Wode Maya aipaisha Tanzania. Wizara ya utalii imtumie.

kiwiko

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
1,341
Reaction score
2,214
Huyu kijana yupo Tanzania sahvi. Amejizolea umaarufu mkubwa kupitia channel yake ya Youtube ambapo ameweka juhudi za kutangaza nchi za Afrika kwa dunia ili kuondoa picha mbaya iliyozoeleka huko duniani.
Katika video yake ya kwanza kufika Dar es Salaam ameisifia sana na kupokea sifa nyingi toka kwa watazamaji kutoka mataifa mbalimbali.
Kiukweli anaitangaza nchi na Afrika hivo wizara ya utalii iangalie jinsi ya kumtumia zaidi kutokana na kuwa na watazamaji wengi.
Cha kushangaza amelalamika kwamba amedaiwa aombe kibali ili kuruhusiwa kurekodi video zake.Hapa sijui sheria gani imetumika. Hii sio vizuri kwa mtu anaetaka kusaidia kutangaza nchi yetu.

Anapatikana hapa:

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuitangaza nchi sio sababu ya kutofuata Sheria. Afuate taratibu zote zinzotakiwa.
 
Kutangaza nchi kwa kuonyesha magorofa!!!! Na mitaa yenye barabara za lami!!!! Angetangaza utalii apige picha mbuga za wanyama na vivutio vya watalii vilivyoko afrika.Anachofanya ni zero hakileti fedha za kigeni kwa bara la afrika ni.mzururaji anayepiga picha mitaa na kurusha YouTube channel yake.Sioni la maana analofanya zaidi ya mipicha ya mijengo ,mibarabara mizurri nk
 
Anatangaza kilingana na uwezo wake sio vibaya kuonyesha vitu vizuri vya nchi. Kama atakua na uwezo wa mbugani atafanya maana anafanya kazi yake kwa kuchangiwa na watazamaji pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kama nyie kwenye jamii hawakosekani
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Anataka awatoe upupu kichwani wazungu kwanza ndipo aende huko.

Siku zote tunawaonyesha twiga,tembo na wamasai.kitu kinachofanya jamii nyingi duniani kudhani africa kuna wamasai na tembo tu.
 
Mkuu hujaona alivyo ipaisha Zanzibar na fukwe zake za kuvutia?

Unajua kwamba ukiachana na kutalii MT. Kilimanjaro na mbuga zetu wageni wengi sana hupendelea fukwe za Zanzibar na historia ya visiwa vile?

Unajaua kwamba waziri wa utalii wa Kenya ilibidi aje ajifunze kwanini Zanzibar hasa hotel zake zinavutia sana watalii toka nchi zilizo endelea kiasi cha kuipuku Kenya na fukwe zake au mbuga zake za wanyama kwa wakati flani?
 
Ndio maana mleta mada kasema wizara imtumie kutangaza utalii wampeleke mbugani huko
 
Umekosea Sana. Unadhani utalii ni kuona wanyama mbugani pekee?
Kama hujui basi kaulizie kuhusu jiji la Paris au new York linapokea watalii wangapi kwa mwaka! Au nenda cape Town uone! Watanzania wengi wamedanganywa eti utalii ni mbuga za wanyama tuu.Huyo do go kaitangaza hadi Zanzibar. Na bado hamuoni.Bodi ya utalii ndio hata kujaribu kuonana nae ili wampeleke kwenye vivutio vingine wameshindwa.
Kuna yule Dada wa USA nae ana Chanel ya you tube inaitwa traveling Sista,nae wameshindwa mtumia
 
wewe kama mtanzania mkaazi umefanya initiative gani kuitangaza nchi yako
 
Anataka awatoe upupu kichwani wazungu kwanza ndipo aende huko.

Siku zote tunawaonyesha twiga,tembo na wamasai.kitu kinachofanya jamii nyingi duniani kudhani africa kuna wamasai na tembo tu.
Ni agent wa wazungu to huyo.Theme ya anavyoonyesha yaweza UA utalii.Sababu anaonyesha hivi kuwa nyie wazungu Kama kwenu Kuna maghorofa na Afrika tunayo.Anayapiga picha lakini hizo picha zina destructive image kwa watazamaji mfano unapiga jengo katikati ya jiji lenye ghorofa 20 wakati kwao wana lenye ghorofa Mia moja conclusion mtazamaji kule anayopata ni kuwa watu hao bado primitive Sana ona barabara za Kati
Kati ya mji Kama uchochoro na kwao ndio wanajiona wako juu!!!! Yeye angepiga vitu ambavyo haviko kwa wazingu mfano migodi ya madini,mbuga za wanyama, mashamba makubwa mfano ya mazao ambayo kule kwao hayapo nk.Lakini kuwaonyesha vlle vilivyoko kwao ambavyo vipo Africa naona Ni ujinga tu haisaidii Africa
 
wewe kama mtanzania mkaazi umefanya initiative gani kuitangaza nchi yako
Nikisafiri nje huwa nabeba vipeperushi vya utalii.Nikikata tiketi ya ndege namwomba tour operator anipe vipeperushi vyake vya utalii na package zake nikawagawie watu huko niendako.Tour opperator walishawahi Nipa tiketi za bure za ndege na kulala free hotel mbugani Serengeti baada ya kupata wateja kwa kupitia kipeperushi nilivyowagawia nje kwani walikuwa wakinitaja kwao kuwa ndio niliwapa hivyo vipeperushi na hivyo kufanya business nao
 
ngie mapow aga huko ughinuni mnapigaga picha za nn si ndo hayo majengo marefu wibu tu umwtujaa ijui tufanyiwe nn mnadhani wazungu wanakuja tu kuangalia mipori yetu haya bana
 
Anayejitahidi kukuelimisha wewe anakazi ya ziada. Yaani huwa unataka watu watende kadri ya maono yako tu? Kama yeye ameonesha maghorofa na barabara nzuri, kazi kwako kuonesha hiyo migodi na mbuga na sio kukaa pembeni na kupiga sound tu.
 
Unajua wewe ni lipumbavu sana? Mleta mada ameleta bonge la wazo la kujenga, kwamba wazungumze na huyo dogo wampe mwelekeo namna ya kuitangaza nchi,we unaleta ulofa wako wa lumumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…