Wizi Serikalini: Wabunge wanawakwepa Mawaziri na Makatibu Wakuu makusudi?

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Msimu huu wa bunge umetawaliwa na taarifa ya CAG ambayo inaonesha wizi mkubwa serikalini. Tatizo malalamiko ya wabunge yanalenga taasisi za serikali na watendaji wake bila kuwataja mawaziri ambao ni wabunge wenzao. Ukweli ni kwamba mawaziri wote wa serikali ya rais Samia wanashindana kuiba pesa za serikali.

Kuna uhakika kwamba waziri wa kilimo anajenga vituo 11 vya mafuta ktk njia ya Kibaha hadi Chalinze. Waziri wa maji yeye ameshatajwa kuiba pesa inayorudishwa kwenye mabonde kwa ajili ya kazi mbali mbali na tatizo kubwa imekuwa ni ushirikianio uliopo kati ya PCCB na hao wanaohisiwa ktk wizi.

Waziri wa fedha ndo hivyo tena na biashara za kununua mabasi rundo na kuyaweka ndani ya kampuni za usafirishaji.

Waziri wa ujenzi anaendesha kampuni ndani ya wizara na pale dodoma sasa naye yuko kwenye tenda za ujenzi wa uwanjka wa ndege wa Msalato.

Pale UDOM kuna shopping Mall ambalo tunaambiwa ni rais wa nchi anjenga; mtu ambaye kisha sema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Kwa ujumla hatuna serikali. Tangu juu hadi chini ni mashindano ya wizi. Mitandaoni wamewekwa wapambe kutetea wizi huo kwa kuomba ushahidi.

Bungeni wanashambuliwa watendaji wa taasisi tu. Taasisi haiwezi kuwa na wizi bila waziri na katibu mkuu kuruhusu.
 
Kwa kweli wizi tunaoshuhudia huku Serikalini ni kama nchi haina mipaka. Kama rais naye anahangaikia biashara ya shopping Mall, nani alinde nchi? NI sawa na familia ya vibaka tu. Jioni kila mtu anafurahia wizi wa mwenzake.
 
Mpinzani wa CCM ni ccm wenyewe maana sijawahi kuwaelewa kuanzia bungeni mpaka kwenye kampeni zao!
 
Walimtanguliza ili wayafanye haya mana aliwabana sana...ndio mana yule nyape alisema upepo umetulia bahari ni shwari kwa kutafuna rasilmali za nchi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Lisemwalo lipo.. Kwa Bashe wala stoshangaa. Kama ambavyo si shangai ya Mwigulu alie tuambia tuhamie Burundi.
 
Lisemwalo lipo.. Kwa Bashe wala stoshangaa. Kama ambavyo si shangai ya Mwigulu alie tuambia tuhamie Burundi.
Nimewaangalia waingereza na mtihani wa kuwa na PM mhindi, nimeelewa kwamba kila nchi ina ubaguzi kwa kazi za aina fulani. Ni aibu kuwa na msomali Bashe kama waziri. Hii inaumiza watu kuisikia lakini huo ndo ukweli kwamba ni watu wanaoweza kuhama wakati wowote bila uchungu, hata kama kazaliwa Kahama.
 
Serikali hii ikiondoka itakuwa ya kwanza watendaji wote kuazia kichwani hadi unyayoni watavuliwa kinga na kushitakiwa wote kwa uhujumu uchumi na hapatakuwa na nafasi ya 'Plea Bargain'
 

Nahisi haya ni machache ambayo umeyasikia. Kwenye umeme hiyo mikataba, madini, maliasili, nk. hatujasikia
Muhimu tukumbuke maneno ya kiswahili-swahili ya rais Kila mtu kwa urefu wa kamba yake:

Your browser is not able to display this video.

Asiyeamini udhaifu wa rais wetu aingie hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…