World Bank: Mwaka 2012 kulikuwa na Watanzania masikini milioni 12; hadi kufikia mwaka 2018 waliongezeka masikini milioni 2!

swali ni....jee JK aliwezaje kupunguza idadi ya masikini pamoja na population increase?

kiongozi yeyote anapaswa kuwaondoa wananchi wake kutoka lindi la umasikini.... akishindwa hafai kuenedelea kuwa kiongozi!


Hilo swali inabidi ulijibu wewe, lkn kwa mujibu wa hapo hao WB wako, TZ yetu imefuzu na kuwa middle income kabla ya muda uliotarajiwa, na kuwa middle income country maana yake ni kwamba wastani la pato la Mtanzania limeongezeka, sasa hilo la kuongezeka kwa umaskini kipindi hiki kulinganisha na kilichopita siwezi kuliongelea kwani sina datas na inaelekea limekaa kisiasa na kitoto zaidi kuliko kitaaluma, labda uweke hapa kipimo cha umaskini kilichotumiwa mwaka 2007 vs 2020, ...
 
Mbona account yenyewe hiyo ya Twitter sio Verified?
 

Data za WB zikionyesha tumeingia Lower middle income then zinakua Valid

Data za WB zikionyesha idadi ya raia maskini wameongezeka then zinakua zimekaa kisiasa na kitoto zaidi.

Kweli hii ni CCM MPYA.
 
Huyu alitakiwa aendelee kuongoza ng'ombe machungani, sio kuongoza Taifa!

Sijui mkosi gani ulitupata! Ameharibu sana nchi hii
 
Uchumi wa kati oyeee !!!
 
taarifa uliyoweka umeitoa NBS (ambayo always ipo lop sided kwa vile NBS ni instrument ya watawala).

taarifa yangu nimeitoa WB.... this speaks volume!
Hiyo taarifa imetoka World Bank na hiyo graph imetoka World Bank ...
Ain't no volumes spoken bruh....
 
Ukitumia asilimia utajua kuwa hao million 2 ni wachache na hivyo kasi ya umasikini imeshuka kwa kiwango kikubwa!
 
taarifa uliyoweka umeitoa NBS (ambayo always ipo lop sided kwa vile NBS ni instrument ya watawala).

taarifa yangu nimeitoa WB.... this speaks volume!

Hii nji kuna Watz wengi sana wamesomea UJINGA(Copy&Paste) kutoka kwa wenye akili kubwa!
Taarifa ya WB kuwa Tanzania imeingia Middle Income Economy (Uchumi wa Kati) ni Usanii na ubabaishaji mtupu. Ukweli ni kwamba kwa miaka 5 CCM ya Magufuli imetengeza MASKINI NA MAFUKARA wengi sana kuliko wakti mwingine wowote!
Jiwe ameua Sekta Binafsi ilokuwa Ina ajili Watz wengi! Lakini pia Jiwe hajaongeza Mishahara ya Watumishi wa Umma kwa miaka 5. Lakini jengine huyu Jiwe amesimamisha ajira kwa Vijana wanaomaliza vyuo! Lakini pia Jiwe ametengeneza Maskini kwa kuwaondoa WAFANYAKAZI aliodai Wanao vyeti fake lakini walifanya kazi zao kwa weledi vipindi vyote vya Marais walopita. Wafanyakazi Hawa hawakulipwa chochote na wengi wao walikufa na kuacha familia zao zikiteseka katika Umaskini mkubwa.
Sifa ya Jiwe ni kuwa RAIS WA VITU badala ya WATU.....!!!!
 
Data za WB zikionyesha tumeingia Lower middle income then zinakua Valid

Data za WB zikionyesha idadi ya raia maskini wameongezeka then zinakua zimekaa kisiasa na kitoto zaidi.

Kweli hii ni CCM MPYA.


Nimesema siwezi kujibu hilo swali kwa maana sina datas ya kipimo cha umaskini walichotumia 2007 vs 2020 mpaka kusema kwamba umaskini umeongezeka, isitoshe kuingia middle income economy ina maana wastani wa kipato cha Mtanzania kimeongezeka, hivyo kwangu habari zinakinzana, mpaka niwe navigezo vilivyotumika kupimia umaskini kati ya 2007 na 2020 siwezi kujua mleta mada anachomaanisha, ...
 
Vipi kuhusu ongezeko la watu? Mfano mwaka 2012 Watanzania walikuwa milioni 47.05 wakati mwaka 2020 tupo zaidi ya 59.8.
 
Mtoa mada hakutaka kuumiza kichwa, hii ndio sababu ya Msingi. Ni the same case kwa Nchi kama India, Nigeria na China kwa mbali.
 
taarifa uliyoweka umeitoa NBS (ambayo always ipo lop sided kwa vile NBS ni instrument ya watawala).

taarifa yangu nimeitoa WB.... this speaks volume!

WB as well ni ya mabeberu, ww unawaamini mabeberu sana inaonyesha, do you think WB ndio source sahihi sanaaaa haina husda na chuki dhidi yetu, ww unataka kutuambia WB ni safiii kama malaika report yake.
 
kumbuka aliyechangia pakubwa kufikia pato la kati ni JK ambaye aliyechangia $480B, akifuatiwa kwa mbali na Mkapa aliyechangia $330B... na aliyeshika mkia ni JPM aliyechangia $100B tu.

the borne of contention ni kwamba JK ali perform vizuri zaidi kiuchumi kuliko JPM.
positives nyingi za JK zimekuwa reversed na JPM.

ndiyo maana October tunahitaji kiongozi ambaye walau ata maintain positive trend ya JK at the minimum.
sasa hivi tunarudi kinyumenyume kwa kujificha nyuma ya mizuka ya SGR na Stiegler's Gorge isiyokuwa na impact yoyote kwa Watanzania.
 
Unaujua mlipuko wa ongezeko la watu Tanzania? Bila kuingiza hilo takwimu,hizo takwimu ni hazina maana, kwa kifupi kulikuwa na watu wangapi TZ 2012 vs 2020?

Ongezeko la watu lilikuwepo hata kipindi Cha JK... Pamoja na watu kuongezeka lkn haliweza kupunguza idadi ya watu masikini...


Acha kupotosha wengine kuongezeka kwa mtoto ktk familia sio sababu ya kuongeza idadi ya watu masikini kitaifa... Kama mtu Ni Tajiri na anamiliki wake wanne na ndani ya miaka 2 kapata watoto 4 + 2 wa michepuko... Kwahiyo hao watoto 6 ndio maskini?

kuzaana hovyo kama awamu ya 5 inavyopigia chapuo ni umasikini pia.
wewe una uwezo wa kulea watoto 2 lakini unazaa 10 unategemea nini?

Kwahiyo hao watoto waliozaliwa kuanzia 2012 Hadi 2018 wengi Ni maskini au kutoka ktk familia masikini?.... na kufanya idadi ya masikini iongezeke kutoka million 12 hd million 14....
 
WB as well ni ya mabeberu, ww unawaamini mabeberu sana inaonyesha, do you think WB ndio source sahihi sanaaaa haina husda na chuki dhidi yetu, ww unataka kutuambia WB ni safiii kama malaika report yake.
mimi siiamini NBS kwani hawana tofauti na chombo kingine chochote cha dola kama polisi, TAKOKURU, nk.

WB nawaamini kwa vile wao hawapepesi.... ikiwa nyeusi wanasema nyeusi na kinyume chake.
juzi tu hapa wametutangazia neema ya uchumi wa kati ambao nina uhakika wewe ulikuwa miongoni mwa walioushangilia sana uamuzi huo na hukuwaita mabeberu!
 
Ukitumia asilimia utajua kuwa hao million 2 ni wachache na hivyo kasi ya umasikini imeshuka kwa kiwango kikubwa!
JK alipunguza vyote.... idadi halisi na asilimia.
huyu kashindwa nini?

apigwe chini October!
 
Utazuia watu wasipigane miti?
 
JK alipunguza vyote.... idadi halisi na asilimia.
huyu kashindwa nini?

apigwe chini October!

Si nyie mlimuita JK ni dhaifuuuuuuuuuuuuuuuuuu, leo mmesahau unaanza kumsifia, au ndio mmeshikwa pabaya na Mh. Magufuli, naona mmepoteana sana, hadi mmeshafanya maongezi na Membe awasaidie kugombea, hali mbaya sana naona huko kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…