World Bank: Umaskini umeongezeka Tanzania

World Bank: Umaskini umeongezeka Tanzania

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,786
Reaction score
1,715
Ripoti ya hali ya uchumi duniani imeonesha kuwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini uliopindukia imeongezeka zaidi, huku jirani zetu wa Kenya na Uganda wakiwa wamepiga hatua zaidi katika kupunguza idadi ya watu wanaoishi katika umaskini wa kipato.

Kwa mujibu wa Ripoti ya World Bank iliyoripotiwa kwenye mtandao na Global Monitoring Report 2013, Watu wanaoishi katika umaskini wa kupindukia (wa kipato) ni 38.01% kwa Uganda, 43.37% kwa Kenya na Tanzania ni 67.87%.

Hata hivyo, kwa kuwa tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hivi karibuni Rwanda na Burundi wamejiunga nasi kwenye Jumuiya hiyo, tunaweza kujifariji kuwa sisi si wa mwisho Afrika Mashariki, kwani tunaizidi Burundi ambayo 81.32% wanaishi kwenye umaskini uliokithiri (wa kipato). Nchi nyingine ndogo, isiyo na bandari na iliyotoka kwenye matatizo ya mauaji ya kimbari na vita, Rwanda, ina asilimia ndogo zaidi ya maskini kulinganisha na Tanzania, ambapo 63.17% ya Wanyarwanda wanaishi katika hali ya umaskini.

Nakaribisha mjadala wa nini kimesababisha sisi tupitwe na Kenya, Uganda na Rwanda katika juhudi hizo za kupunguza umaskini licha ya wingi wa rasilimali zetu, na licha ya kuwa na uchumi unaokua zaidi.

cc: Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi, Lukolo, EMT, ZeMarcopolo, Zitto, Mwigulu Nchemba, @J. Mnyika, Nape Nnauye, Mkandara, Invisible, nisaidieni kusambaza kopi kwa wengine

=====================

‘Kenyans poorer than Ugandans'

By Monitor Reporter | Monday, April 22 2013

Kenya has poorer people than Uganda, despite having a far larger economy, a new report by the World Bank and the International Monetary Fund shows.

According to the Global Monitoring Report 2013, Uganda's poverty head count stands at 38.01 per cent against Kenya's 43.37 per cent, using the poverty cut-off point of $1.25 per person.

The poverty level scoring is based on the number of people living below Sh105 ($1.25) a day. Previous studies have used $1 daily but that has since been replaced with the higher amount. According to the report, the level of poverty in Tanzania stands at 67.87 per cent, based on the latest available data.

In Rwanda, poverty stands at 63.17 per cent while in Burundi it is at 81.32 per cent, showing the extent to which war has continued to adversely impact livelihoods in the agriculture-rich country.

Burundi and neighbouring Tanzania therefore have the largest proportion of poor people among the members of the East African Community.

According to the report, sub-Saharan Africa has lagged behind in attaining the millennium development goals (MDGs), including halving poverty levels. "In 1990, with poverty rates of about 55 per cent, sub-Saharan Africa and East Asia were at the same starting position for MDG (and intention) to halve the number of people in extreme poverty," the report reads.

"By 2010, East Asia made spectacular progress and reduced extreme poverty rate to 12 per cent compared to sub-Saharan Africa which still had a poverty rate of 48 per cent."

The report suggested that growth of town dwellers helps to reduce poverty. In Africa urbanisation has increased from 30 per cent of the population in 1980 to 50 per cent in 2011. "Urbanisation helps pull people out of poverty and advances progress towards the MDGs, but, if not managed well, it can also lead to burgeoning growth of slums, pollution, and crime," says the report.

At global levels
From a global perspective, the report says urbanisation has been a major force behind poverty reduction and progress towards other MDGs. It noted that more than 80 per cent of global goods and services were produced in cities such that countries with relatively higher levels of urbanisation such as China, and many others in East Asia and Latin America, had played a major role in lowering extreme poverty worldwide.

"In contrast, the two least urbanised regions, South Asia and Sub-Sahara Africa), have significantly higher rates of poverty and continue to lag behind on most MDGs.

Source: 'Kenyans poorer than Ugandans' - National - monitor.co.ug
 
Naona umeweka asilimia tu, wala hatujui asilimia hizo zimepatikanaje na kipimo gani cha umasikini kimetumika! Bila kupata ufafanuzi wa haya tutakuwa tunachangia kisiasa na kiuzushi zaidi kuliko kiuchumi
 
Mkuu Mtu wa Shamba, katika CC nafikiri ulimsahau ZeMarcopolo, Sumu, bungeni, Wingu, Atongwele etc ambao wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii na wana pua lakini hazinusi kwamba CCM inaimaliza nchi.

Back to the point: Tanzania imeshindwa kuibua vipaumbele vya kiuchumi na vya kijamii. Kitendo cha Taifa la Tanzania kuwa halina umeme kwa zaidi ya miaka 20 sasa kwa kiasi kikubwa kimechangia sana kushuka kwa uzalishaji viwandani na mashambani. Maana kama viwanda havizalishi ni dhahiri kwamba flow ya materials kwenye soko inapungua na hivyo kuongeza ugumu wa maisha kwa watu wote wa mjini na vijijini

Lakini kitu cha hovyo kabisa ambacho Tanzania na CCM imeshindwa kukifanya ni kuinua uchumi wa wananchi vijijini. Imeshindwa kujenga uwezo wa wananchi wa vijijini ambao wanategemea kilimo kwa ajili ya kuendesha maisha yao. Wale wananchi wa kijijini ambao ni asilimia zaidi ya 70 ya watanzania wote wanazalisha kwa gharama kubwa sana. Bei za pembejeo (mbolea, mbegu bora na hata zana za kilimo) vimekuwa ni aghari ajabu, lakini akishavuna, serikali inatangaza soko huria ambapo walanguzi (wanunuzi binafsi) wanapita vijijini na kununua mazao kwa bei za hovyo. Mwaka unaofuata wananchi wanakuwa hawana tena mitaji ya kuwawezesha kulima, na matokeo yake uzalishaji unashuka mwaka hadi mwaka.

Wamekuja na mfumo wa stakabadhi ghalani lakini wakashindwa kuwalipa wananchi pesa zao kwa wakati na kusababisha kuua mitaji yao na mwisho wa siku kadri siku zinavyokwenda hali ya maisha ya wananchi vijijini inazidi kuwa mbaya.

Haya tugeukie kwenye ubunifu wa miradi ya maendeleo. Inasikitisha sana kwamba serikali hii kila kuchwapo inakopa na kuwekeza kwenye miradi ambayo si ya uzalishaji. Na zaidi ya yote, katika miradi yote ya maendeleo inayobuniwa kila mwaka, hakuna hata mradi mmoja unaolenga kuwaendeleza wananchi wa vijijini. Miradi yote inaangalia Dar, na maeneo mengi ya mijini. Hakuna miradi ya maji vijijini, hakuna miradi ya afya, barabara etc. Na huko vijijini ndiko kwenye watu wengi zaidi. So ukija kutafuta wastani wa vipato unakuja kukuta hata tugawanye kile kipato cha matajiri wakubwa wa Dar bado hakitoshi kutuweka pazuri. Wenzetu Rwanda wamakuja na mkakati wa kupeleka maendeleo vijijini.

Lakini tangu Kikwete aingie madarakani amekuja na style ya aina yake ambayo ni ya kutoa misamaha ya kodi na kuruhusu wizi wa waziwazi katika sekta mbalimbali huku akishindwa kuchukua hatua. Style ya uongozi ya Kikwete inawapa watu nafasi ya kuendelea kuhujumu mbinu za uzalishaji na kuvuruga mfumo wa uchumi wa nchi. Kama kwa mfano Tanesco walinunua nguzo za umeme kwa sh. 5000 kule Njombe halafu wakazipeleka Mtwara wakapakia kwenye meli na kuziandikisha kwamba zimeagizwa kutoka South Africa na kila nguzo ikalipiwa 200000, mwisho wa siku hakuna aliyewajibishwa tutegemee nini? Kama serikali imeambiwa kabisa tena kwa ushahidi kwamba kuna watu wameficha mabilioni uswisi inashindwa kuchukua hatua unafikiri ni mabilioni mangapi mengine yameibwa ambayo yumkini yangetunzwa yangeweza kutumika kujenga viwanda vidogovidogo huko vijijini?

Mfumo wa usalama wa taifa ni mbovu na uliokosa mwelekeo kabisa. Laiti ningekuwa mimi, hii idara ilikuwa ni ya kuivunja na kuanza kuajiri upya na kwa training mpya kabisa. Waliopo sasa ni wachumia tumbo ambao pamoja na kwamba jukumu lao mojawapo ni kuilinda nchi dhidi ya hujuma zozote za kiuchumi. Hii mijamaa imeruhusu watu wacheze na pesa yetu wanavyojisikia, pasipo kuchukua hatua yoyote wala kushauri jambo lolote. Badala ya kushughulikia matatizo yanayohusu usalama wa nchi ikiwemo usalama wa chakula, vita na uchumi, wenyewe wanashughulika na kung'oa watu meno.

Ndani ya miaka saba tu tangu Mkapa aondoke madarakani, ambapo Tanzania ilikuwa ni ya pili kwa Kenya kiuchumi tayari imeshashuka hadi kufikia kuwa ya nne. Huu ni ushahidi kwamba katika Africa mashariki Tanzania ndiyo nchi yenye Rais mbovu kuliko wote. Rais ambaye anapenda starehe kuliko ubunifu wa kujenga uchumi imara wa nchi. Rais ambaye kila leo yupo tu kwenye ndege anakwenda kutarii na kuuza sura kwa kutumia pesa za walipa kodi wa Tanzania. Rais asiye na hata uchungu na maisha ya watanzania zaidi ya kuchekelea kuona familia yake ikiendelea kustawi na kuimarika kiuchumi.

Kiujumla, pamoja na mambo mengi yanayoweza kuwa yamechangia kushuka kwa uchumi wa Tanzania, kuwa na Rais asiyejielewa ni kwanini anaitwa Rais ni tatizo kubwa zaidi kwa nchi yetu.

Nimeelezea kimtizamo zaidi. Wataalamu wa uchumi msije mkanirushia mawe.
 
Naona umeweka asilimia tu, wala hatujui asilimia hizo zimepatikanaje na kipimo gani cha umasikini kimetumika! Bila kupata ufafanuzi wa haya tutakuwa tunachangia kisiasa na kiuzushi zaidi kuliko kiuchumi
Hicho ni kipimo cha kawaida cha umasikini, ambacho kinatumia hesabu ya idadi ya wananchi wanaoishi kwa matumizi chini ya $1.25 kwa siku (Sh. 2040 hivi) au Sh. 61,000 kwa mwezi (hii ni kwa mtu mmoja si kwa familia), kugawanya na raia wote nchini.

Kinatumika kipimo hicho kwa kuwa kinatoa uwiano wa watu walio kwenye hali ngumu ya maisha kulinganisha na raia wote nchini. Benki ya Dunia wana ofisi zao hapa kwetu, na bila shaka walitumia data za sensa pia, na wana ushirikiano wa karibu na Benki Kuu yetu na Wizara ya Fedha.
 
Mkuu Mtu wa Shamba, katika CC nafikiri ulimsahau ZeMarcopolo, Sumu, bungeni, Wingu, Atongwele etc ambao wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii na wana pua lakini hazinusi kwamba CCM inaimaliza nchi.

Lugha ya namna hiyo haifai.

Sidhani kama mjadala huu umedhamiriwa in context ya kutaka kuwe na kubishana. Huu mjadala umeletwa tujadili sio tubishane. Lugha yako inachochea mbishano. Jifunze kuwa kila kitu na mahala pake...
 
Kubishana ndiyo mjadala wenyewe ZeMarcopolo. Wewe unafikiri kutakuwa na mjadala kama hakuna kubishana? Anyway ilikuwa kama ni joke, na ndiyo maana mstari uliofuata niligeukia kwenye hoja nilizotaka kujadili. Sasa twende kwenye mjadala, achana na huo utani mwingine. Nakujua daima kwenye mambo ya msingi huwa unapunguza ushabiki wa kichama. Twende kazi.
 
Pamoja na mambo mengine utekelezaji wa mwongozo wa azimio la Zanzibar wa mwaka 1991 umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza gap kati ya msikini na tajiri nchini. Ni wazi kuwa mwongozo/azimio la Zanzibar lilikuwa ni sehemu ya CCM kujiandaa na sera za vyama vingi pamoja na kukubaliana na hali ya uchumi duniani, lakini kwetu umetuletea hii hali tunayoona ya masikini kuwa wengi na watu wachache kunufaika na njia kuu za uchumi.

Kwa waliofuatilia mazishi ya The Baroness of UK watakumbuka kuwa sera zilizoinfluence kuwepo kwa mwongozo wa Zanzibar zimesababisha mpaka kiongozi mkuu wa UK azikwe katika mazingira tatanishi.

Sera zetu za sasa zinalenga kujenga tabaka la mabepari ili washike njia kuu za uchumi. Ukisona nakala za kikazi na za kisera za chama cha mapinduzi jambo hilo haliruhusiwi, lakini iin practice hicho ndicho kinachofanyika.

Vilevile yapo madhara yanayosababishwa na ukwepaji wa kodi na wizi. Hapa ninazungumzia pesa zinazotolewa kwenye mzunguko na kufichwa nje ya nchi kwa vile upatikanaji wake haukuwa wa halali au kwa vile mmiliki wake anahofia jambo. Pesa hizo badala ya kutoa ajira Tanzania zinakwenda kuajiri watu wa nchi zilikopelekwa. Siwezi kutaja exact figures hapa lakini ni pesa nyingi sana za watanzania wanaoishi Tanzania ziko nje ya nchi.

Katika hili tunaona siasa zetu nazo zinachangia. Tunasikia wanasiasa wanazungumzia tukiingia madarakani fulani tutamfilisi etc. Ndio maana watu wanaogopa kuweka fedha zao nchini hata zile halali. Labda tujifunze siasa za kuheshimu sheria kuliko kutishiana kufilisiana. Nakumbuka mimi hapa JF several times "nimepigwa biti" kuwa chadema ikiingia madarakani (something which obviously wont happen) zemarcopolo nitakimbilia Msumbiji. Sasa unfortunately mimi kwenye account as I write nina sh. elfu 50. Ningekuwa na billions maybe ningeshawishika kuzitanguliza huko Msumbiji.

Ingependaza zaidi tungepata table inayoonyesha trend in the past 20 years ya gap ya masikini since azimio la Zanzibar kupitishwa.
 
Ni kushindwa kuweka vema vipaumbele.

Pamoja na kuwa uchumi unakua, sekta ya kilimo inarudi nyuma. Takwimu nilizo nazo za hali ya Uchumi ya Tanzania zinaonesha kuwa pato letu toka Kilimo katika Biashara ya nje linapungua licha ya bei kuongezeka:

Mwaka 2010 Tanzania ilipata $101.2 tokana na mauzo ya Kahawa nje wakati 2009 tulipata US $ 111.2 tokana na zao hilo, licha ya bei ya kahawa kuongezeka toka $1,984.6 kwa tani 2009 hadi $2,852.4 kwa tani. Hii ina maana uzalishaji wa Kahawa ulipungua.

Vilevile Pamba, tulipata mapato ya $84 milioni kutokana na mauzo ya pamba mwaka 2010 kulinganisha na $111 milioni 2009. Na hapa pia ni baada ya bei ya pamba kuongezeka toka wastani wa $1,117 kwa tani mwaka 2009 hadi $1,241.8 kwa tani mwaka 2010. Hapa tena uzalishaji wa pamba ulipungua.

Kwa zao la chai, pato la mauzo ya nje ya chai lilipungua toka US $47.2 millioni 2009 hadi US $ 34 millioni 2010. Hapa pia bei kwa tani iliongezeka katika soko la dunia toka wastani wa $1.538 kwa tani 2009 hadi $1948.7 kwa tani 2010. Maana yake tena uzalishaji ulishuka toka tani 30,600 mwaka 2009 hadi tani 18,700 mwaka 2010.

Karafuu pia, mapato ya mauzo ya nje yalipungua toka $14.4 million hadi $7.6 million kati ya 2009 na 2010, licha ya bei kupanda toka $2,977 kwa tani hadi $3,449 kwa tani. Hapa tena uzalishaji ulishuka toka tani 4800 mwaka 2009 hadi tani 2200 mwaka 2010.

Wakati huo huo, kwa upande wa dhahabu, ambayo wawekezaji wanamiliki 100% hisa za migodi yote (nisahihisheni kama nimekosea) na mikataba inawaruhusu kupeleka kwao pesa zote za faida ya migodi, mauzo ya nje ya dhahabu yalikuwa $1.5 billioni mwaka 2010, juu toka $1.23 billioni mwaka uliotanguliwa, na ongezeko hilo la zaidi ya $200 milioni lilitokana na kuongezeka uzalishaji na bei.

Point yangu ni hii:
Sekta zinayosukuma ukuaji wa uchumi ni sekta zisiyobeba watu wengi. Kilimo, ambacho kina zaidi ya watu 76% kinazidi kushuka kwa kiasi cha mazao yanayozalishwa na kuuzwa ndani na nje. Tutategemeaje maskini wapungue?

Viwanda pia huwa vinasaidia kuondoa watu kutoka sekta isiyo rasmi (informal or subsistence sector) kuingia formal sekta navyo havina msukumo wa pekee.

Ili tuondoe umaskini kwa dhati tunahitaji Mabadiliko ya Vijijini (Rural transformation). Hii, pamoja na mambo mengine ni kuhakikisha kuwa serikali inapunguza matumizi yasiyo ya lazima, ikiwemo mishahara isiyo halisi ya viongozi na magari yao ya fahari, na kuwekeza katika miundombinu ya vijijini (barabara, umeme) na kushawishi wawekezaji wa viwanda vya kuchakata mazao kuwekeza maeneo karibu na wakulima, ili kubadili hali ya maisha ya watu wa huko, na kuwatoa wengi kwenye sekta isiyo rasmi.

Nimetumia data hizo za 2010 na 2009 kwa kuwa ndizo latest nilizo nazo. Na chanzo changu ni Economic Survey 2010 iliyotolewa na Wizara ya Fedha August 2011.

Ntarudi baadaye..
 
Inawezekana kweli kwamba azimio la Zanzibar limechangia sana kuanguka kwa uchumi. Lakini sitaki kukubali kirahisi hivyo. Hivi unajua wakati Mkapa anachukua nchi, Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya saba kwa umasikini kutoka mkiani? Lakini hadi kufikia mwaka 2008, Tanzania ilikuwa imefika nafasi ya 27 kutoka mkiani. Katika miaka yake kumi Tanzania ilizipita nchi 20 kiuchumi. Ukuaji ule wa kasi wa uchumi wa Tanzania ulimfanya mkapa aanzishe ile vision 2025, ambayo Kikwete kaamua kuifunika kabisa, hata kuiongelea anaona aibu. Hilo linanifanya niwe mzito kukubali kuwa hali yetu mbaya ya sasa inatokana na azimio la Zanzibar. Lakini hata tukisema hilo ndiyo sababu, bado nchi kama Kenya, Rwanda na Uganda ambazo zimetupita zinafuata mfumo huohuo wa kiuchumi. So tatizo siyo azimio la Zanzibar, tatizo ni Kikwete.

Hapo kwenye nyekundu ndipo panaponifanya nihoji uadilifu wa idara ya usalama wa taifa nchini. Inawajibika kwa lipi? Katika nchi yenye usalama wa taifa ambao moja ya majukumu yake ni pamoja na hilo. Na hawa watu wapo katika kila idara, si kwenye mabenki, taasisi za kukusanya kodi, na wanaaccess kwenye kila nchi. Ni kwa vipi haya mamboa yanatokea? For sure hali mbaya ya uchumi nchini imechangiwa pia na kitendo cha Kikwete kuanza kuitumia idara ya usalama wa taifa kwa manufaa yake binafsi badala ya manufaa ya taifa.

Kuhusu siasa, wala sidhani kama zinaweza kuwa na mchango wowote. For example tukiangalia siasa za Tanzania, hakuna wakati ambao matajiri wamekuwa na free room ya kujidai na kufanya wayatakayo kama wakati huu wa utawala wa Kikwete. Mkapa aliwafilisi wengi sana lakini alipoingia Kikwete kaachilia tu kila mtu anafanya anavyotaka. Matajiri hawa siku hizi hawalipi kodi, na huku wafanyakazi wa TRA wakipokea rushwa za laki mbilimbili nakuachilia mamilioni ya pesa yaende bure. Tulisikia habari ya bandarini jamaa aliyetaka kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni 100. Sasa utajiuliza huku bandarini si kuna idara ya usalama wa taifa? Wanafanya nini? yanapobainika haya wanachukuliwa hatua gani? Miiko yao ya kazi inasema nini? Viapo vyao vya kazi vinasema nini? Tuna tatizo kubwa sana la kiuongozi katika utawala huu wa Kikwete. Kwa hakika ninatamani hata angeamua tu kujiuzuru hata kesho ili aingie mtu mwignine ambaye ni mbunifu na mwenye uwezo wa kutoa order kama Rais siyo huyu ambaye anaona mambo yanakwenda hovyo anabaki anaangalia tu kwa kuwa tu wanaofanya hayo ni jamaa zake.

Kwa kweli nchi yetu haina Rais kwa sasa. Na kama watanzania wataichagua CCM tena, basi ni dhahiri hii nchi itakuwa ni ya mataahira. Wasiokuwa na hata uwezo wa kureason out.
 
Mtu wa shamba nimezipenda data zako. Angalau hizi zinaprove kile nilichokisema kwenye post namba nne juu ya namna ambavyo serikali ya Tanzania imekitelekeza kilimo ambacho ndicho kinachochangia kwa kiasi kikubwa kipato cha watanzania wa vijijini ambao ni majority.
 
Inawezekana kweli kwamba azimio la Zanzibar limechangia sana kuanguka kwa uchumi. Lakini sitaki kukubali kirahisi hivyo. Hivi unajua wakati Mkapa anachukua nchi, Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya saba kwa umasikini kutoka mkiani? Lakini hadi kufikia mwaka 2008, Tanzania ilikuwa imefika nafasi ya 27 kutoka mkiani. Katika miaka yake kumi Tanzania ilizipita nchi 20 kiuchumi. Ukuaji ule wa kasi wa uchumi wa Tanzania ulimfanya mkapa aanzishe ile vision 2025, ambayo Kikwete kaamua kuifunika kabisa, hata kuiongelea anaona aibu. Hilo linanifanya niwe mzito kukubali kuwa hali yetu mbaya ya sasa inatokana na azimio la Zanzibar. Lakini hata tukisema hilo ndiyo sababu, bado nchi kama Kenya, Rwanda na Uganda ambazo zimetupita zinafuata mfumo huohuo wa kiuchumi. So tatizo siyo azimio la Zanzibar, tatizo ni Kikwete.

Hapo kwenye nyekundu ndipo panaponifanya nihoji uadilifu wa idara ya usalama wa taifa nchini. Inawajibika kwa lipi? Katika nchi yenye usalama wa taifa ambao moja ya majukumu yake ni pamoja na hilo. Na hawa watu wapo katika kila idara, si kwenye mabenki, taasisi za kukusanya kodi, na wanaaccess kwenye kila nchi. Ni kwa vipi haya mamboa yanatokea? For sure hali mbaya ya uchumi nchini imechangiwa pia na kitendo cha Kikwete kuanza kuitumia idara ya usalama wa taifa kwa manufaa yake binafsi badala ya manufaa ya taifa.

Kuhusu siasa, wala sidhani kama zinaweza kuwa na mchango wowote. For example tukiangalia siasa za Tanzania, hakuna wakati ambao matajiri wamekuwa na free room ya kujidai na kufanya wayatakayo kama wakati huu wa utawala wa Kikwete. Mkapa aliwafilisi wengi sana lakini alipoingia Kikwete kaachilia tu kila mtu anafanya anavyotaka. Matajiri hawa siku hizi hawalipi kodi, na huku wafanyakazi wa TRA wakipokea rushwa za laki mbilimbili nakuachilia mamilioni ya pesa yaende bure. Tulisikia habari ya bandarini jamaa aliyetaka kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni 100. Sasa utajiuliza huku bandarini si kuna idara ya usalama wa taifa? Wanafanya nini? yanapobainika haya wanachukuliwa hatua gani? Miiko yao ya kazi inasema nini? Viapo vyao vya kazi vinasema nini? Tuna tatizo kubwa sana la kiuongozi katika utawala huu wa Kikwete. Kwa hakika ninatamani hata angeamua tu kujiuzuru hata kesho ili aingie mtu mwignine ambaye ni mbunifu na mwenye uwezo wa kutoa order kama Rais siyo huyu ambaye anaona mambo yanakwenda hovyo anabaki anaangalia tu kwa kuwa tu wanaofanya hayo ni jamaa zake.

Kwa kweli nchi yetu haina Rais kwa sasa. Na kama watanzania wataichagua CCM tena, basi ni dhahiri hii nchi itakuwa ni ya mataahira. Wasiokuwa na hata uwezo wa kureason out.

Kwanza kabisa naomba tuwekane sawa juu ya mjadala ulio mbele yetu.

Mjadala wetu ni kujadili asilimia kubwa ya watanzani kuwa masikini kuliko nchi za jirani yetu. Masikini kuwa wengi na uchumi kuwa dhaifu ni vitu viwili tofauti. Nchi tajiri inaweza kuwa na masikini wengi zaidi kuliko nchi masikini. Ukisoma habari iliyowekwa unaona kuwa Kenya ni tajiri kuliko uganda lakini Kenya kuna masikini wengi kuliko Uganda.

Kwahiyo tunachojadili hapa ni mgawanyo wa njia kuu za uchumi. Keki ya taifa anakula nani? Je, tunakula wote au wanakula baadhi tu. Hapa hatujadili ukubwa wa keki, tunajadili mgawanyo wake. Kwahiyo maelezo kuwa kipindi cha Rais fulani uchumi ulikuwa juu kuliko kipindi kingine yana umuhimu wa nyongeza tu na si vinginevyo.

Kuhusu Kenya kufuata uchumi wa kibepari, nimesema sisi tunafanya kwa kufichaficha kwa hiyo hata mfumo unachelewa kuwa mature. Tunaongea ujamaa, tunaishi ubepari which means hata mifumo mingine haiwekwi kwenda sambamba na ubepari ndio maana kunakuwa hakuna balance of matters. Wakenya wameshakubali kuwa mfumo wao ni ubepari kwa hiyo kuanzia thinking yao mpaka matendo yako hivyo. Sisi watu wetu masikini tunawaweka katika mkao wa kufikiria ujamaa utawaokoa halafu unawaacha wanabaki katika hali ngumu. Pengine tungeweka bayana kuwa mambo ni ubepari wangejua cha kufanya.

Leo Bungeni Mbunge mmoja wa Shinyanga akichangia bajeti ya Kilimo na Chakula alisema watu wake wa Shinyanga wameambiwa na serikali kuwa wakipatwa na njaa wataletewa chakula, lakini chakula kilichopelekwa hakitoshi. Akasema kama serikali haina uwezo ni bora iwaambie tu wananchi tangu awali kuwa watajijua wenyewe ili wasikae wakitegemea kuokolewa na serikali ambayo haja inapotokea haiwasaidii.Hapa unaona anachokisema huyu mbunge kuwa iwapo watu wa Shinyanga tangu awali wangejua hakuna ujamaa ingebidi watafute back up zao wenyewe. Wakenya wametafuta bck ups zao wenyewe long enough ndio maana they are better off.

Vision 2025 haijaachwa. Inatekelezwa na ndio dira ya serikali katika mipango yake. Kuna siku nilipata kusema humu kuwa ni muhimu sana kwa nchi yetu kuhakikisha inaendelea kuwa stable mpaka mwaka 2025 ili kuona kama vision 2025 itafanikiwa. Iwapo itafanikiwa itakuwa ni jambo lenye umuhimu mkubwa sana kwa future ya taifa letu.Nilisema hivyo kuwaonya vijana waliokuwa wanatamani mapinduzi ya utawala kwa njia za maandamano kama zile za Libya, Tunisia na Misri. Kwahiyo siyo ukweli kwamba vision 2025 imeachwa.

Pamoja na kuwa lengo la thread sio kufananisha marais lakini umeongelea jambo ambalo nalazimika kuligusia. Unasema Rais Mkapa alifilisi matajiri. Jambo hili sio kweli hata kidogo. In hi own words Rais Mkapa amepata kusema kuwa iwapo Nyerere atafufuka atashangaa kuona tabaka la matajiri alilolitengeneza na sehemu kubwa ya mashirika ya umma aliyoyabinafsisha. Kuanzia mwaka 1991 baada ya mwongozo wa Zanzibar idadi ya matajiri (baadhi ya wanazuoni wanawaita matajiri uchwara) imekuwa ikiongezeka. Hakukuwa na ufilisi wa matajiri kama sera ya serikali. Kitu pekee ambacho Mpaka alijaribu kukifanya ni kujaribu kupunguza wafanyabiashara wanaogombea ubunge ndio kina Adamjee, Abood na wengine wakaenda na maji (ingawa mitaani kuna sababu nyingine zilikuwa zinazungumzwa in case of Adamjee).

Nyongeza: Kwavile kwenye mchango wako several times umefananisha marais wawili Kikwete na Mkapa, naomba nitoe angalizo hili. Ilani ya uchaguzi ya CCM haitengenezwi na mgombea. Inatengenezwa na kupitishwa na vikao vya chama kabla hata mgombea hajapatikana. Mgombea akipatikana anakabidhiwa ilani iliyotengenezwa tayari. Mwaka 2005 Kikwete alikabidhiwa ilani iliyotengezwa chini ya mwekekiti wa chama Rais Mkapa. Hapa utaona mfumo wetu ni tofauti na ule wa Marekani ambao mgombea anatengeneza blue print ya sera zake tangu kura za maoni na akishinda hizohizo ndio zinakuwa sera za serikali. katika awamu ya pili tayari Rais anakuwa ameshakuwa mwenyekiti wa chama na anakuwa na influence kubwa na contents za ilani. Kwahiyo kwa Tanzani kumlaumu Rais in his name si sahihi. CCM kama chama inapenda hii tabia ya watu kumlaumu Rais kama jina kwa sababu akiondoka chama kikiweka mtu mwingine anaonekana ni baggage free, lakini as matter of fact ilani ya mwaka 2005-2010 iliyokuwa inatekelezwa kikwete hakuwa na influence kubwa za uundwaji wake. Iwapo ilani ya 2010-2015 sio nzuri hapo inakuwa sahihi kumlaumu Kikwete. Kwahiyo kucompare marais wawili wa CCM kusema mmoja alikuwa na sera nzuri mwingine sera zake sio nzuri CCM ni jambo linalopendwa ila haireflect uhalisia wa mambo yanavyofanywa.
 
Mimi sio mchumi ila naongezea tu kwa uhalisia wa maisha yanayotuzunguka. Kipato cha mtanzania wa kawaida kinategemea zaidi kilimo sio ajira, na hii ni karibia dunia nzima ajira zimekuwa adimu. Sasa kwetu hapa kilimo na biashara serikali haijawekeza kabisa, maskini mtji wake ardhi na vimifugo ktk hivi hakuna benki wala shirika linalokubali kumkopesha.

Mabilioni ya Kikwete yapo mjini kwa mama lishe na wengineo waliosajili biashara ndogo za mkono kwenda kinywani hawakwamuki. Mkulima na ardhi yake angewezeshwa kwa kupewa hati na kulima eneo kubwa kiutaalamu nchi ingeinua kipato cha wengi sana. Hata kati yetu tuna vishamba hapa, viwanja tungewezeshwa mikopo tungeacha hata hizi ajira fresh graduate wakafanya ila ndo hivo mikopo ni vimeo interest 20% ni kubwa sana.

Ukija tena upande wa pili serikali inanyang'anya ardhi kwa maelfu na kuwahamisha kwa fidia ndogo bila kujali ilivyowaathiri kiuchumi na wachache wanaopewa kwa kigezo cha uwekezaji hawalipoi kodi itakayoinua uchumi wa wengi ila inaenda kwenye account za wachache. Gap ni kubwa na inazidi kukua, wakulima ambao ndo asilimia kubwa wanazidi kudidimia hata kidogo wanachovuna hawaruhusiwi kuuza nje kinaozea shambani au kuuzwa kwa stakabadhi ya mwaka mzima. Hawawezi kusomesha watoto wao na hivyo vicious cycle inaendelea kizazi hadi kizazi.

Ni hayo tu kwa leo lakini kuna mengi ukichanganya rushwa na mabadiliko ya hali hewa, huduma za msingi kama maji, umeme na matibabu kupanda ni kongwa kubwa kwa maskini kujikwamua.
 
Naona umeweka asilimia tu, wala hatujui asilimia hizo zimepatikanaje na kipimo gani cha umasikini kimetumika! Bila kupata ufafanuzi wa haya tutakuwa tunachangia kisiasa na kiuzushi zaidi kuliko kiuchumi

wewe usijitowe fahamu uchumi ni siasa
 
wewe usijitowe fahamu uchumi ni siasa
Siziamini hizo data mpaka zichapishwe na nizione, au nipewe link ya kuziona hizo data.
Ni ulimbukeni kuamini bila kuhakiki hasa haya magazeti uchwara. Siyo kila usomacho ni kweli.
IMF hawana data kama hizo .... I stand to be corrected.
 
Hicho ni kipimo cha kawaida cha umasikini, ambacho kinatumia hesabu ya idadi ya wananchi wanaoishi kwa matumizi chini ya $1.25 kwa siku (Sh. 2040 hivi) au Sh. 61,000 kwa mwezi (hii ni kwa mtu mmoja si kwa familia), kugawanya na raia wote nchini.

Kinatumika kipimo hicho kwa kuwa kinatoa uwiano wa watu walio kwenye hali ngumu ya maisha kulinganisha na raia wote nchini. Benki ya Dunia wana ofisi zao hapa kwetu, na bila shaka walitumia data za sensa pia, na wana ushirikiano wa karibu na Benki Kuu yetu na Wizara ya Fedha.

Mtu washamba, kipimo hiki ambacho kimetokana na kipimo cha awali cha international poverty line ni kipimo ambacho wachumi nguli wa maendeleo wanakipinga na hakika ni kipimo dhaifu cha kupuuziwa.

Kipimo hiki kinalazimisha tupime utajiri au umasikini kwa kutumia ela(monetarization of aspects of life). Kipimo hiki hakijali non-marketable goods, behavior, na life-style ambazo zina umuhimu mkubwa kwenye maendeleo. Mfano kwa mujibu wa kipimo hiki Africa haikuwa na maendeleo yeyote wakati wa batter trade (bihashara ya kubadirishana bidhaa). Huko vijijini wakulima wanabadirishana mazao, mifugo ili kumudu maisha yao ya kila siku. Kipimo hiki kinawahukumu kuwa ni masikini. Kisa? Hawatumii ela na kama wanatumia ni chini ya dola moja.

Kipimo hiki wala akioni kuwa furaha, amani, upendo baina ya dini na makabila mbalimbali kuwa ni sehemu ya maendeleo kwa sababu vitu hivi havina thamani ya kifedha. Anayeishi kwa dola 100 kwa siku kwenye nchi ya vita au anayeishi kwa dola 200 kwa siku kwenye nchi isiyo na furaha na upendo kwa mujibu wa kipimo hiki yeye sio masikini.

Kipimo hiki wala hakifuatilii dola hizo kwa siku zinatumika zaidi wapi. Kana kwamba watu wote wana matumizi sawa na kuona maendeleo kwa definition moja. Jiulize mtu anayeishi New York na anayeishi kajificheni mashambani nani ataweza kuishi bila ela? Sasa ikitokea anayeishi New York kwenye "ela nyingi" na anayeishi kajificheni wote wakapewa kiasi sawa cha ela za kujikimu kwa siku, yupi anauwezo mkubwa wa kubaki na salio? Ni yule wa kajificheni maana mahitaji mengi ya chakula yapo ndani ya nguvu zake. Sasa kwanini wote wapimwe kwa kipimo kimoja? Ukoloni mamboleo.

Vile vile hao World Bank watupe sampling techniques walizotumia. Lakini cha msingi watupe justification ya kuchagua kipimo hiki. Justification ya kisayansi.
 
wewe usijitowe fahamu uchumi ni siasa

Duh! Uchumi ni Siasa? Hii inafundishwa shule gani na somo gani? Najuwa somo linaloitwa political economics ikiwa na maana ya mchanganyiko wa vitu viwili tofauti. Hii ya uchumi=siasa utakuwa umeanza wewe.

Ukianzisha biashara manake umeanzisha siasa? Ukianza kuuza mitumba ni siasa? Exports na imports ni siasa? Kipato chako cha mwaka ni siasa? Hatuwezi wote tukawa sahihi kwa hili; moja wetu hayuko sahihi.
 
Back
Top Bottom