Wizi wa Mtandaoni umekithiri sana, ndugu yangu alinusurika. Weka kisa chako hapa kuokoa mwingine atakayetaka kutapeliwa kama wewe

Wizi wa Mtandaoni umekithiri sana, ndugu yangu alinusurika. Weka kisa chako hapa kuokoa mwingine atakayetaka kutapeliwa kama wewe

w0rM

Member
Joined
May 3, 2011
Posts
81
Reaction score
192
Habari wanajamvi,

Utapeli na wizi wa Mitandaoni kwa kweli umekithiri sana jamani, yaani kuna ndugu yangu kidogo aibiwe na hawa watu. Ukweli ni kwamba wizi huu pia hutegemea zaidi bahati ila wengi sana wanaumia na wizi huu. Ngoja niwape kisa kilivyokuwa;

Nina kaka yangu mwenye mke na mtoto anayesoma darasa la 3. Siku moja akiwa kazini alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Mwalimu wa Mtoto na kumwambia kuwa mtoto wake ameanguka shuleni na kupelekwa hospitali hivyo anatakiwa kuchangia fedha kiasi cha TSZ 80,000/- kwa ajili ya kufungua faili na kumuona daktari.

Kilichomfanya amini ni kwa sababu mtu yule alitaja jina la mtoto wake la kweli na kutaja shule ya kweli anayosoma mtoto huyo (Baadaye tulihisi taarifa hizo tapeli alizipata katika mtandao wa Facebook kwenye akaunti ya Kaka ambapo kuna namba ya simu ya Kaka na huwa anatabia ya kumposti mwanaye na mara kadhaa ametaja shule anayosoma mwanaye).

Baada ya kupokea simu hiyo alimtafuta mke wake, aliyekuwa nyumbani lakini simu yake haikupokelewa pia akamtafuta dada (Msaidizi wa kazi za ndani) naye hakupokea simu. Lengo la kuwatafuta ni kutaka kujua kama wamepata taarifa yoyote. Kutokupatikana kwao kulimfanya Kaka awaze na kufikiri kweli kuna shida ndio maana Mke wake wapokei simu kumbe mke wake na dada wote hawana hili wala lile, wameacha simu ndani na wanashughulika nje ya nyumba

Wakati bado akiwa amechanganyikiwa na kuanza kutafuta hela (hakuwa nayo kwa simu) ili atume na kuongea na wenzake kazini kwamba amepata dharura inabidi kwenda nyumbani, mwezake mmoja ndio alimwokoa na kumfanya asitume fedha hiyo. Mwenzake huyo alimwambia, siku hizi wizi ni mwingi kwanini badala ya kutuma fedha usifike kabisa pale hospitali kuona kinachotokea? Maana hawataacha kumtibu wakiambiwa mzazi unaaenda. Lakini pia alimuuliza hauna hata namba ya simu ya Mwalimu kumuuliza kama kuna shida yoyote?

Hapo ndio akili sasa zikaanza kumkaa sawa na kuanza kutafuta namba za Walimu na kuipiga namba moja wapo na kupata taarifa kuwa mwanaye yupo tu shuleni na anaendela na masomo kama kawaida.

Sasa nawaza kama asingekuwa na mtu karibu au angekuwa na fedha kwenye simu, angekuwa ameshatapeliwa.

Ushauri wangu: Ni vema kuwa waangalifu na makini na hawa matapeli jamani, na tusiweke taarifa zetu sana kwenye mitandao ya kijamii, kwani wanaweza kuzitumia vibaya.

Karibu tushikishane hapa namna ulivyotapeliwa au ulivyotaka kutapeliwa mtandaoni, itasaidia kuokoa watu wengine
 
Mimi nilitapeliwa na pages za instagram, mmoja 1.1M mwingine 650k na zote bado zinaendelea kutapeli.. despite RB na kila kitu… almost 3 - 2 years tangu nitapeliwe
Pole sana ulitapeliwa vipi haujasema ulitumaje Pesa au uliwapa Mkononi?
 
Nilishawahi kufanya huu mchezo unalipa sana watoto wa ifakara wana nyumba na boda za kutosha kupitia huu mchezo
Kauli kama hizi ndio zinafanya watu hawaachi kitapeli. Maana wanajua mchezo huo unalipa
 
Angemuuliza ni hosipitali gani, akitaja wewe mwambie nampigia daktari wangu pale amsaidie.
 
Back
Top Bottom