Wizi wa Biti za Muziki

Wizi wa Biti za Muziki

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Kwa mtu anayejua muziki vizuri, akiangalia kesi kadhaa amazo zimetokea huko Youtube kwa madai ya kuibiwa biti, akaweza kukubaliana nami kuwa kesi hizo zote ni frivolous na zinatakiwa kuwa zinatupiliwa nje. Sababu kuwa ni kuwa biti zote za muziki zina msingi wa aina moja. Ndiyo maana ingekuwa ni vigumu sana kwa Bob Marley kudai kuwa UB 40 au Lucky Dube walikuwa wakiiba biti zake.

Kufanana kwa mdundo na mkong'osio wa muziki haina maana ya kuibiwa biti, vitu ambavyo mtu anaweza kulalamikia kwenye muzki ni vitu vitatu tu: mashairi (lyrics), melody, na video. Kama kuna mdundo fulani wa vyombo unaoonekana kufanana lakini melody ya muziki wenyewe havifanani, hiyo siyo copyright infringement hata siku moja.

Ingawa copyrights zinaruhuru parts zote za muziki kuwa protected, ila nature ya composition ya muziki inasababisha mambo mengi ambayo watu wanadai kuibiwa biti yasiwe na maana. Kwa mfano kama mtunzi mmoja ametumia scale ya C, halafu akatumia mdundo wa 4/4, kwa tempo ya 120, na pigo lake kuu likawa ni lile la tatu, halafu yale mengine yakawa na ufahifu kama kwenye mjuziki wako huwezi kusema kakuibia biti.

Hiyo ni standard kabisa.
 
Vipi wale wanaoikopi beat kama ilivyo? Na wale wanaoitumia beat ile ile bila maafikiano?
 
Vipi wale wanaoikopi beat kama ilivyo? Na wale wanaoitumia beat ile ile bila maafikiano?

Kukopi ni lazima kuwe na clear evidence ya originality kwa kitu kinachodaiwa kukopiwa. Kama unachodai kuibiwa ni beat ya muziki, inabidi uwe specific maana ya beat ni nini; kama beat maana yake ni mdundo yaani Rhythm, huwezi kusema kakopi ila kama una maana melody na harmony, hapo ndipo kutakuwa na violation hata kama mashairi ni tofauti. Ngoja nikupe mfano, reggae ya UB40 na reggae ya Lucky dube wantumia mdundo mmoja. Lakini wanatumia melodies tofauti na harmony za nyimbo zao ni fofauti pia. Hakuna anayemalalamikia mwenzake kuibiwa beat. Ila wimbo wa You got me wa UB 40 ulitumia mashariri na melody ya Cher na Sonny. Kama wasingekuwa na makubaliano, hapo ungesema kuwa UB40 walikopi ingawa wao walitumia rhthyms na harmony tofauti kabisa

Mfano mzuri wa kukopi ni wa wimbo wa Kilwa jazz wa Napenda nipate lau nafasi. Ingawa wimbo huo umetumia mashairi tofauti sana na wimbo wa Mokolo nakokufa wa Lochereau, hapa ni wazi Kilwa Jazz walikopi Melody, rhythm na harmony wakaweka mashairi yao tu. Hiyo ni volataion

Sasa angalia wimbo kama kama huu wa fela kuti halafu ulinganishe na ule wa Manu Dibango. Kwa masikio ya harakaharaka ni wazi hizo ni nyimbo mbili tofauti sana, lakini sasa ukichimbua ndipo utagundua kuwa percussion zao na rhythm yao ni sawa kabisa- one to one, ila zinatofautiana tempo. Dibango anakwenda tempo ya chini wakati Kuti anakwenda na tempo ya juu sana

Hapo huwezi kusema kuwa kuna mtu kakopi bit. Ningekuwa na muda wa kutosha ningeweza kutafuta mifano zaidi ya kuonyesha kukopi na kutokopi. Michael Jackson katika wimbo wake huu wa "Wanna Starting' Something" kuanzia dakika 4:44 ametumia maneno "mama-say-mama-say-mama-coosa mama-say-mama-say-mama-coosa " ambayo ni kopi ya Manu Dibango ya "mamako mamase makomakusa mamako mamase makomakusa mamako mamase makusa"

Ingawa nyimbo zao ni tofauti kabisa kwa rhythm, melody, harmony na hata mashairi yenyewe, ila kipande hicho alichokopi ni distinct sana na hivyo kufanya hiyo iwe ni infringement. Ni jambo la ajabu kuwa ilimchukua Dibando zaidi ya miaka 30 kutambua infingement hiyo na kumshitaki Michael (na Rihanna). The Strange Story of “Mama Say Mama Sa Mama Coosa” « American Songwriter

Nyimbo zote ambazo nimeona zilalamikiwa huku kwetu unakuta tu kuwa kuna sehemu fulani za vyombo zinafanana (wanayoita sample) lakini bado mtu analalamika kuwa kaniibia beat yangu wakati hakuna kitu distinct kuonyesha originality ya kinachodaiwa kukopiwa. Ukiangalia program zote za kutengenezea Muziki za siku hizi (Dr. drum, Ableton Live, FL Studio, Dub turb0, n.k) zinazotumiwa na wanamuziki mbalimbali nazo huja na samples kibao. Sasa kama watunzi kadhaa wametumia samles hizo hizo na kwa scale ile ile na tempo ile ile, kuna mtu anaweza kudai kuwa kakopiwa wimbo wake wakati siyo kweli.
 
Kwa mtu anyejua muziki vizuri, akiangalia kesi kadhaa amazo zimetokea huko Yutube kwa madai ya kuibiwa biti, akaweza kukubaliana nami kuwa kesi hizo zote ni frivolous na zinatakiwa kuwa zinatupiliwa nje. Sababu kuwa ni kuwa biti zote za muzikii zina msingi wa aina moja. Ndiyo maana ingekuwa ni vigumu sana kwa Bob Marley kudai kuwa UB 40 au Lucky Wube walikuwa wakiiba biti zake.

Kufanana kwa mdundo na mkong'osio wa muziki haina maana ya kuibiwa biti, vitu ambavyo mtu anaweza kulalamikia kwenye muzki ni vitu vitatu tu: mashairi (lyrics), melody, na video. Kama kuna mdundo fulani wa vyombo unaoonekana kufanana lakini melody ya muziki wenyewe havifanani, hiyo siyo copyright infringement hata siku moja.

Ingawa copyrights zinaruhuru parts zote za muziki kuwa protected, ila nature ya composition ya muziki inasababisha mambo mengi ambayo watu wanadai kuibiwa biti yasiwe na maana. Kwa mfano kama mtunzi mmoja ametumia scale ya C, halafu akatumia mdundo wa 4/4, kwa tempo ya 120, na pigo lake kuu likawa ni lile la tatu, halafu yale mengine yakawa na ufahifu kama kwenye mjuziki wako huwezi kusema kakuibia biti.

Hiyo ni standard kabisa.
Mkuu unamaanisha hakuna anayekwiba kwa sababu hicho cha kuiba hakipo au?
 
Mkuu unamaanisha hakuna anayekwiba kwa sababu hicho cha kuiba hakipo au?
Swali zuri; kitu kinachoibiwa ni ile "creation" ya mwanamuziki; yaani tungo ambazo ni dhahiri. Kusikika kama kuna vyombo fulani vinavyotoa sauti zinazofanana kwenye wimbo hata kwa sipidi (tempo) siyo jambo linaloibiwa iwapo tungo zenyewe ni tofauti kabisa kwa wasikilizaji.

Kuna jamaa mmoja hapo Kenya amekuwa anakurupukia watu mbalimbali, siyo watanzania tu bali hata wamarekani, kudai kuwa wameiba biti zake jambo ambalo siyo kweli kabisa; huwa ni hisia zake tu.
 
Kukopi ni lazima kuwe na clear evidence ya originality kwa kitu kinachodaiwa kukopiwa. Kama unachodai kuibiwa ni beat ya muziki,
Inabidi uwe specific maana ya beat ni nini; kama beat maana yake ni mdundo yaani Rhythm, huwezi kusema kakopi ila kama una maana melody na harmony, hapo ndipo kutakuwa na violation hata kama mashairi ni tofauti. Ngoja nikupe mfano, reggae ya UB40 na reggae ya Lucky dube wantumia mdundo mmoja. Lakini wanatumia melodies tofauti na harmony za nyimbo zao ni fofauti pia. hakuna anayemalalamikia mwenzake kuibiwa bit. Ila wimbo wa You got me wa UB 40 ulitumia mashariri na melody ya Cher na Sonny. Kama wasingekuwa na makubalianoi, hapo ungezema kuwa UB40 walikopi ingawa wao walitumia beat tofauti kabisa

Mfano mzuri wa kukopi ni wa wimbo wa Kilwa jazz wa Napenda nipate lau nafasi. Ingawa wimbo huo umetumia mashairi tofauto sana na wimbo wa Mokolo nakokufa wa Lochreau, hapa ni wazi Kilwa Jazz walikopi Melody, rhythm na harmony wakaweka mashairi yao tu. Hiyo ni volataion

Sasa angalia wimbo kama kama huu wa fela kuti halafu ulinganishe na ule wa Manu Dibango. kwa masikio ya harakaharaka ni wazi hizo ni nyimbo mbili tofauti sana, lakini sasa ukichimbua ndipo utagundua kuwa percussion zao na rhythm yao ni sawa kabisa- one to one, ila zinatofautiana tempo. Dibango anakwenda tempo ya chini wakati Kuti anakwenda na tempo ya juu sana

Hapo huwezi kusema nakuwa kuna mtu kakopi bit. Ningekuwa na muda wa kutosha ningeweza kutafuta mifano zaidi ya kuonyesha kukopi na kutokopi. Michale Jackson katika wimbo wake huu amateumia maneno "mama-say-mama-sa-mama-coosa " ambayo
ni kopi ya ya Manu Dibango ya "mamako mamase makomakusa mamako mamase makomakusa mamako mamase makusa:

Ingwa nyimbo zao ni tofauti kabisa kwa rhythm, melody, harmony na hata mashairi yenyewe, ila kipande hicho alichokopi ni distinct sana na hivyo kufanya hiyo iwe ni infringement. Ni jambo la ajabu kuwa ilimchukua Dibando zaidi ya miaka 30 kutambua infingement hiyo na kumhsitaki Michael (na Rihanna). The Strange Story of “Mama Say Mama Sa Mama Coosa” « American Songwriter

Nyimbo zote ambazo nimeona zilalamikiwa huku kwetu unakuta tu kuwa kuna sehemu fulani za vyombo zinafanana (wanayoita sample) lakini bado mtu analalamika kuwa kaniibia beat yangu wakati hakuna kittu distinct kuonyesha originality ya kinachodaiwa kukopiwa. Ukiangalia program zote za kutengenezea Muziki za siku hizi (Dr. drum, Ableton Live, FL Studio, Dub turb0, n.k) zinazotumiwa na wanamuziki mbalimbali nazo huja na samples kibao. Sasa kama watunzi kadhaa wametumia samles hizo hizo na kwa scale ile ile na tempo ile ile, kuna mtu anaweza kudai kuwa kakopiwa wimbo wake wakati siyo kweli.
Nashukuru mkuu kwa darasa hili kubwa nimekupata vema.
 
Swali zuri; kitu kinachoibiwa ni ile "creation" ya mwanamuziki; yaani tungo ambazo ni dhahiri. Kusikika kama kuna vyombo fulani vinavyotoa sauti zinazofanana kwenye wimbo hata kwa sipidi (tempo) siyo jambo linaloibiwa iwapo tungo zenyewe ni tofauti kabisa kwa wasikilizaji.

Kuna jamaa mmoja hapo Kenya amekuwa anakurupukia watu mbalimbali, siyo watanzania tu bali hata wamarekani, kudai kuwa wameiba biti zake jambo ambalo siyo kweli kabisa; huwa ni hisia zake tu.
Mkuu...soma case ya Christina Milian kuhusu beat ya "Deep it low" uongeze maarifa zaidi.
 
Mkuu...soma case ya Christina Milian kuhusu beat ya "Deep it low" uongeze maarifa zaidi.
Kesi ile haifanani na haya malalamiko frivolous ninayosikia siku hizi huku kwetu. Wimbo uliolalamikiwa ulichukua sample ya sekunde 12 kutoka wimbo wa mtu mwingine na kurudia rurudia hiyo sample katika kujenga wimbo wote. Na maana ya "sample" ni kipande kamili cha wimbo siyo "sehemu ya vyombo" tu; kipande hicho kilikuwa na element za mdundo, harmony na melody; ingawa mashairi yalikuwa tofauti. Kosa lake kubwa ni kuwa hakukuwa na ongezeko lolote kwenye kipande kilichokopiwa, alikichukua one to one, na hivyo kuwa provable kuwa kuna kazi ya mtu mwingine ndiyo imetumike kutengeza wimbo huu bila ruhusa ya mwenyewe.
 
Mkuu upo sahihi Ila Kuna mahali nakupinga kwa mfano alichokifanya harmonize kwenye wimbo wa Amen tukitoa huruma ya msiba Ni kweli kakopi beat japokuwa melody na harmony zinatofautiana maana producer katumia ubunifu wake alafu mwingne anachukua Kama ilivo na kutumia bila ruhusa
 
Asante sana; sijui wimbo wa harmonize ukoje, na wa yule aliyedai kuibiwa pia ukoje. Ila sheria inayotawala copyright iko wazi kabisa kuwa ni kazi inayolindwa siyo vipande vya vidogo vidogo vilivyoko kwenye kazi hiyo. Kwa mfano nikiandika kitabu changu ninaweza kutumia maneno yoyote katika uandishi wangu. Maneno hayo yanaweza kutumiwa na mwandishi mwingine tena, tofauti itakuwa ni jinsi nilivyotumia maneno yale kwenye kitabu changu, na ambavyo yule mwingine alivyoyatumia. Iwapo itaonekana kuwa matumzi ya maneno ni marudio ya kazi ya mwingine, basi hapo inakuwa ni violation. Lakini huwezi kumlamamikia mtu eti kwa sababu katika uandishi wake ametumia maneno kama uliyotumia wewe
 
Asante sana; ila sijui wimbo wa hamronize ukoje, na wa yule aliyedai kuibiwa pia ukoke. Ila sheria inatotawala copyright iko wazi kabisa kuwa ni kazi inayolindwa siyo vipande vya vidogo vidogo vilivyoko kwenye kazi hiyo. Kwa mfano nikiandika kitabu changu ninaweza kutumia maneno yoyote katika uandishi wangu. Maneno hayo yanaweza kutumiwa na mwandishi mwingine tena, tofauti itakuwa ni jinsi nilivyotumia maneno yale kwenye kitabu changu, na ambayo yule mwingine alivyoyatumia. Iwapo itaonekana kuwa matumzi ya maneno ni marudio ya kazi ya mwingine, basi hapo inakuwa ni violation. Lakini huwezi kumlamamikia mtu eti kwa sababu katika uandishi wake ametumia maneno kama uliyotumia wewe
Gat you!!
 
Mkuu upo sahihi Ila Kuna mahali nakupinga kwa mfano alichokifanya harmonize kwenye wimbo wa Amen tukitoa huruma ya msiba Ni kweli kakopi beat japokuwa melody na harmony zinatofautiana maana producer katumia ubunifu wake alafu mwingne anachukua Kama ilivo na kutumia bila ruhusa
Nimepata kusikiliza nyimbo zile mbili leo. Samahani kwa kuchelewa kusema hivyo.

Ningekuwa ni mtetezi wa Harmonize huenda angeshinda kesi hiyo kwa sababu hizo ni tungo mbili tofauti kabisa; kinachoonekana kufanana ni rythm tu ambayo huenda producer ndiye anaweza kulalamika iwapo vyombo vyote vina mdundo unaofananana. Ni kweli rythms za nyimbo hizo zinafanana sana kwa vyombo vingi mno. Lakini ni nyimbo mbili tofauti kabisa inapokuja vigezo vingine ambavyo viko protected na sheria
 
Back
Top Bottom