Wizi wa Mtandaoni umekithiri sana, ndugu yangu alinusurika. Weka kisa chako hapa kuokoa mwingine atakayetaka kutapeliwa kama wewe


Hahahaaaaaaaaaa. Aseeee nimecheka sio poa. Mbinu hii ya kujenga uaminifu kwa mlengwa inatumiwa sana. Wahanga wakubwa wa hii mbinu ni wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo.

Hufanyika kwa namna hii, bwana “X” anajenga uaminifu kwa bwana “z” kwa kumchangia/kununua bidhaa ktk ofisi yake kwa pesa taslimu, baada ya muda flani ataanza kukopa na kulipa, kadri siku zitakavyo yoyoma bwana “Z” atamwamini bwana “X” ni mteja wake mkubwa na mwaminifu kwani hukopa na kulipa. Baada ya imani hiyo kujengeka bwana “X” hutumia fursa hiyo kutengeneza pancha nyingi kadri awezavyo katika mtaji wa bwana “Z” kwakuchukua bidhaa, kutokulipa kwa wakati na mwisho hutokomea kabisa.

Kuepukana na hili, kwa wafanyabiashara wote ni kuwa na marengo ya muda mrefu na mfupi ili kutoruhusu kuendesha biashara kwa hisia na mazoea.

Mi walinijaribu kwa kunipigia simu wakidai wao ni mawakala wa usafilishaji mizigo na vifurushi kutoka kampuni fulani ya mabasi iliyoko Tabora. Walinitaka nifike ofisini kwao kwaajili ya kuchukua mzigo wangu kwani umetumwa muda kitambo na mpaka sasa sijauchukua.

Aliyenipigia simu nilimuuliza maswali matatu ya ufahamu wa chap chap;
1. Mzigo husika umetoka wap?
2. Jina la mtumaji na
3. Namba zake za simu pamoja na namba ya mzigo.

Hakunijibu zaid ya kunitaka kufika ktk ofisi zao kwa taarifa zaidi na kuuchukua mzigo husika. Kwa wakat huo mi nilikuwa Tarime, sina ndugu Tabora wala rafiki na mbaya zaidi sijawai kukaa Tabora. Kitu ambacho kilianza kunifikirisha.

Kwakuwa tamaa juu ya jambo/kitu ambacho si changu ni mwiko, na nafsi yangu ilisita juu ya mzigo husika, hivyo basi, nikafikia maamuzi ya kuachilia mambo yaende kama yalivyokusudiwa. Sikupata ujumbe wowote kutoka kwa ndugu, marafiki na jamaa juu ya mzigo husika wala wahusika wa utapeli hawakuni tafuta mpaka leo hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…