Wizi wa vifaa vya magari

Wizi wa vifaa vya magari

Mwasapile

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2020
Posts
214
Reaction score
448
Kuna suala limetrend sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wizi wa vifaa vya magari.
Unakuta umepaki gari lako usiku ukija asubuhi unakuta show yote ya mbele hakuna, taa zimetolewa..wakiweza kufungua milango wanatoa power window wanasafisha redio na kila kitu.

Sasa concern yangu ni kwamba katika wizi huohuo unaotrend unafanyika haswa kwa baadhi ya models za magari...mostly ni Toyota na subaru.

Ila kwakweli sijawahi kuona BMW mashine ya kijerumani imenyofolewa show kuibiwa taa na kufumuliwa show ya ndani.

Hili limekaaje!? Ni kwamba BMW haziibiki au!?
 
Ukiachana na soko la spea kuwa dogo, hizo BMW ni kazi kufungua hizo spea kwa hao wezi kutokana na kukosekana kwa vibaka wenye uzoefu na hizo gari, maana gari za kufanyia majaribio ni chache. Wengine huishia kupoteza muda, kuharibu gari na kuondoka na vitu ambavyo havina thamani...

Aisee itakuwa kuifungua Bmw sio suala la mchezo ndio maana cases za hizo gari kuibiwa vifaa ni kama hamna...ntanunua bmw. Naitamani sana bmw x1 ila kwa kuanzia ntaanza na 3series
 
ha ha ha ha hamna faza ni vile tu nazikubali bmw na nafurai ambavyo naona haziibiwi. Hili ni funzo tuache kununua matoyota

Mjerumani vifaa vyake bei ghali halafu gari chache na haviingiliani. Ukiiba taa ya 3 series ya M-performance huwezi funga kwenye 3 series ya kawaida ikafanya kazi.
Ukiiba taa ya Audi A4 Avant ya mwaka 2006 haiingiliani na ya mwaka 2003 japo ukiziona unaona ziko sawa 😂😂😂
 
Kuna suala limetrend sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wizi wa vifaa vya magari.
Unakuta umepaki gari lako usiku ukija asubuhi unakuta show yote ya mbele hakuna, taa zimetolewa..wakiweza kufungua milango wanatoa power window wanasafisha redio na kila kitu.

Sasa concern yangu ni kwamba katika wizi huohuo unaotrend unafanyika haswa kwa baadhi ya models za magari...mostly ni Toyota na subaru.

Ila kwakweli sijawahi kuona BMW mashine ya kijerumani imenyofolewa show kuibiwa taa na kufumuliwa show ya ndani.

Hili limekaaje!? Ni kwamba BMW haziibiki au!?
Ila Toyota RunX generation moja taa zinaingiliana, mfano ya 2000-2004
 
Back
Top Bottom