Wizi wa Mtandao wa Kukopa Akiba Commercial Bank

BabbOchu

Member
Joined
Apr 4, 2014
Posts
25
Reaction score
5
Jamani kuna habari zimezagaa mjini kuwa kuna mikopo inatolewa Akiba Commercial Bank, katika pita pita zangu kuna jamaa wameweka namba zao za simu kwamba watu wanatuma pesa za kujiunga na walioweka pesa wote wameliwa.

Kuna link ii apa lakini iyo namba ya Voda si ya ACB
http://akibacommercial-bank.wapka.mobi/index.xhtml


Na katika pita pita kwangu nimekutana na izo attachment jamaa wanatoa namba zao za kutuma izo pesa ambazo katika kuzilinganisha ni namba za simu tofauti na zina majina tofauti ya Izo tigo Pesa na Mpesa. Sasa nataka udhibitisho namba za kweli ni zipi.


Cha Kushangaza zaidi, inakuwaje mpaka sasa hawa jamaa hawajakamatwa na ukipiga simu zao zinapokelewa?

Na inakuwaje Mitandao ya simu iruhusu watu wasajili namba zao kwa kutumia majina ya Kampuni na mpaka leo izo account zinafanya kazi???

Izo picha apo chini hatujui ukweli uko wapi manake kina website imetoa namba zake za tigo/M-pesa kwa ajili ya mkopo huo huo.

Unaweza kusoma zaidi kupitia link izi apa chini:

1- HANDENI KWETU: Zitto Kabwe, aingizwa mtegoni kwa wizi wa mtandaoni?
2- http://akibacommercial-bank.wapka.mobi/index.xhtml
 
Inatakiwa kuwa makini sana na hizi huduma za simu hasa ukizingatia hakuna uhakiki wakati wa kusajiri (mtu unakwenda na photocopy ya kitambulisho chochote na hakuna uhakiki wa hiyo photocopy na kitambulisho halisi hivyo naweza nikatengeza photocopy na kuweka jina la BabbOchu na nikawa napiga hela kwa jina lisilo langu) na makampuni ya simu yamejitoa kabisa ili msala usiwaangukie wao na mbaya zaidi TCRA nayo focus imeweka kwa wateja na simu makampuni maana utasikia usiposajiri mteja unachukuliwa hatua badala ya kuchukulia hatua kampuni ya simu kwa kushindwa kumkatia huduma mteja asiesajiriwa
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…