Wizkid aitakia happy Independence day Tanzania


Hio ni opportunity mkuu...nadhani hulioni hilo...dont you see hili mfano wa bifu linafanya watu wote watake kujua who is diamond....

Kwa wajanja hapa ndipo wanapiga pesa....usiogope,....sometimes vitu kama hivi hua vinatengenezwa
 
Mimi nina swali kwmb inapotokea mashindano ukawa mshindi. Alafu yakatokea maneno kwmb wandaaji wamecheat. Maana yake si kwmb nawewe mshindi sio halali.
 
Hio ni opportunity mkuu...nadhani hulioni hilo...dont you see hili mfano wa bifu linafanya watu wote watake kujua who is diamond....

Kwa wajanja hapa ndipo wanapiga pesa....usiogope,....sometimes vitu kama hivi hua vinatengenezwa
Ndo kosa lile lile la akina Babu Talle!! Kwanza, naunga mkono siku Diamond alipogoma kupanda jukwaani German akitaka kwanza alipwe pesa zake jambo ambalo hatimae lilipelekea kuzuka kwa vurugu! Katika hali ya kushangaza, Babu Talle bila kufikiri mara mbili akadai eti mambo kama yale yangempandisha Chibu... that's was a stupid comment to reveal in public kwa manager wa msanii coz' hata kama aiamini hivyo angebaki na hizo peke yake! Babu Talle ile kuona polisi wa Ujeruman wanakuja kwenye tukio ndo basi tena akadhani itakuwa ni talk of the town huku akisahau kabisa mambo kama yale hapa Dar yanaweza kutokea Keko na wala Ilala wasifahamu kwamba kuna mtiti ulitokea Keko!!!

Tukija upande wa hili sakata, am sure ndivyo wengine wanavyoamini... kwamba eti litakuwa ni kiki kwa Diamond! Hivi unatarajia huko Naija hivi sasa watu ndo basi tena watakuwa wanajadili masuala ya Diamond kwenye nchi yenye wasanii kila kona?Tuache na hizi habari za sifa za kijinga ambazo zingekuwa na manufaa endapo tu Diamond angekuwa na base ya mashabiki kule Nigeria! Yaani mnashabikia matusi ya kiuendawazimu kwa kigezo cha kwamba itampa kiki? Hivi wewe unaweza kugombana na mshirika wako na kufurahia mshirika wako anatukanwa matusi mazito mazito huku ukidhani hiyo itakuongezea umaarufu?

UKitaka kupata jibu kwamba ni kweli itamuongezea kiki, jaribu kupitia tweet za wanaija na linganisha za hapa JF! Kwenye sakata hilo, hapa TZ hususani JF kuna watu wanamonda Diamond wazi wazi... je, huko Instagram na Tweeter umeona kuna wanaija ambao wanamponda Davido wazi wazi na kumuunga mkono Chibu? Kama unadhani wapo, basi hao ndio ambao wataanza kumfuatilia Diamond baada ya bifu hili lakini ukweli ni kwamba anapoteza mashabiki wa Davido ambao walikuwa wanaonesha love kwake kwa ajili ya ukaribu wake na Davido!!
 
nimemzungumzia wizkid coz ana uhasama na davido na hajawai hapo nyuma,ukiachana
Hapo nyuma hakuwahi kwavile Tanzani yenyewe ilikuwa bado haijaingia kwenye ramani ya muzlki manake sidhani hata kama huyo Inyanya alishawahi hapo kabla! Kazi ya Chibu ndiyo imewafanya yatokee haya!
 
chige unajidanganya mkuu...USA wasanii wana ma beef kila siku na wana survive

kwa hio wewe unadhani mashabiki wa Naigeria wote wanampenda davido.

Wapo ambao wako against nae...nao wataopt kwa diamond kutokana na sakata hili

Diamond hajatukana mtu...Davido hajatukana mtu....sasa sijui kwa nini unadhani wao wawili hawawezi kaa meza moja

Kukujulisha tu this can be a beef that is orchestrated by both Davio and Diamond........

Hili ndilo linaitwa game la muziki

Tofautisha kabisa na vurugu za ujerumani...that was something else.

Cha msingi kubali kwamba hili sakata litawafungua wanaija wengi zaidi kumjua Chibu...

Hata hivyo chibu hajawatukana wanaija
 
Last edited by a moderator:
Kwanini nitofautishe na vurugu za Ujerumani wakati Meneja wa Chibu aliamini kama unavyoamini wewe hivi sasa kwamba vurugu zile zingempa kiki Diamond? By the way, kama kuna bifu za wasanii zinazomsaidia mtu sio dizaini hii.

Kisha unahoji ikiwa mashabiki wote wa Nigeria wanampenda Davido, jibu ni hapana lakini kama unatarajia eti wale wasiompenda Davido leo hii ndo watakuwa mashabiki wa Diamaond basi nadhani unatakiwa kufikiria mara mbili mbili mawazo hayo! Wale wasiompenda Davido bado wana options mia moja kidogo within NIgeria boundaries not mentioning West Africa... kama suala ni kwamba adui wa adui ni rafiki basi wataanza kuwafikiria watu kama WizKid kabla ya Diamond... wana lot of options... kuna wasanii lukuki!!!

Nitarudia tena hapa... tuzo tatu za Channel O wala zisitupe kiburi kwa kudhani ndo basi tena Tanzania tupo juu! Bado sana coz' foundation hakuna! Ni kama leo hii Wakenya wajione wapo top kwenye filamu kwa kuwa Lupita Nong'o amechukua tuzo za Oscar! Sie mashabiki wa Diamond tuishie tu hizi tuzo kuwaringishia mahasimu wetu akina Matola lakini tutaonekana hata tasnia yenyewe hatuhijui tukitaka kuwaringishia Afrika mzima, hususani NIgeria ambazo tuzo kubwa kubwa zote zimerundikana kule kwa miaka nenda rudi!!

Kisha unahoji sijui kwanini nadhani hao watu hawawezi kukaa meza moja! Hakuna popote niliposema hawawezi kukaa meza moja... tena kwenye ule uzi wa Diamond's Fans Special Thread nimeshasema wazi kwamba the relationship can be fixed. Kwamba Diamond hajamtukana Davido na wala Davido hajamtukana Diamond wala usidhani kwamba Davido haimuumi! Juzi tu hapa tumemshuhudia Zitto akimwaga chozi bungeni baada ya kutajwa mama yake ambae tayari ni marehemu! Sasa ikiwa Zitto baba zima limemwaga chozi, what do you expect kwa kijana mdogo, under 25 kama Davido wanapotokea watu na kusema "fuc'k your dead mama and papa...!" Unadhani haumii? Au ulitarajia uone picha instagram ikimuonesha anavyolia au alivyohuzunika? Ikiwa amefikia hadi kuichukua ile post kutoka Instagram na kuiweka Tweeter, huwezi kubashiri ni namna gani imemuumiza? Nini kipo akilini kwake? Unataka kusema anaona hao ni wahuni tu na sio mashabiki wa mshikaji wake? Diamond kasema nini? Bila shaka anaogopa kupoteza mashabiki maandazi at the expense of urafiki... urafiki ambao tukubali au tusikubali (kwavile tumejawa na kiburi) umemnufaisha zaidi Diamond kuliko Davido! Tukubali tusikubali, percentage ya Watanzania waliokuwa wanamfahamu Davido kabla hajashirikiana na Chibu ni kubwa mara dufu kuliko percentage ya domiciled Nigerians waliokuwa wanamfahamu Diamond (na kama walikuwepo)!


Kwamba eti bifu linaweza kuwa orchestrated by both Diamond na Davido; there's no way! Davido ka-tweet message ya kawaida kabisa, Diamond nae akajibu na mashabiki wa Tanzania wakaingia kichwa kichwa bila kujiuliza! KItu ambacho naamini ni kwamba, pametokea misunderstanding! Hata Chibu mwenyewe endapo angefahamu kwamba mambo yange-turn the way yalivyo, sidhani kama angekuwa amejibu vile... hali kadhalika, hata Davido nae kama angefahamu what would happen, basi sina shaka tweet yake ingekuwa clear kama aliona ni lazima a tweet!
 
Kuna watu wana maneno mengi kama wanasiasa!lol sipati picha wangekua wahubiri...
 
yani unataka kusema emmanuel tv wametupa airtime coz ya kilichotolea???hope ur not serious



Wewe vipi? Mada inahusu wishes za uhuru wa Tanzania, au wewe umeleta mada nyingine? Zinduka.
 
chige one point you should note is mashabiki watabaki kuwa mashabiki....wana maoni yao

Kama umekubali diamond hajamtukana Davido

Na wala davido hajamtukana diamond

Sasa unataka diamond afanye nini?

Acha mashabiki wafanye ushabiki wao
 
Last edited by a moderator:
Wewe vipi? Mada inahusu wishes za uhuru wa Tanzania, au wewe umeleta mada nyingine? Zinduka.

tunamuongelea wizkid, ww unaleta habari za emmanuel Tv
nway keep it up!!!!
 
ahsante,bora yako nyepesi
 

We jamaa ni punga😡 sana
 
wizkid ambaye ni msanii wa nigeria na hasimu mkubwa wa davido ameitakia happy indepence day Tanzania.Hii imekaaje au ndio kutumia fursa kwa lile wingu lililoibuka upande wa davido na watanzania.
Kweli wenzetu wanajua kutumia advantage

Huyu ni mbumbumbu tu kama wewe, ni Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…