Wizi mkubwa kwa njia ya Mizani kwenye Butcher

Lengo la mteja ni kununua nyama sio mifupa, sasa hana uhakika kwenye hiyo nusu kilo aliyouziwa kapata nyama kiasi gani na mifupa kiasi gani, shombo tu, watoto wanaramba mifupa.
Nunua steki
 
Nunua steki
mabutcher mengi hawataki kuuza steki, wanakwambia mifuta tutaipeleka wapi? Nadhani kuna haja ya kujenga viwanda vinavyotumia mifupa kama malighafi
 
Mkuu.. Ng'ombe hasimami kwa msaada wa upepo, anatumia mifupa..

Mbona kuna butcher zinasema kabisa kuwa ukitaka stake tupu kuna bei yake na ukitaka mchanganyiko kuna bei yake.

Ni wewe tuu na suala la kuchagua
 
Shoppers Plaza Mikocheni wako vizuri kabisa, wameshafika huko unakokutamani mimi na familia yangu tunanunua nyama (sio mifupa) kule, na ukitaka kiungo kama mkia, chicken wings, breasts, figo, nk nenda kule bhana ukajionee mwenyewe.
 
Mkuu.. Ng'ombe hasimami kwa msaada wa upepo, anatumia mifupa..

Mbona kuna butcher zinasema kabisa kuwa ukitaka stake tupu kuna bei yake na ukitaka mchanganyiko kuna bei yake.

Ni wewe tuu na suala la kuchagua
Mchanganyiko wa aina gani, nyama na mifupa au mifupa na nyama? mtume mtoto au house girl uone atakuletea mchanganuiko wa aina gani
 
mabutcher mengi hawataki kuuza steki, wanakwambia mifuta tutaipeleka wapi? Nadhani kuna haja ya kujenga viwanda vinavyotumia mifupa kama malighafi
Huwa ina bei y@ juu zaidi
 
Hapo unakuwa umepigwa inatakiwa upande wa hela pale afutee aanze na zero
 
Lengo la mteja ni kununua nyama sio mifupa, sasa hana uhakika kwenye hiyo nusu kilo aliyouziwa kapata nyama kiasi gani na mifupa kiasi gani, shombo tu, watoto wanaramba mifupa.
Si wanatuzuga nao wana bundle la steak na mixer
 
Hasa hizi mizani za digital,wanazichezea sana,bora za mawe
 
Hasa hizi mizani za digital,wanazichezea sana,bora za mawe
Siku hizi nikifikani kitu cha kwanza kabla sijaagiza ninachotaka kununua nakimbilia kuondoa mawe kwenye mizani, nikifika petrol station nashuka kabisa kwenye gari na kuangalia pump inaanzaje na kuishiaje
 
Kavulata, kwani si inawezekana pia hata pampu ikianza 0 mteja kupunjwa mafuta.
Au mzani kuwa balance lakini mteja kupunjwa?
 
Kavulata, kwani si inawezekana pia hata pampu ikianza 0 mteja kupunjwa mafuta.
Au mzani kuwa balance lakini mteja kupunjwa?
Ikoje hiyo mkuu, hebu tonya wengine
 
Kuna haja serikali itunge sheria kuzua uuzaji wa nyama ya ngombe pamoja na mifupa take kama VP nyama iuzwe peke take na mifupa peke take.

Nijuavyo mthibiti was vipimo huwa ni wakala was vipimo na wanafanya ukaguzi wao kila mwaka lkn kwenye mabucha watembeleaga mara kwa mara, mbinu ingine wanayotumia ni kugandisha nyama ya mafuta kwenye sahani ya mzani ambayo haitoki na pia na kufunga Uzi kwenye upande mwingine na kuukanyagia chini ili mzani uonekane umebalance
 
Sa tunaibiwaje..nlitegemea utatililika madini ya maana..kumbe maoni tu.
 
Hapo kuanzaje Na sifuri...?
 
Wauza nyama wana njia kadhaa za kukuibia. Mbali ya kukujazia mifupa, hawa jamaa wanaiba kwa kukupunja uzito. Kwenye uzito njia tatu ambazo nilishawabaini wauzaji na kutaka kuwaweka ndani
1. Wakati wanakupimia nyama, kwenye ile bakuli huwa kunakuwa na nyama mbovu au mfupa. Na muda wote hawa hawatoi jiwe kwenye mzani. Wanakujazia nyama kwenye chombo wakati kulikuwa na nyama mbovu. Kwa wale hawana mashine za kukatia, pale kwenye gogo Kunakuwa na nyama mbovu au mfupa, wanakusanya na nyama ulioiona nzuri bila kujua.
2. Pale katika ya mzani kunakuwa na kibati akiwa anapima anasogeza na kidole, mzani unakula kwako.
3. Yale mawe hayajafika uzito unao hitajika. Kunasiku walijichanganya,,walinipimia nyama kg 2, wakati anahangaika kutafuta chenji nikaona jiwe lingine la kg 2 lipo chini. Nikalichukua nikaweka ndani ya bakuli la kupimia (nina maana nikayapima mawe yenyewe). . Duuh ziito kuliko alilotumia kunipimia. Aliporudi akakuta hilo zoezi jamaa akakimbia, mwenzake akaja kunituliza na kunipa chenji yangu na rushwa ya nyama ya kutosha.

Ushauri: nunua nyama kwenye maduka ya nyama yenye mizani ya kielektroniki
 
Tunahangaika kupima inayotoka na kwenda nje ya Tanzania lakini tunasahau mizingo inayokwenda kwa wananchi wetu wa kawaida kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…