KERO Wizi wa mita za maji Mbezi Mtaa wa Luis (Upendo)

KERO Wizi wa mita za maji Mbezi Mtaa wa Luis (Upendo)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari za leo,

Ninatokea Mbezi mtaa wa Luis kitongoji cha Upendo.

Hivi karibuni kumeibuka wizi wa mita za maji hapa mtaani kwetu bila kujua wanaoiba wanazipeleka wapi, Dawasa tumewapa taarifa lakini hawana majibu.

Sasa cha kushangaza hizi mita zina namba zake ambazo ni za usajili. Je, hawa watu wanazipeleka wapi? Ama kuna janja janja za watu wa DAWASA kutuuzia mita nyingine kwa namna hiyo?

Pia soma ~ Albert Chalamila: Sijaridhishwa na hiki mlichofanya DAWASA, pia wanaoiba Mita za Maji washughulikiwe
 
Pengine ni mateja wanakwenda kuuza chuma chakavu.

Kama teja anaweza akang'oa mataruma ya reli atashindwa kubeba meter?
 
Maji yenye tangu mwaka Jana mwezi wa tisa hakuna. Acha wapite nazo tu.
 
Back
Top Bottom