Suriya ni kijakazi au msaidizi wa kazi wa kike ambaye kwa watu wa Middle East enzi hizo mwanaume alikua anaweza akajitwalia na kumfanya mkewe. Kwa mfano Bibi Hajira ambaye ni mama yake Nabii Ismael alikua ni Suriya kwenye nyumba ya Nabii Ibrahim na kwa ushauri wa Bibi Sara(Mke wa Nabii Ibrahim na mama wa Nabii Is-haq), Nabii Ibrahim alimtwaa Suriya Hajira na kuwa mkewe ambapo walimzaa Nabii Ismael