Wolper afunguka mazito kuhusu mapenzi

PRINCE PRIS

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2015
Posts
347
Reaction score
587
Wolper amesema hawezi kuvumulia ujinga wa kunyanyasika na kuteseka kwenye uhusiano na mwanaume kwa kuogopa jamii kumsema ubaya wakati mkosaji akiwa ni mwanaume


"Kila mtu anatakiwa kuwa na maamuzi yanayo mpa faraja,si kila jambo lazima liwe sawa na mtu mwingine kifikra,kuna baadhi ya wanawake wanajikuta wakinyanyasika kwa kuhofia jamii itawaonaje wakiachana na wanaume wasaliti,ila kwangu haipo hivyo"amesema wolper
 
Haukosagi cha ku-Comment mkuu. [emoji3][emoji3][emoji3]
Hivi hii nchi ikoje!yaani hawa wasanii na hao wanao jiita mastar ambao wanastahili kuwa kioo cha jamii wamekua uchafu mtupu!Yaani bila kuwa na skendo za uasherati wanona ustar wao haujakamilika!Yaani ni kama wamerogwa, utadhani hawakulelewa na wazazi!Mpaka sasa wanatupa kazi mara dufu ktk malezi maana kila kukicha mara huyu kamwagana na nani,mara huyu kazaa na nani!yaani hadi watoto wanaamini kuwa star maarufu Tanzania hii ni lazima uwe mpenda ngono,mwasherati n.k.
Cha kushangaza hao wanao bomoa maadili yaliwekwa na kulindwa kwa nguvu zote na wazazi,wazee,viongozi wa dini,viongozi wetu wa kisiasa hawakemei, hawaoni huo uchafu,zaidi sana ndio wanawakumbatia na kuwafanya ndio marafiki wa kubwa!
Sisemi ni wote Ila sasa kwa hao baadhi wanaojitambua na kujieshimu wanachafuka kupitia hao wenzao kwani samaki mmoja akioza kwenye gunia,ni wote!
Haya mambo pia utakuta yanamkasirisha Mungu hadi anawachia tu haya maharamia kutuibia kila kona ya rasilimali za nchi yetu,matokeo yake tunaanza kuangamizana wenyewe badala ya kuweka nguvu pamoja na kuwaadabisha!
Mungu atuhurumie na kutusamehe!
 
Na yeye bora angepotelea kusikojulikana, hana mpya.
 
Huyu nae hana bahati, kila siku anaachwa tu na huo uzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…