World Bank Report: Transforming Agriculture | Realizing the Potential of Agriculture for Inclusive Growth and Poverty Reduction


Ni jambo jema kwa wananchi wa kawaiada,
 
Bila serikali imara tumeona jinsi sekta binafsi ilivyopewa nafasi lakini kwa asilimia kubwa sana walikeza kwa maslahi yao binafsi huku nchi na wananchi wa hali ya chini wakiendelea kubaki kama wateja na watazamaji tuu na kuwa maskini wa kutupwa. Mifano michache inaonyesha uwekezaji haukua kwa maslahi ya nchi sababu uliambatana na hujuma zilizopelekea baadhi ya sekta muhimu kuzorota na unasababisha wananchi wa kawaida kukosa kilicho bora kama kwenye Sekta ya mawasliano, Sekta ya elimu, Sekta ya afya, Taasisi za fedha, Kilimo n.k.

Sekta binafsi inaweza kuwekeza katika uchumi wetu na imekua ikifanya hivyo kwa miaka mingi sasa ila tatizo kubwa lilikuja kwenye
1.Vipaumbele vya wawekezaji vs nchi - tumeona viwanda vyetu vilivyonunuliwa na kufa kabisa
2.Uimamizi kwa upande wa serikali haswa watendaji wakuu
 
Hiyo akili mkuu pale Lumumba unafikri inaweza kutoka kwenye kichwa cha nani? Kifupi ccm hakunaga akili!
 
Bahati mbaya kilimo sio priority kwa serikali ya awamu ya 5. Miaka hii minne kilimo kimezidi kua na hali mbaya sana kwa tz
 
WAZIRI MBARAWA: ''TUSIPOPANGA VIZURI KTK KILA SEKTA, KUTATOKEA MACHAFUKO KAMA NCHINYINGINE'

Prof. Makame Mbarawa - Miradi mingi iliyoanzishwa itakuwa magofu

Tunajenga na kuzindua miradi mingi bila kuwa na mipango madhubuti hivyo miradi hii itageuka magofu 'white elephant'. Ametolea mfano awamu hii hakuna mpango wa kutunza vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhakikisha miradi mingi ya WASA water supply nchi nzima DAWASA n.k haina mipango ya kulinda vyanzo vya maji iwe mito n.k


Source: millard ayo
 
Hapana.
Sikubaliani na mawazo yako, na wala hayaendani na aliyoandika mkuu 'FUSO' na nilivyochangia kwa hoja yake ya kuhudumiwa wakulima.
Wewe umetoka huko kabisa na kuingiza hoja tofauti, ambayo pia huijui. Ningekuwa na muda wa kutosha ningekufundisha juu ya hilo.
Kenya licha ya kuwepo na mashamba makubwa ya michai, mahindi na mengineyo, lakini bado wakulima wadogo wadogo nao bado wapo, na ndio wengi zaidi. Hawa wanapata huduma kutoka kwa wataalam wa kilimo, sio kama hapa kwetu.

Wewe unadhani maziwa mengi yanayozalishwa Kenya na kuuzwa Brookeside, yote yanazalishwa na wafugaji wakubwa?
Una mawazo potofu juu ya 'ujamaa', in fact unaonyesha huelewi lolote.
 
It is about time they start talking; or else, it will be too late!
 
Mimi huwa siwapendi kwa machapisho yao yenye maneno meeeengi, kiasi kwamba hayamsaidii anayelengwa na tafiti zao.
Badala ya kumsaidia yanamchanganya zaidi.
Ndo siasa zenyewe hizo sasa
 
 
mkuu august, unanionyesha hayo ili iweje. Mbona unataka kuhamisha tuliyokuwa tunajadili na kuyapeleka kwingine?
'FUSO" alizungumzia jinsi asivyopata msaada wowote kutoka kwa wataalamu wa kilimo katika juhudi zake za kilimo.
Wewe unaingiza maswala ya mifumo ya 'ubepari na ujamaa', ambayo hayakuwa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

Sasa ukitaka kuyajadili hayo, nipo tayari kukukabiri pia. Inaonekana bado umeswekwa kwenye nadharia za mifumo hiyo yote miwili ambayo imekwishaonekana yote inalenga sehemu moja, baada ya waChina kutoa jawabu juu ya mfumo wao.
Wewe bado umeganda tu kule kule kwenye vita baridi?
 
It is about time they start talking; or else, it will be too late!

4 Dec 2019
KITWANGA - "NAMUHESHIMU MAGUFULI, ILA TUTAANDAMANA, ASITULETEE ASKARI"

Mbunge wa Jimbo la Misungwi huko kanda ya Ziwa nchini Tanzania, Mh. Charles Kitwanga ameeleza kuwa kama ahadi za kukamilisha miradi ya maji haitekelezwi hadi Mei mwakani atahamasisha wakazi wa jimbo hilo kuandamana na kufunga mitambo inayotoa maji ziwa Victori kupeleka Shinyanga na Tabora.....
Source: Global TV online
 

RIPOTI ya Benki ya Dunia kuhusu Maendeleo ya Kilimo Tanzania, imebainisha kuwa sekta ya kilimo nchini imeanza kuwa na mabadiliko chanya. Imesema mabadiliko hayo yakitumiwa vyema, yataleta fursa zaidi katika kuongeza ajira, kuondoa umasikini na kuongeza uzalishaji.

Aidha, ripoti hiyo iliyofanyiwa utafiti kwa muda wa miaka miwili, pia imeendelea kuitaja Tanzania kuwa ni nchi namba moja kati ya nchi za Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.

Taarifa fupi kuhusu ripoti hiyo iliwasilishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bella Bird.

Bird alisema pamoja na mabadiliko hayo, iko haja kwa serikali kuchukua hatua za kuboresha sera na mazingira ya uwekezaji katika sekta hiyo ya kilimo.

Alisema ripoti hiyo imeonesha kuwa kutokana na jitihada mbalimbali, zinazofanywa na serikali katika kukuza sekta ya kilimo, mabadiliko chanya yameanza kuonekana, ikiwemo kuwepo kwa ongezeko la wakulima wa kati, huku wakulima wadogo wanaolima kwa ajili ya chakula tu wakipungua.

“Ripoti inaonesha wakulima wa kati wameongezeka na kufikia 368,000 katika kipindi cha mwaka 2018 hadi mwaka 2014 na hivyo kuingiza takribani dola za Marekani milioni 225 hadi 300,” alisema Bird.

Alitaja maeneo ambayo yameanza kuwa na mabadiliko chanya kuwa ni ongezeko la uzalishaji, ongezeko la ardhi ya kilimo, masoko, huduma za kijamii kama vile barabara na huduma za fedha kwa wakulima na ajira za kilimo.

“Hali ya sasa ya kilimo inatoa fursa kubwa ya kuhamasisha uwekezaji wa kibinafsi na wageni na hivyo kuongeza kipato kwa watu masikini,” alisema Bird.

Alisema kwa takwimu za mwaka 2006 hadi 2016, kilimo kinachangia takribani asilimia 3.5 katika Pato la Taifa huku kukiwa na ongezeko la mchango wake kwenye pato hilo kwa asilimia sita kila mwaka.

Hivyo, ni muhimu kwa serikali kuhakikisha sekta hiyo, inatumika vyema kupunguza umaskini. Alieleza kuwa kiuchumi, Tanzania inafanya vizuri, kwani inaongoza kwa nchi za Jangwa la Sahara kwa uchumi wake kukua kwa kasi, huku mfumuko wa bei ukizidi kushuka.

Alitaja maeneo yanayochangia ukuaji wa kasi wa uchumi wa Tanzania kuwa ni sekta ya ujenzi na madini, huku sekta za kilimo na huduma zikielekea kushuka.

Alisema sekta ya nishati, nayo ilipanda kwa asilimia 15, huku akielezea sekta ya ujenzi kuwa ilipanda kutokana na uwekezaji mkubwa wa sekta binafsi na sekta ya uzalishaji iliongezeka kwa asilimia tano.

Kwa upande wake, Meneja wa Kilimo na Chakula kutoka Benki ya Dunia, Holger Kray alisema kwa hali ilivyo ya kilimo Tanzania, endapo kutakuwa na uwekezaji wa kutosha kwa sekta hiyo kwa angalau hata asilimia moja, takribani ajira 220,000 zinaweza kutengenezwa kwa mwaka.

Alishauri uwekezaji zaidi katika sekta ya kilimo, uhusishe sekta binafsi, kwani huko ndiko kutakuwa na mageuzi makubwa ya kilimo. Alieleza kuwa tayari kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ya serikali, uwekezaji binafsi kwenye kilimo unatarajia kuchangia kwenye eneo hilo kiasi cha dola za Marekani bilioni 20, kati ya dola za Marekani bilioni 45, zinazohitajika kwa ajili ya programu hiyo.

Mchumi Mwandamizi Kilimo katika Benki ya Dunia, Emma Modemba alisema ripoti hiyo, imependekeza kuwa ili kuleta mabadiliko chanya zaidi ya kilimo, serikali haina budi kuhakikisha inaboresha mazingira ya biashara.

Aidha, alisema ripoti hiyo imeshauri serikali kutenga fedha zaidi katika eneo hilo la kilimo, kwa kuwa huko ndiko kwenye ajira na kunakomgusa zaidi mtu masikini. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, bajeti ya kilimo imekuwa ikiongezeka kila mwaka, ambapo kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 imeongezeka kwa asilimia tatu.

Chanzo: Habari Leo
 
Hizi ni juhudi za kilimo kwanza za Jaakaya Kikwete sasa nchi imeingizwa kwenye ndege kwanza.
Hii awamu itaingia kwenye vitabu vya historia kwa kulitia taifa hasara.
 
Mimi sipo kwenye vita baridi especially ktk biashara au shughuli zetu za kiuchumi iwe kilimo au biashara na viwanda
Mfano issue ya mkulima au mfugaji wa ngombe wa maziwa, kwanza dam hatuna kiwanda cha maziwa fresh zaidi ya maziwa ya unga ambayo yanawekwa kwenye packet kama maziwa ya maji, cha pili wenye viwanda wanaweza kuwa na mifugo yao na ku complement kutoka kwa wazalishaji wengine na kutoa bidhaa zingine kama samli, jibini n.k.
Na kuhusiana na maafisa ugani, ikumbukwe kwanza wanaweza kuwa wachache, lakini hizi ni biashara binafsi ya mtu si ya serekali, hivyo ili upate huduma yao lazima umlipe, ili aje sehemu yako aone changamoto zako au unataka serikali ikulipie??
Kwenye hilo hilo la ufagaji wa ngombe wa maziwa kuna suala la malisho, je wakati wa masika unahifadhi malisho ya kutumia wakati wa kiangazi ili ku hakikisha uzalishaji unaendelea vizuri, lingine wengi wa wazalishaji ni retired people na umri umekwenda hivyo kushindwa kutekeleza majukumu mengine kama kutafuta malisho ya kutosha hivyo wanabakisha mifugo kama hobby na sio shughuli ya kiuchumi, sasa sijui na hapo serikali iingilie
 
Hizi ni juhudi za kilimo kwanza za Jaakaya Kikwete sasa nchi imeingizwa kwenye ndege kwanza.
Hii awamu itaingia kwenye vitabu vya historia kwa kulitia taifa hasara.
Punguzeni chuki za kitoto....
mna mazivu nyie.....
ina maana mpaka leo hujui viwanda na kilimo ni vitu vinavyokwenda sambamba!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…