Wizi mkubwa mechi ya Simba na Yanga

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
16,784
Reaction score
23,312
Mechi hii iliyofanyika Jumamosi ilikuwa na matukio mengi ya uwanjani na nje ya uwanja lakini wakati washabiki wengi wakijikita kwenye mjadala wa penati ya Kagere kama ni halali au siyo halali na wengine kujikita kumjadili Aishi Manula juu ya magoli yaliyofungwa huku nje kabla ya kuingia kulikuwa na mtafaruku mkubwa kwa waliokuwa wakiingia baada ya mashine za Selcom kukataa kuzitambua tiketi zao kwa kushindwa kusomeka kwenye mashine.

Cha ajabu watu wamenunua tiketi zaidi ya moja sehemu moja nyingine zinasomeka huku nyingine hazisomi kama sio busara za kuamua watu wote wenye tiketi waingie bila shaka kungetokea maafa makubwa kwani hakuna mtu ambaye angekubali azuiliwe kuingia uwanjani na hali amelipia pesa ili aone mpira.

Kwa haraka haraka unaweza kuchukulia ni tatizo la kimfumo lakini ukweli ule ni wizi ambao ulipangwa kistadi kwa kuiibia mamlaka ya mapato na club kwa kushirikiana na watendaji wa club na ndiyo maana labda mpaka leo wamekuwa na kigugumizi cha kutangaza mapato yaliyopatikana.
 
Hii ndio Bongo bana.

Kama na ukali wote bado Watu wanaigiza usalama wa Taifa wewe nani usiwavulie kofia Wabongo?
 
Na kusema Tiket za elf 7000 zimeisha ili wauze za VIP na walitujaza VIP mpaka tukakosa paa kukaa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Na kusema Tiket za elf 7000 zimeisha ili wauze za VIP na walitujaza VIP mpaka tukakosa paa kukaa


Sent from my iPhone using JamiiForums
Yaani Watu wanafahamu kabisa kuna siti 100 lakini wanauza tiketi 500.

Wabongo brain ni 0.
 
Na kusema Tiket za elf 7000 zimeisha ili wauze za VIP na walitujaza VIP mpaka tukakosa paa kukaa


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ndo mkome next time. Biashara za watu zile
 
Ushamba wa Nchi imekuwa mzigo mkubwa. Najiuliza kwa nini namba za viti hazitumiki. Kwa nini milango yote aliyoweka Mchina kwa kuzingatia ukubwa wa uwanja haitumiki. Wanalazisha watu elfu 60 kutumia milango michache na kutengeneza foleni..
Hadi ije itokee stampede watu wafe ndiyo waanze kuunda tume za uchanguzi ambazo hazitoi taarifa yoyyote.. Kikubwa ndugu zao wamekula posho.
 
Mi najiuliza sana,huu wizi wa wazi hadi mh. Rais aje?

Nilitarajia watu wawe rumande na wabinywe ili waseme wanaibaje.
Taifa la matapeli majizi majizi tu inatakiwa ifike mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WE UNAHISIII MAGUUU AWAJUIII AKAWAONDOAAA KWENYEE MWENDOKASII HAOOO BALAAAAAA TFF WENYEWE WANAJUA WANACHPATA NDIOMAANA WAKAPEWA DILII HAOOO KUPATAKAZI LAZIMA WAKUPE MZIGOO WANAJUA WANARUDISHAA WAPIII
 
UNAJUA KUNA VIONGOZI WA TTT HUKO NYUMA KILA MECHI ZA SIMBA NA YANGA WAKIMALIZA JTATU WAKO SHOW ROOM WANANUNUA MAGARI MAPYA NA WENGINE SI CHINI YA MOJA MWACHENI KAGERE WANGU HATAKAMA MMEMSHTUKIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…