NYOTA wa Bongo Movies Tanzania ambaye pia anakua kwa kasi kwenye ujasiriamali, Jacqueline Wolper amepiga moyo konde kusimama na bosi wa Benchmark inayoandaa shindano la kusakura vipaji Afrika Mashariki (Bongo Star Search au BSS), Rita Paulsen 'Madam Rita' kufuatia kadhia iliyojitokeza usiku wa kumpata Miss World Tanzania.
Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki, Dar ambapo Madam Rita alikuwa miongoni mwa majaji.
Baada ya onesho hilo kukamatika huku mlimbwende Latricia Ian akiibuka na umalkia, ndipo paprazi wa Mike 360 Online Tv alipoomba mahojiano mafupi na Madam Rita.
Kimbembe ni pale ambapo, paparazi huyo alipokuwa akimuuliza swali Madam na kujibiwa jibu lililotafsiriwa kuwa ni la 'shiti' kwa mtangazaji huyo na kituo chake cha kazi cha Mike360.
Madam Rita aliulizwa anasemaje baada ya kumalizika kwa shindano hilo. Kabla hajajibu, aliuliza; "kwanza we ni Media gani?"
Alipojibiwa, akasema: "Media za uchwara-uchwara mi sifanyi." Akaondoka zake.
Kufuatia tukio hilo, hakukucha kufikaJumatatu ya leo, tayari mitandao ilitrendi tukio la Madam Rita na mtangazaji huyo.
Soma Pia: JUMIKITA: Media zisimpe tena ushirikiano Madam Rita
Hata hivyo, mgawanyiko haukukosekana miongoni mwa watu wa mitandao. Wengine wakisema Madam Rita alikosea kujibu 'shiti' huku wito ukitolewa kwa vyombo vya habari kwamba, bosi hiyo wa BSS asipewe 'tafu' wala ushirika kwenye kazi zake kama njia ya 'kumshikisha' adabu kwa dharau yake kwa 'midia' hiyo.
Wengine wakasema; Hapana. Mtangazaji wa 'midia' hiyo alikosea. Alimuuliza swali 'la kitoto' Madam. Na pia alimsimamisha kwa kitambo kisha kuja kuuliza swali 'bovu'.
Sasa miongoni mwa watu waliomtetea Madam Rita ni staa huyo wa filamu Tanzania ambaye pia ni mjasirimali, Jack Wolper au siku hizi maarufu kwa jina la Mama P (mama Paschal).
Mama Paschal alisema kuwa, Madam Rita naye ni binadamu na ana hasira kutokana na mwili kuwa na uchovu mwingi. Kwa hiyo hatakiwi kushambuliwa kwa kiwango cha juu kuliko kile kilichoonekana ni kosa lake.
"Hata kama kakosea lakini kuna muda binadamu anakuwa hayupo sawasawa. Siyo kama hatambui umuhimu wa media, hapana. Anajua ila kuna wakati mtu anakuwa hayupo sawasawa. Mimi namtetea Madam na namwombea msamaha kwa sababu namjua, si mtu wa kudharau media wala watu. Hakuwa na nia ya kudhalilisha mtu bali muda wenyewe ule mwili haukuwa sawa," alisema Wolper.
Wakati huohuo, Madam Rita amejitokeza hadharani akimwomba radhi mtangazaji huyo akisema hakuwa sawa.
"Binadamu tumeumbwa kukosea. Na mimi jana niliteleza. Naomba radhi kwa Mike 360 na kwa kila aliyekwazika kwa kauli yangu ambayo niliisema huku nikiwa na mood mbaya. Nyiye media zote ni wadau wangu na naomba tuendelee kushirikiana," amesema Madam Rita.