Kumbe wizi wa CRDB part II ni Kimei must go
you sound like a disgraced former CRDB employee
Kimei anakunyima usingizi.
Angalia makato ya CRDB kulinganisha na benki nyingine haswaa NMB.
Mleta anachuki binafsi na CRDB na huu uzi ni mahususi kwa KUICHAFUA BENKI HIYO.
Kimei hana jipya...umeona benki inavyokuwa.
Au kwasababu alikataa kupokea vimemo vya kuzuia mnada wa nyumba za mzee wa msituni.
Tuache unafiki.
Huyu jamaa hata kama atakuwa na lake jambo, ukweli unabaki palepale kwamba Kumkata mteja sh 700 anapotoa hela kwenye atm, na sh 200 kila anapouliza salio ni unyonyaji. CRDB iwekeze hela za wateja ili ipate faida lakini sio kumkata mteja hata kwenye transaction za kawaida za kila siku. Ukitoa hela kwenye atm mara 10 kwa wiki au mwezi ujue umeliwa 7000. ukiangalia salio mara 10 tayari 2000 imekwenda. hapohapo kila mwezi kuna fee gani sijui sh 4000. Huu ni unyonyaji.
Benk ya Barclays, kutoa hela na kuangalio salio kwenye atm ni bure haijalishi umefanya mara ngapi. na mwisho wa mwezi unakatwa 2000 tu.
CRDB hawafai kabisa mie nimetoka kabisa. Nimefunga akaunti yangu hivi majuzi japo walinibembeleza sana kwa nini unachota hela na kufunga akaunti nikawadanganya naenda kusoma Masters Norway. Walikoamaa kwamba hata huko nje naweza tumia huduma zao kwa kutumia viza yangu nikawaambia NO. Naenda kuanza mambo yangu yote upya wakaufyata nikachomao changu na kusepaaaaaaaa. kiukweli charges zao zipo juu sana. hakuna benk yoyote ya kawaida inacharrge sh 1500 ya kuendesha akaunti kwa mwezi zaidi ya CRDB
Equity bank hawana charges za kutunza helaBila shaka mleta uzi hapa ana hoja, lakini alipaswa kueleza bank ipi haina charges, hasa withdrawal na kama anadhani zingine ni nafuu bora ahamie bank nyingine. Sioni sababu ya kumshambulia, maana hiyo haijengi hoja. Lakini ninavyojua uwepo wa charges kwenye bank ni kawaida, hata nikiulizia salio kupitia simbanking bado nachajiwa pia (?). Niulize tu mleta uzi endapo hizi charges ni hidden charges ama ziko well articulated kwenye info packs za crdb
Labda niwambie wanajamvi, kwangu wizi ingekuwa kama amekuta hela zimechotwa kwa akaunti yake bila kuwa na taarifa, ama wamemchaji hela ambazo hazijui hata baada ya kuuliza hajapata maelezo ya kina
Soma home yaani ww ulichoona ni Kimei must go. Badala ya point; kweli elimu ni kila kitu.Kumbe wizi wa CRDB part II ni Kimei must go
you sound like a disgraced former CRDB employee
Hongera sana kaka, mfumo wa soko huria unalengo la kuchochea ushindani ili upatikane unafuu kwa wateja/walaji....0 nikaenda kuangalia nikakutana na 11000 nikaomba bank statement baada ya hapo kilichofuatia nikaenda kufungua account bank nyingine
ATM wamekodi ...! I Guess.Haiwezekani, CRDB wanasema kila mwaka wanapata faida in billions of money kumbe ni kuwakata wateja wao charges tena za kutoa pesa kwenye ATMs. Wezi wakubwa hawa.
Natoa Hoja!
MkuuNilitoa maada kuhusu Wizi wa CRDB na nimesoma reactions za wana JF. Nimepata furaha sana kwa sababu nimegundua wachangiaji wana mawazo tofauti sana. Wengine ni kejeli na wengine wanaona kama wana pesa nyingi kwahiyo hiyo shs. 700/= kwa kila withdraw sio issue. Lakini niseme kwamba mitandao kama hii ya JF ni kusaidia jamii kwa mambo mengi sana mojawapo ni kuelimisha au kukemea.
Sasa baada yaku-sample maoni ya wachangiaji, ninaleta hii hoja upya kama Wizi wa CRDB Part II.
Itabidi nirudi darasani nianze kufundisha upya tena kwa sababu ninaona watu wengine hata hawajui maana ya kusema CRDB ni wezi. Bank inakusanya deposits kutoka kwa wateja ili ifanye biashara na kufanya biashara sio kutoza charges ambazo hazina maana yo yote.
Ledger fee is okay, lakini sio kila withdraw unakatwa pesa. CRDB imeshindwa hata kuvuka mipaka na kwenda kufanya biashara inakalia kuwanyonya maskini wa kitanzania. Eti CRDB ina tawi nchini Burundi, kila mtu anajua uchumi wa Burundi is very poor, wananchi wake is very poor, huko kwa maskini ndiko CRDB inafungua matawi. Mbona wasiende Kenya, Uganda, Rwanda au hata Kusini mwa Afrika? Jibu ni moja, hawajui biashara za ki-bank, wao wamekalia kukata watu fedha za wizi.
Halafu mwisho wa mwaka wanasema wamepata faida ya billions of money, from what businesses? Kwahiyo hata nyie watetezi wa CRDB ni vizuri mjue kuwa CRDB hawafanyi biashara ya ki-bank, biashara ya ki-bank sio kuishi kwa kukata depositors so many charges, biashara ya ki-bank ni kuchukua deposits kutoka kwa wateja then unatoa mikopo, which in turn will give you interests ambayo sasa ni income yako.
Ndugu watanzania wakati ni sasa, hebu tuamke tuseme unyonyaji sasa basi. Hapa tunazungumzia CRDB lakini ninajua Mabank yote mchezo ni huu huu. Huko Kenya, ukiwa na tabia ya akina CRDB wateja wanaondoka. Hebu angalia bank za Kenya zilivyosambaa Tanzania utafikiri ni kama m-pesa, huoni KCB, Equity, CBA, NIC, nyingi tu. Nenda Kenya huoni bank yo yote ya ki-bongo. Hapa wa-TZ tutasema wakenya ni wabaguzi, sio kweli kabisa, ukweli ni kuwa bank za ki-bongo hazijui biashara za ki-bank full stop. Tuache kulia kulia kama watoto wa fisi, miaka 50 ya uhuru kilio ni kile kile.
Hao wanaosema, eti kama unaona CRDB inaiba hamisha pesa yako, wana mawazo mgando. Kwani ukiwa na mke au mume mwenye tabia inayoenda kinyume unamuacha? Basi utaoa au kuolewa kila siku. Let us fight from within. CRDB is a public bank, hakuna wa kuondoka ila tutamulika sera zao za wizi na uvivu wa kufikiri. Nao Kimei ame-overstay and he must leave. He has out-lived his ideas. Hana jipya, aondoke. Kimei Must Go. Kimei Must Go. Kimei Must Go. Kimei Must Go. Kimei Must Go.
Haiwezekani, CRDB wanasema kila mwaka wanapata faida in billions of money kumbe ni kuwakata wateja wao charges tena za kutoa pesa kwenye ATMs. Wezi wakubwa hawa.
Natoa Hoja!
Hahaha..Vodacom na wao wapewe za mbavu sio??Ukitosha watandike nyundo Vodacom , vifurushi vya chuo wanawabana mno watu wa chini.