 na litres ikaanzia 0, bado nitakuwa nimepigwa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…