samurai
JF-Expert Member
- Oct 16, 2010
- 11,495
- 24,223
Kilimo cha kisasa pamoja na uwekezaji mkubwa kwenye kilimo ni moja ya suluhusisho kubwa kwa tatizo la ajira kwa watu wetu pamoja pia na kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja..
Rasirimali za Tanzania zikitumika vizuri kwa kuwawezesha raia kuzifikia ni moja ya sababu itakayofanya watanzania wengi wawe matajiri kuliko nchi zote za EA lakini pia zaidi ya nchi nyingi za Africa..
Serikali iondoe vikwazo kwa wazawa baadala yake iwasimamie na kuwawezesha, Tanzania ni nchi yenye ardhi kubwa iliyobikra na yenye rutuba bali inahitaji tu nguvu kazi na kilimo cha kisasa kuweza kuleta matokeo chanya kwa watanzania, Tanzania ina madini mengi ardhini yanayohitaji nguvu kazi na uwekezaji wa kisasa kwa watanzania kuweza kuyafikia na kuwa matajiri..
Serikali iwekeze kwa watu, uwekezaji huu utanufaisha watu wengi maana mtu mmoja akijengewa uwezo anaweza pia kujengea uwezo wengine na mwisho wasiku tutatengeneza pool kubwa ya matajiri na mwisho kabisa hata manpower itabidi tuimport kutoka nje..