Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Mimi ni Mkazi wa Arusha - Moshono, Mtaa wa Nanja, huku kwetu kuna tabia ya wizi wa Mita za Maji kiasi kwamba inakuwa changamoto kupata huduma za maji kwa sababu huwezi kujichukulia Mita mtaani ukaweka, lazima iwe imetoka kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA).
Tukienda kuripoti AUWASA wanatuambia tutoe ripoti Polisi kisha tupeleke ripoti kwao kisha tusubiri kurejeshwa kwa maji.
Ninachojiuliza wanapoiba hizi Mita wanaenda kumuuzia nani? Je, kuna mtu anaweza kufunga Mita ya wizi ambayo hajatoka kwenye mamlaka ya maji? Na je inapofungwa Mamlaka kama AUWSA inaweza kuiingiza kwenye mfumo wake wakati tayari Mita hiyo ilishaingizwa kwenye mfumo awali?