Women issues [maalum kwa wanawake wa JF]

Women issues [maalum kwa wanawake wa JF]

mawazo yako yamejaa kitchen party tu wewe huna lolote la maana la kufanya acha wanawake wenzako wafanye kitu humu jf uone jf itakavyokuwa mbali zaidi tena tunamwambia founder wetu afanyie kazi hii post nilituma kwani muhimu kwake na wanawake na wadada wa jf
this is likely introducing kitchen party in JF
 
King'asti nashukuru kwa kunipongeza na napenda watu kama nyie kwani mnachangamoto zuri kwani hiyo namba tatu imefanyaje jamani king'asti si ni wazo zuri bana maana wadada zetu wamesahau maadili na tamaduni nasi wanawake wa jf tunaataka tuwakumbushe tu japo kidogo yale maadili ya mtanzania aweje?
sasa king'asti wewe ni mwanamke unakaribishwa kwa mawazo, ushauri wako na hata kujiunga pia karibu
Hiyo namba tatu! Mmh.
Hongera kwa wazo zuri. Unamaanisha huo umoja wa humu humu jf nyuma ya key board ama mbele zake?
 
sweetylady karibu sana toa comments, hoja, na kitu chochote kitakachofanya women issue iendelee kwani tunataka kabla haijafika mwakani tumwambie founder wetu aisajili hii kitu kwani ni chema sana hususani kwa ajili ya kumkomboa mwanamke wa kitanzania dhidi ya mfumo dume na ukandamizaji hasa wanawake wa vijijini.

mwambie elizabeth kuwa umri kuanzia miaka 18 na kuendelea hakuna limitation yeyote ya umri awe ana akili tamamu na mwenye upeo ulipevuka tu anatakiwa kujiunga naomba ushauri , maoni na vilevile tunapendekeza kuwatafuta viongozi watakaoongoza kitu hii 'WOMEN ISSUE' hapo baadaye tunaweza kuweka kipindi katika media mbalimbali ili tujadili na kutoa mapendekezo yetu kwa jamii inayotuzunguka KARIBU
 
wewe umeshazoea kupewa nini? kwani hujaona chombo cha TAMWA kinavyofanyakazi yake hujawaoona wanawake wakiwasaidia wanawake wa vijijini unaishi mbingu hipi wewe? ya hapa duniani au uko ahera? angalia tena wewe yaelkea ni mwanaume hapa ni wanawake maalum tu na sio wewe acha hivyo mwambie bibi, dada na mama yako wajiunge uone kama hatutawaiidia weeeeeeeeeeeeeeeeee

Nifafanulie nikuelewe ili na yeye niweze kumuelimisha faida za kujiunga nanyi....
 
Tutakuandikisha madame B ondoa shaka
asante kwa kutaka kuwa pamoja nasi muda si mrefu utakuwepo hapo ila subiri tufanye mambo yaliyomakini kidogo katika ukurasa huu utakuwepo ondoa shaka na nitakufahamisha kama umeshajiandikisha

karibu
 
Tinmo wewe ni mwanaume au mwanamke maana ukurasa huu unahusu wanawake wa jf sasa huyo bibi yako yeye ni member wa jf au kwa niaba yako wataka nae awapo, oky nitakuelekeza ondoa shaka
 
Hiyo no.2 Nadhani ingekuwa kusisitiza fursa sawa kwa wote si tu kwa kutetea wasiojiweza au wenye matatizo bali wanawake wote wanavyonyanyapaliwa na mfumo dume. Hii huwapata hata waliosoma, wenye afya na wasio na matatizo simply kwa sababu ni wanawake!

Hili ni wazo zuri sana lakini in a very wrong place. Huwezi kuleta uanaharakati wa ana kwa ana kupitia JF, simply can't work, believe me. Hapa ni mahali pa watu kusemea jambo na umma upate nafasi ya kulichambua na kulifanyia kazi bila lazima ya kuhusianisha ujumbe utolewao na mtu anayeutoa; lakini kwamba tufahamiane sisi ni nani (physically), tukae pamoja na kudai haki zetu the base ikiwa JF, sahau hilo.

Tujiunge au tuanzishe NGO's za ukweli kupambana na mfume dume si kupitia JF!!!
 
una mawazo mazuri ila ungefocus may be mkoa fulani mfano wanawake wa jf waliopo labda arusha bt kwa tz nzima ni ngumu kwa kuanzia
 
Back
Top Bottom