Wizi wa Bank ya CRDB Part II

Wizi wa Bank ya CRDB Part II

Status
Not open for further replies.
Nahisi watu wamegoma kuekewa kwan wanadhan we unahamisisha huduma ziwe za buree.
Mweee wa Tz ni wa bishi kuekewaaa ingawa wanaelewaaa
 
Ila kweli charge zimekuwa too much. Ukitoa million moja kwenye atm unakatwa 2,100. Naona wanataka kurudisha foleni ndani tu hawa.
 
Kumbe wizi wa CRDB part II ni Kimei must go

you sound like a disgraced former CRDB employee


Mleta uzi huu juu ya charges za CRDB ana hoja nzito ambayo hata BOT wanatakiwa kuifanyia kazi. Benki nyingi hapa Tanzania na hasa za kibongo hazifanyi kazi za kibenki kwa ufanisi na hivyo faida wanayoipata kila mwaka inatokana na TOZO[ charges] ambazo nyingine kusema kweli hazina maana; kwa nmfano charges za kutoa pesa kutoka kwenye akaunti ya mteja ni unyonyaji wa dhahili kabisa ukifahamu kuwa wateja tunalipa ledger fees kila mwezi!!! Sioni mantiki ya mteja kulipa tozo kwa kutoa pesa yake benki!!
 
Mtoa hoja una hoja japo watu wengi hawajakuelewa. Tujiulize hivi ni kwa nini benki zetu mfano CRDB hazijitanui ktk nchi za SADC na EAC. huenda ni Sera au sheria au kukosa uthubutu. Suala la kuhama benki ni ushauri mzuri Lakini hauna mantiki. Kwenye jamii lazima baadhi ya watu wajigeuze reli ili treni ipite. Huko kwenye nchi za dunia ya kwanza wateja huwa wanajihami kwa kuanzisha vyama Imara ili kulinda maslahi yao. Mfano chama cha wateja wa taasisi za fedha, chama cha wavuta sigara n.k. Waingereza husema "for every effect there is a cause"
 
Mleta mada uko sahihi sasa hivi mabenki yanatoza gharama ambazo hazieleweki wala hazina maelezo maalumu.

Tena benk nyingi zinamakato yanayoelekeana , Sema watanzania wengi sio wafuatiliaji wa benki statement.

Ila siku ukiamua kufuatilia makato ya ki benk unaweza kuondoka na Pesa yako ukaenda kuichimbia nyumbani.

Mimi sio mteja wa CRDB, ila nina account benk tatu tofauti.

Watanzania tujenge mazoea ya kuomba benk statement walau kila mwezi kama huwezi dai hata baada ya miezi mitatu.

Naamini wengi mtakuja kuungana na mleta mada, uendeshaji wa benk Tanzania Hauna tofauti na mitandao ya simu.
 
Kimei anakunyima usingizi.
Angalia makato ya CRDB kulinganisha na benki nyingine haswaa NMB.
Mleta anachuki binafsi na CRDB na huu uzi ni mahususi kwa KUICHAFUA BENKI HIYO.
Kimei hana jipya...umeona benki inavyokuwa.
Au kwasababu alikataa kupokea vimemo vya kuzuia mnada wa nyumba za mzee wa msituni.
Tuache unafiki.

CRDB hawafai kabisa mie nimetoka kabisa. Nimefunga akaunti yangu hivi majuzi japo walinibembeleza sana kwa nini unachota hela na kufunga akaunti nikawadanganya naenda kusoma Masters Norway. Walikoamaa kwamba hata huko nje naweza tumia huduma zao kwa kutumia viza yangu nikawaambia NO. Naenda kuanza mambo yangu yote upya wakaufyata nikachomao changu na kusepaaaaaaaa. kiukweli charges zao zipo juu sana. hakuna benk yoyote ya kawaida inacharrge sh 1500 ya kuendesha akaunti kwa mwezi zaidi ya CRDB
 
Huyu jamaa hata kama atakuwa na lake jambo, ukweli unabaki palepale kwamba Kumkata mteja sh 700 anapotoa hela kwenye atm, na sh 200 kila anapouliza salio ni unyonyaji. CRDB iwekeze hela za wateja ili ipate faida lakini sio kumkata mteja hata kwenye transaction za kawaida za kila siku. Ukitoa hela kwenye atm mara 10 kwa wiki au mwezi ujue umeliwa 7000. ukiangalia salio mara 10 tayari 2000 imekwenda. hapohapo kila mwezi kuna fee gani sijui sh 4000. Huu ni unyonyaji.


Benk ya Barclays, kutoa hela na kuangalio salio kwenye atm ni bure haijalishi umefanya mara ngapi. na mwisho wa mwezi unakatwa 2000 tu.

nakubakiana na wewe
 
CRDB hawafai kabisa mie nimetoka kabisa. Nimefunga akaunti yangu hivi majuzi japo walinibembeleza sana kwa nini unachota hela na kufunga akaunti nikawadanganya naenda kusoma Masters Norway. Walikoamaa kwamba hata huko nje naweza tumia huduma zao kwa kutumia viza yangu nikawaambia NO. Naenda kuanza mambo yangu yote upya wakaufyata nikachomao changu na kusepaaaaaaaa. kiukweli charges zao zipo juu sana. hakuna benk yoyote ya kawaida inacharrge sh 1500 ya kuendesha akaunti kwa mwezi zaidi ya CRDB

Ulikuwa na sh. ngapi mkuu kama hiyo 1500 unaiona kubwa.
 
Bila shaka mleta uzi hapa ana hoja, lakini alipaswa kueleza bank ipi haina charges, hasa withdrawal na kama anadhani zingine ni nafuu bora ahamie bank nyingine. Sioni sababu ya kumshambulia, maana hiyo haijengi hoja. Lakini ninavyojua uwepo wa charges kwenye bank ni kawaida, hata nikiulizia salio kupitia simbanking bado nachajiwa pia (?). Niulize tu mleta uzi endapo hizi charges ni hidden charges ama ziko well articulated kwenye info packs za crdb
Labda niwambie wanajamvi, kwangu wizi ingekuwa kama amekuta hela zimechotwa kwa akaunti yake bila kuwa na taarifa, ama wamemchaji hela ambazo hazijui hata baada ya kuuliza hajapata maelezo ya kina
Equity bank hawana charges za kutunza hela
 
Yaaani Kuna Siku Nilidata Mwenyewe
nilideposit 50,000 kwa simu mwisho wa mwezi nikaenda kuangalia nikakutana na 11,000 nikaomba bank statement baada ya hapo kilichofuatia nikaenda kufungua account bank nyingine.

Pesa ya kwangu halafu ninyanyasike mwenyewe, aaaaarrrrrrrrrrg akuuu siwezi kwakweli
 
...0 nikaenda kuangalia nikakutana na 11000 nikaomba bank statement baada ya hapo kilichofuatia nikaenda kufungua account bank nyingine
Hongera sana kaka, mfumo wa soko huria unalengo la kuchochea ushindani ili upatikane unafuu kwa wateja/walaji.

Kwa kiasi kikubwa huduma za benki zetu nyingi hasa zile ambazo tunazimiliki wenyewe(watz) na kwenye menejimenti tupo wenyewe zinakuwa na uendeshaji wenye kukwaza wateja.

Jambo la msingi ni kuhakikisha tunaishi kwa ku-reason
 
CRDB,
Afisa Mahusiano wa CRDB/ Customer Manager,
Hakikisha unachukua hizo hoja na kuziwasilisha kwenye vikao vya Management, myafanyie kazi na kuonyesha kujali hasa mnapopewa dukuduku kama hizi, hata kama zingine siyo sawa lakini kiujumla kuna wachangiaji wameonyesha kuumizwa na makato yenu.

Mimi ni Mteja wenu tena mwenye Account 5, Ya Co. na za binafsi na ni Premium Member, Nimeona makato yenu ni makubwa ukilinganisha na uhalisia wenyewe, Kukua kwenu kutategemea mnajisahihisha vipi kwenye makosa mnayoambiwa au mnayoyagundua wenyewe.

Kwa sisi ambao hatujasomea Accounting & Finance, we look blindly on charges..kwahiyo ni vizuri mtutendee haki kwa kuorodhesha charges zenu zote kwenye vipeperushi na kwenye website yenu ili itupe picha halisi tunapofanya transaction zetu tunakatwa kiasi gani..Kwa mfano Premium member tunaambiwa tu kwa mdomo utakatwa 17,000 kwa mwezi, lakini utakuta unakatwa 22,300 kwa mwezi, kwanini msiyaweke wazi hayo kwenye vipeperushi vyenu.

Ni kweli bila ubishi mnahudumia wateja vizuri lakini muwe wepesi wa kujibu hoja kama hizi tena kwa uwazi.

Msilazimishe wateja waanze kufikiri kuhamia bank nyingine kwa mamabo ambayo yako ndani ya uwezo wenu, Yafanyieni kazi na kama hayana majibu kwenye Management yapelekeni kwenye Bodi na Kwenye Vikao vya Wanahisa.

Ndaga.
 
Haiwezekani, CRDB wanasema kila mwaka wanapata faida in billions of money kumbe ni kuwakata wateja wao charges tena za kutoa pesa kwenye ATMs. Wezi wakubwa hawa.
Natoa Hoja!
ATM wamekodi ...! I Guess.
 
Nilitoa maada kuhusu Wizi wa CRDB na nimesoma reactions za wana JF. Nimepata furaha sana kwa sababu nimegundua wachangiaji wana mawazo tofauti sana. Wengine ni kejeli na wengine wanaona kama wana pesa nyingi kwahiyo hiyo shs. 700/= kwa kila withdraw sio issue. Lakini niseme kwamba mitandao kama hii ya JF ni kusaidia jamii kwa mambo mengi sana mojawapo ni kuelimisha au kukemea.
Sasa baada yaku-sample maoni ya wachangiaji, ninaleta hii hoja upya kama Wizi wa CRDB Part II.
Itabidi nirudi darasani nianze kufundisha upya tena kwa sababu ninaona watu wengine hata hawajui maana ya kusema CRDB ni wezi. Bank inakusanya deposits kutoka kwa wateja ili ifanye biashara na kufanya biashara sio kutoza charges ambazo hazina maana yo yote.

Ledger fee is okay, lakini sio kila withdraw unakatwa pesa. CRDB imeshindwa hata kuvuka mipaka na kwenda kufanya biashara inakalia kuwanyonya maskini wa kitanzania. Eti CRDB ina tawi nchini Burundi, kila mtu anajua uchumi wa Burundi is very poor, wananchi wake is very poor, huko kwa maskini ndiko CRDB inafungua matawi. Mbona wasiende Kenya, Uganda, Rwanda au hata Kusini mwa Afrika? Jibu ni moja, hawajui biashara za ki-bank, wao wamekalia kukata watu fedha za wizi.

Halafu mwisho wa mwaka wanasema wamepata faida ya billions of money, from what businesses? Kwahiyo hata nyie watetezi wa CRDB ni vizuri mjue kuwa CRDB hawafanyi biashara ya ki-bank, biashara ya ki-bank sio kuishi kwa kukata depositors so many charges, biashara ya ki-bank ni kuchukua deposits kutoka kwa wateja then unatoa mikopo, which in turn will give you interests ambayo sasa ni income yako.
Ndugu watanzania wakati ni sasa, hebu tuamke tuseme unyonyaji sasa basi. Hapa tunazungumzia CRDB lakini ninajua Mabank yote mchezo ni huu huu. Huko Kenya, ukiwa na tabia ya akina CRDB wateja wanaondoka. Hebu angalia bank za Kenya zilivyosambaa Tanzania utafikiri ni kama m-pesa, huoni KCB, Equity, CBA, NIC, nyingi tu. Nenda Kenya huoni bank yo yote ya ki-bongo. Hapa wa-TZ tutasema wakenya ni wabaguzi, sio kweli kabisa, ukweli ni kuwa bank za ki-bongo hazijui biashara za ki-bank full stop. Tuache kulia kulia kama watoto wa fisi, miaka 50 ya uhuru kilio ni kile kile.
Hao wanaosema, eti kama unaona CRDB inaiba hamisha pesa yako, wana mawazo mgando. Kwani ukiwa na mke au mume mwenye tabia inayoenda kinyume unamuacha? Basi utaoa au kuolewa kila siku. Let us fight from within. CRDB is a public bank, hakuna wa kuondoka ila tutamulika sera zao za wizi na uvivu wa kufikiri. Nao Kimei ame-overstay and he must leave. He has out-lived his ideas. Hana jipya, aondoke. Kimei Must Go. Kimei Must Go. Kimei Must Go. Kimei Must Go. Kimei Must Go.
Haiwezekani, CRDB wanasema kila mwaka wanapata faida in billions of money kumbe ni kuwakata wateja wao charges tena za kutoa pesa kwenye ATMs. Wezi wakubwa hawa.
Natoa Hoja!
Mkuu

Maajabu Haya ya wizi ni Bongo tu, UKi withdraw unachajiwa, wakati nchi za we zetu ni free, unless uchange atm current.
 
Aisee kwahiyo yjayo hayafurahishi kabisa humo CRDB! Nmefungua account mpya juzi kwao ina maana pesa zangu zitakatwa bila sababu ya msingi
 
Ukitosha watandike nyundo Vodacom , vifurushi vya chuo wanawabana mno watu wa chini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom