Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Kuna kipindi nyumbani tulikuwa tunajenga nyumba ya familia, Ikaanza kila tukinunua sementi unakuta mifuko inapungua, kumbe kibarua akichanganya mchanga na sementi, anapakia mchanganyiko kwenye mifuko anaifukia chini kisha usiku anaibeba anaenda kuwauzia watu.
Sasa siku moja wakati akiwa kashafukia mfuko wa mchanga wenye sementi chini mvua ikanyesha, maji yakaondoa ule mchanga wa juu ambao ulikuwa umefunika mfuko mfuko ukaanza kuonekana, mmoja ya ndugu akauona mfuko akaufata kuutoa kwenye kishimo ndio kugundua ni mchanga wenye sementi.
Usipokuwa makini kwenye usimamizi mafundi wanakupiga mpaka utajuta.