Wizi wa Mtandaoni umekithiri sana, ndugu yangu alinusurika. Weka kisa chako hapa kuokoa mwingine atakayetaka kutapeliwa kama wewe

Wizi wa Mtandaoni umekithiri sana, ndugu yangu alinusurika. Weka kisa chako hapa kuokoa mwingine atakayetaka kutapeliwa kama wewe

2018 nilitapeliwa kwa kujitakia.ilikuwa ni plan ndani ya muda wa miezi 3.ndio nikapigwa elfu 76000/.
Kuna post nilikutana nayo FB Miaka hyo ikielezea msaada wa mgeni kupata usaidizi wa kujua mazingira ya kitarii tanzania,

So nika comment kwa maelezo machache juu y tanzania.baada ya siku kadhaa,nikapata txt kutoka kwa yule mtu alie kuwa akiuliza juu ya tanzania.

Basi tukasalimiana ika isha hivo,baada ya wiki kama mbili.akanitext kwa kuomba email ili tune tunawasiliana kwa email.

Picha ndio likaanza hapo,basi akawa ananitumia email za kujuana zaidi.lakin Huacha sku zpite kama nne au wiki.

Kunasku akanambia anataka kupata nyumba ya kuishi tanzania,kwan anakuja kwaajiri ya kufungua na kuwezesha watoto yatima na wa mtaaani.

Southern Highland mkoa wa mbeya,kwani alisha wahi kutembelea na shirika moja la misaada.

Kwahiyo akahoji kuhusu bei za kupanga nyumba.nikawa na mjibu kwa experience.mwishowe akasema anasafiri toka jimbo moja USA, then atakuja tanzania.lakini akaomba ni mpokee mwenzie ate tangulia tanzania.alatuma email yake nikamcheki.

Movie ndio inaendelea kuiva.basi baada ya kujuana na huyo mwenzie mpya au sijui ndio yuleyule.tukawa tuna chart mambo tofauti tofauti.nakumbuka hapo ni miez miwili inaenda kuisha.


Ngoja nifupishe.tulipo zidi kuwasiliana ndani ya miez mitatu sasa,yule mtu wa kwanza akanambia kama niko jirani na Bandari ya mtwara kunavitu vilitumwa kwajiri ya ofisi nikavipokee.mmmh ishu ikawa hapo akanitumia documents za hizo bidhaa zimetoka Japan lakin vimekaa kwa agent kama miez miwili.
Kwan walipotegemea kuwahikuingia bongo mambo yakawa mengi.


Nikamwambia mimi nko mbali wakati huo nilikuwa safarini toka mbeya to lusaka.

Basi akanambia anitumie namba za agent niweze kumpa address ili vitu nivipokee na kuvitunza hadi watapokuja bongo.

Sasa nilipo fika boda ya tunduma nika piga ile namba niliyo tumiwa.jamaa akajitambulisha ni agent yuko mtwara.akasema eleza shida yako nkamjuza kuna bidhaa za flan hapo akasema kwa mshangao kwan ww ndio ilibidi upokee mbona mmeviacha kwa muda mrefu na kuanza kunipa lawama.utadhani vitu ni vyangu ng'ombe yule.


Akasema nmpe location nkamwambia sasa inasomba boda akasema hapo nirahisi kwa leo kwani kuna ndege ndogo ya cargo inaenda songwe saa 10 jioni.so akasema ngoja alike ofisin aka fanye arrangement.

Baada kama ya lisaa akanipa mtu ambaye ni mdada eti ni secretary na yule mdada akanijuza mzgo unavailable elfu 76.

Nikamwambia mbona umelipiwa akasema nimchek mwenye mzgo nilpo mchek akanambia ngoja awacheki.baada ya muda mwenye mzgo akaniludia na kusema niwatumie hyo 76 kwan muda sio mrefu saa kumi itaingia na mzgo hautaondoka.[printer2,computer1,camera canon]

Nikajaribu kumtafuta mate wangu alikuwa anaishi mtwara,nilipo muelekeza ofisi ya agent ilipo akasema maeneo hayo anapajua ila yy yuko mbali.nikatafuta jamaa angu husema anaishi huko nae akanambia yuko tandahimba.

Basi nikatuma 76 kwan huyu mwenye kujifanya ndio mwenye mzgo alikuwa ananisumbua kwamba tumejuana more than three months alafu nashindwa kumsaidia na ameniamin kutunza mali yake.


Akili ilipokuja shituka Nepalese jamaa alipo nipigia tena na kusema amedakwa Airport.kudai kunabox ambalo waliweka dollars kama 10000/ so police wana mtuhumu kwa usafirishaji wa pesa.akasema nimtumie lak2 awahonge.nkamwambia chukua hzo dollar zote wape naww kama hapo ya Pole.tuma hivo vifaa.


Jamaa akadai hawataki zle wanataka nitume.nkamwambia rudisha mizgo ofisini kwenye ile 76.nenda kainjoi.usinitafute tena.nikarudi kwa yule mwenye mzgo na kuandika neno kubwa F@*K YOU.

Hahahaaaaaaaaaa. Aseeee nimecheka sio poa. Mbinu hii ya kujenga uaminifu kwa mlengwa inatumiwa sana. Wahanga wakubwa wa hii mbinu ni wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo.

Hufanyika kwa namna hii, bwana “X” anajenga uaminifu kwa bwana “z” kwa kumchangia/kununua bidhaa ktk ofisi yake kwa pesa taslimu, baada ya muda flani ataanza kukopa na kulipa, kadri siku zitakavyo yoyoma bwana “Z” atamwamini bwana “X” ni mteja wake mkubwa na mwaminifu kwani hukopa na kulipa. Baada ya imani hiyo kujengeka bwana “X” hutumia fursa hiyo kutengeneza pancha nyingi kadri awezavyo katika mtaji wa bwana “Z” kwakuchukua bidhaa, kutokulipa kwa wakati na mwisho hutokomea kabisa.

Kuepukana na hili, kwa wafanyabiashara wote ni kuwa na marengo ya muda mrefu na mfupi ili kutoruhusu kuendesha biashara kwa hisia na mazoea.

Mi walinijaribu kwa kunipigia simu wakidai wao ni mawakala wa usafilishaji mizigo na vifurushi kutoka kampuni fulani ya mabasi iliyoko Tabora. Walinitaka nifike ofisini kwao kwaajili ya kuchukua mzigo wangu kwani umetumwa muda kitambo na mpaka sasa sijauchukua.

Aliyenipigia simu nilimuuliza maswali matatu ya ufahamu wa chap chap;
1. Mzigo husika umetoka wap?
2. Jina la mtumaji na
3. Namba zake za simu pamoja na namba ya mzigo.

Hakunijibu zaid ya kunitaka kufika ktk ofisi zao kwa taarifa zaidi na kuuchukua mzigo husika. Kwa wakat huo mi nilikuwa Tarime, sina ndugu Tabora wala rafiki na mbaya zaidi sijawai kukaa Tabora. Kitu ambacho kilianza kunifikirisha.

Kwakuwa tamaa juu ya jambo/kitu ambacho si changu ni mwiko, na nafsi yangu ilisita juu ya mzigo husika, hivyo basi, nikafikia maamuzi ya kuachilia mambo yaende kama yalivyokusudiwa. Sikupata ujumbe wowote kutoka kwa ndugu, marafiki na jamaa juu ya mzigo husika wala wahusika wa utapeli hawakuni tafuta mpaka leo hii.
 
Back
Top Bottom