Wolper afunguka pesa itayogharimu harusi yake

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Mwanadada mwanamitindo na mwigizaji maarufu nchini, jackline Wolper Massawe ametangaza makubwa ujio wa ndoa yake inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni mara baada ya kuwa tayari ameshatolewa mahali.

Wolper amedai kuwa ndoa hiyo inatarajia kugharimu kiasi cha shilingi milioni 60 za kitanzania, ikiwa milioni 50 kutumika kwa ajili ya harusi itayofanyika Dar huku milioni 10 kutumika harusi itayofanyika Marekani.

“Milioni kama 50 zitatumika kwenye sherehe ya hapa Bongo na nyingine 10 nje kwa sababu kule Marekani hatutakuwa na watu wengi sana,” alisema Wolper.
Akizungumza hayo pindi alipohojiwa na moja ya chombo cha habari mjini , Wolper amesema kuwa kwenye harusi inayotarajiwa kufanyika Marekani anatarajia kusindikizwa na wasanii wanne akiwepo Anty Ezekiel, huku wengine watatu bado hawajajulikana kwa majina yao.

‘’Wasanii ambao nitaenda nao kwa ajili ya kuhudhuria harusi yangu ni wanne tu, mmoja kati yao ni Aunt Ezekiel kwa sababu huwa ananipa sapoti kwenye biashara zangu hivyo siwezi kumwacha,” alisema Wolper

Wolper amesema kuwa gharama zote za wasanii watao msindikiza zitaakuwa juu yake yaani kuanzia usafiri wa hapa nchini hadi pesa yao ya kujikimu pindi wawapo nchini Marekani.


Dar 24
 
Harusi za siku hizi huku mtaani gharama zake mil 25 hadi 60, za matajiri kidogo huwa zinafika hadi 100, za matajiri sijui maana huwa hata hawasemi. Wolper kama msanii mkubwa na mkongwe Tanzania kujinadi harusi ya mil 60 akidhani ni kubwa sana ni ulimbukeni.
Harusi nilizowahi kuchangia/kwenda mimi hazijawahi kuzidi mil 15 na wanandoa wamedumu kuliko za hao wabongo movie na fleva baada ya miezi miwili wanaachana
 
Kwani cha muhimu kwenye ndoa ni gharama yenyewe au ni upendo miongoni mwa wahusika?
 
VISA NA MIKASA VYA MASTAA WA BONGO: Msanii mwenye mikasa mingi, Jacqueline Wolper ainadaiwa kuwa amepatwa na taharuki baada ya Jana tarehe 14 kugundua kuwa mchumba aliyemtambulisha kwa jina la Leonard kuwa alishaoa miezi mitatu (3) iliyopita.

Mcheza Filamu huyo ambaye alishajiaminisha kufunga ndoa na mwanaume huyo, amepatwa na mshtuko huo huku wakiwa tayari wameshajipanga mwezi ujao, kwenda kukamilisha taratibu za kujitambulisha kwa wazazi wa Wolper.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wolper amesema, alidhani amempata mwanaume sahihi kumbe siyo na kwamba, anasikitika kwa kitendo hicho cha kudanganywa.

"Ninasikitika kwani nilichanga pesa zangu kwaajili ya kumuongezea jamaa kununua taxi ili kufanya biashara kama wanandoa watarajiwa kumbe mwenzio kashaoa bila kuniambia."

Wolper amewaalaani wote waliofahamu hilo na kukaa kimya pamoja na mwanamke wa jamaa na huyo aliyemuoa kwa kusema muda aliopoteza na machozi yake hayataenda bure.
 

Sasa hii ndiyo hiyo harusi ya milioni 60?
 
Isije kuwa anaandaa video mkajua kweli anataka kufunga ndoa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…