Pre GE2025 Wizi wa kura ni mchakato mrefu, wapinzani mmejipangaje?

Pre GE2025 Wizi wa kura ni mchakato mrefu, wapinzani mmejipangaje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
829
Reaction score
1,120
Tatizo la wapinzani huwa kama kondoo wenye kujipeleka kwenye kundi la simba kuliwa au mbwa kujipeleka kwenye mdomo wa chatu bila kujitetea.

Acheni kulalamika tu mna mbinu gani za kufuatilia na kuzuia msiibiwe kura. Msisubiri hisani ya CCM eti wawape ushindi kwenye sahani. haiwezekani.

Wakeup men
 
Tatizo la wapinzani huwa kama kondoo wenye kujipeleka kwenye kundi la simba kuliwa au mbwa kujipeleka kwenye mdomo wa chatu bila kujitetea. Acheni kulalamika tu mna mbinu gani za kufuatilia na kuzuia msiibiwe kura. Msisubiri hisani ya CCM eti wawape ushindi kwenye sahani. haiwezekani. wakeup men
Hatushiriki chaguzi Kwa tume ya ccm
 
Nimewahi kuwa Wakala wa CHADEMA uchaguzi fulani.

Nilishiriki kuiba kura za vyama vingine Kwa manufaa ya CHADEMA. Na hizi mbinu tulifundishwa kwenye semina.

Sijui ni kwanini CHADEMA wanalalamikia wizi wakati wao ni wezi wakubwa wa kura.
 
Nape kasema ukweli, lkn ccm wamekasirika sana na hivi sasa wanauandalia zengwe. Nape mdomo umemponza.
 
Uchaguzi ujao 2025 hatuibiwi kura na CCM ( chama Cha majambazi ) tunaweka V.A.R 😃😃😃😃😃😃😃
 
Hatushiriki chaguzi Kwa tume ya ccm
Msingi wa umasikini wa taifa umejengeka kwenye fikra.

Tume ya uchaguzi siyo ya chama cha siasa kikatiba, sheria na hata akili ya kawaida tu.

Tatizo siyo CCM, ni tume. Ukimdhibiti mwizi aliyetumwa kuiba kwako, tayari umemdhibiti aliyemtuma kwa wakati huo. Kama tunashindwa kudhibitiana ndani tutaweza vipi ushindani wa kimataifa?

Kuaminiana ndani ni muhimu sana ili kupambana na maadui au washindani wa nje. Vita vya panzi furaha ya kunguru.

Kwa hiyo, wananchi wote wanatakiwa wapewe uelewa wa njia zenye ufanisi kupambana na changamoto badala ya mawazo hasi ya kukata tamaa na kususa.
 
Tatizo la wapinzani huwa kama kondoo wenye kujipeleka kwenye kundi la simba kuliwa au mbwa kujipeleka kwenye mdomo wa chatu bila kujitetea. Acheni kulalamika tu mna mbinu gani za kufuatilia na kuzuia msiibiwe kura. Msisubiri hisani ya CCM eti wawape ushindi kwenye sahani. haiwezekani. wakeup men
Tushauri tufanyeje? Kama ni wewe ungefanyaje! Halafu siyo kila anayepiga kura anapigia chama. Nahisi bado umelala na aliyekupulizia dawa ni CCM. Kura ni uchaguzi. Nakuchagua ni kubagua kati ya unachokihitaji na usichokihitaji hata kama vyote unavipenda. Huwezi kunilazimishe eti nimchague wa CCM, CUF, ACT au Chadema eti Kwa sababu ni chama changu huku nikijua hawezi kufikisha mawazo yangu kunakohusika maana tunachagua wawakilishi siyo viongozi tu. Kwahiyo Kura niliyopiga nina haki kujua imefanya nn imeenda wapi. Kama zimehesabiwa kihalali, hata kama niliyemchagua hajashinda. Kwa uelewa wako wewe unachagua chama ndiyo maana kila mwaka tunapata watu wa kwenda kusinzia bungeni. Kuna wabunge tangu wameenda bungeni miaka 3 na nusu iliyopita huenda wamechangia kila Kikao mara 2. Matatizo yetu tunasemewa na wabunge majirani. Tulia ujifunze maana ya kupiga kura (kuchagua)
 
Wananchi wapewe elimu ya uraia ili wachague mtu bora wa kuwwakilisha kisha wazilinde kura kwa njia za wazi na siri. Iwapo wanasiasa watadiriki kuiba kura kupitia serikali wananchi wataripiza kisasi,na watendaji wanaweza kuingia kwenye shida. Hapa tutakaribisha mahasimu wetu kutoka nje ya nchi kuchochea machafuko kama Kenya.
 
Back
Top Bottom