Wizi mwingine wa mitandao ni makampuni ya simu kukata bando lako kwa kuhesabu SMS zilizoingia

Wizi mwingine wa mitandao ni makampuni ya simu kukata bando lako kwa kuhesabu SMS zilizoingia

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kuna hili jambo limekuwa linanitatiza kwa muda mrefu.

Mimi siyo mtumaji sana wa SMS, unakuta napata SMS 100 au zaidi katika bando la mwezi. Unashangaa mwezi haujafika wananiambia SMS zangu zimeisha wakaki najua kabisa sijatuma idadi hiyo ya SMS ndani ya muda huo.

Njia pekee ya kufikisha idadi higo ya SMS ni kama wahesabu na zile SMS zilizoingia katika simu yangu.

Swali ni je, ni sahihi kuhesabu SMS zilizoingia kama sehemu ya bando alilolipia mtu? Hii ina tofauti gani na kumkata mtu dakika kwa muda ambao amepigiwa yeye simu?
 
Duh aiseee wezi sana
Leo baada ya kutuma post hii nimefanya kuhesabu msg zangu zote maana sipendagi kutoa lawama bila vithibitisho. Nimekuta zilikuwa zimefika aisee!

Ingawa siku za nyuma pia nilikuwa nahisi kama bando lilikuwa linakata bila kumaliza hizo SMS, embu ngoja niahirishe kwanza tuhuma hizi hadi nitakapopata ushahidi usio na shaka.
 
Back
Top Bottom