UDENYE
JF-Expert Member
- Mar 17, 2016
- 318
- 201
Wadau kwa mara nyengine tena jana tarehe mosi ya mwezi June 2024, kampuni ya DSTV inayomiliki haki ya kipekee ya kuonyesha matangazo ya moja ya mashindano ya ligi barani ulaya ,na khususan Uingereza na ligi ya mabingwa wa ulaya, wamefanya tena wizi wao dhidi ya walala hoi wa Tanganyika na Zenj.
Mtanange wa fainali baina ya magwiji kutoka Madrid na Dortmund ukiwa unaendelea, kati kati ya sherehe, wadau hao kwa makusudi waliamua kukata matangazo hayo kwenye vin'gamuzi kadhaa bila kujali maokoto ambayo washakusanya kama malipo ya vinga'amuzi hivyo wala kujali kuwa muda wa maongezi uliosalia wa wananzego. Kana kwamba haitoshi wajuba hao walipopigiwa simu na wadau kadhaa wa mabanda ya kuonyesha burudani hiyo ya kandanda walitowa majibu mepesi ya kiwango cha huduma katika ofisi za sirikali.
Baadhi ya majibu nayanukulu hapa "Huu sasa hivi sio muda wa kazi hivyo mtutafute Jumatatu ya tarehe 3 mwezi huu",Mwisho wa kunukulu,
Sasa kwa niaba ya kina ujugu na kwa niaba ya watanganyika na wazenj wanaolazimika kutumia huduma hiyo mbovu kwa miaka kadhaa sasa, tunaomba Mama Samiya Raisi wetu msikivu aingilie kati na ikiwezekana waziri muhusika wa tasnia hiyo ajambishwe kidogo ili ashughulikie kero hii ya muda mrefu sasa. kama vipi wananzengo wapewe ruksa kujipachikia madishi yao ya magumashi kunasa mubashara mitanange hiyo, kuondokana na ugaigai wa hawa makaburu.
Kwa wadau kama kina ujugu, mechi kama hizi za fainali ndo wanazofunga hesabu na ada za watoto, pango za kumbi na nyumba zao ndio zinapopatikana, achilia mbali wadau waliopatwa na taharuki ya kukatishwa kwa matangazo hayo ghafla tena bila sababu za msingi kama umeme wa Tanesco.
Kwa taarifa za ndaaani zilizopo ni kuwa wajuba hao wa DSTV ambao hutumia mbinu hiyo hata kwenye zile mechi za dabi na magiant ya soka huko Ungereza kujiongezea kipato cha haraka cha Dhulma hasa kutoka kwa wale wadau wasiopenda ngonjera.
Chonde chonde wizara husika tunaomba ukiritimba huu mtuondelee, leteni kampuni zaidi ya mbili za kurusha matangazo ya soka mibashara, ili kuleta ushindani na kuboresha huduma, ama mruhusu vishoka watupachikie midishi ya Arabuni tujinafasi mubashara kutoka duniani.
DSTv Wameshashindwa zamani wamebaki na vioja badala ya hoja.
Naomba kuwasilisha
Mwananzego kutoka pande za Vikindu.