Kimsingi nilipigiwa simu akajitambulisha ni afisa utumishi wangu kutoka niliko hama kuja hapa dar akinisisitizia malipo yangu ninayodai toka mwaka 2017 yametoka hivyo natakiwa kwenda kuchukua barua zangu ofisi ya masijala na kwakuwa niko mbali nikamtuma mshkaji wangu kwenda kufuatilia akajibiwa wewe sio mhusika aje mwenyewe akawajuza kuwa jamaa kahama yupo dar kwasasa.
Wahudumu wa masijalala hawakumsikiliza wala kumpa ushirikiano kilichofuata baada ya siku 4 mbele nikapata tena simu toka kwa afisa huyo akinilink na afisa wa halmashauri niliyopo wakitaka nipele barua ya madai na nilivyofikisha nikampigia akaniambia ametoka niiache masijala ya mkurugenzi.
Baada ya hapo nikapigiwa simu nikisisitizwa kufanya kufanya mazungumzo na mtu aliyejitambulishwa kwangu kama dereva wa halmashauri niliyotoka nimwombe kama itawezekana na kwakuwa magari yapo kwenye kazi maalumu afisa utumishi atajitolea gari lake hivyo dereva huyo atabeba barua zangu kuzipeleka mkoani kwa kulipia mafuta,posho zote za dereva na kwakuwa mshahara ulikuwa karibuni nikakubali nakuanza kufanya miamala na kila hatua tunawasiliana na kuna wakati wanakwama napigiwa simu qakihitaji pesa nakaendelea kutuma mpaka ikafikia 1.350,000/= nikitaarifiwa pesa hiyo nitalipwa mara mbili kwakuwa ulikuwa ni uzembe wa afisa utumishi aliyepita kushughulikia madai hayo kwa haraka.
Kilichokuja kunistua kuwa natapeliwa nilipatq simu kutoka kwa mkuu wangu wa idara akielekezwa na mkurugenzi hayo madai yangu niliyowaandikia barua anayajua? Ndipo nikapigiwa simu nikiwa nyumbani kuulizwa nikaeleza story nzima nikaambiwa hakuna kitu kama hicho kimsingi laiti kama mkurugenzi angep3lekewa barua yangu mapema nisingetqpeliwa hivyo inshu ilikuwa hivyo maelezo najua hayajitoshelezi lakini ni hivyo.
Nb namba zao mpaka leo zinapatikana mwenye kuweza au ushauri tafadhali naombeni msaada maana hata polisi nimeripoti sijapata msaada wowote ule
NAAHIDI ATAKAE NISAIDIA TUWAKAMATE WAHUSIKA DONGE NONO LITATOLEWA NAWAOMBENI SANA MAANA WAMENITESA NA KUNINYANYASA SANA KISAIKOLOJIA