Shirika la hali ya hewa la Umoja wa Mataifa limetoa onyo kali kuhusu hali ya hewa ya El Niño, likisema inaongezeka kwa kasi na huenda ikawa tukio lenye nguvu zaidi kuwahi kurekodiwa tangu ufuatiliaji wake ulipoanza miongo minne iliyopita.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Katibu Mkuu wa WMO, Celeste Saulo, alionya kwamba utabiri wa sasa wa hali ya hewa unavuka viwango vya kihistoria na kwamba kuna uwezekano wa karibu asilimia 100 El Niño kuendelea hadi Februari 2027.
Shirika hilo limeonya kuwa iwapo mwenendo wa sasa utaendelea, ongezeko la joto la baharini na mabadiliko ya anga yanaweza kuvunja tena rekodi za joto duniani, baada ya mwaka 2024 kuwa miongoni mwa miaka iliyokuwa na joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa.
WMO imeonya kuwa hali hiyo inaweza kusababisha ukame mkali, mafuriko na hali mbaya ya hewa, huku ikiathiri kilimo, biashara, afya, nishati, usafiri na upatikanaji wa maji duniani.
Kutokana na hatari hiyo, viongozi wa hali ya hewa duniani wamepewa wito kuchuka hatua mapema, ikiwemo kuimarisha mifumo ya tahadhari, kutoa fedha za dharura na kujiandaa kukabiliana na majanga ili kupunguza madhara ya kiuchumi na kulinda jamii zilizo katika hatari zaidi.