ZITTO KABWE AUMBUKA.
Kampeni yake chafu dhidi ya Tanzania yakwama.
_
Benki ya Dunia yaidhinisha Mabilioni ya fedha za kusaidia Elimu alizotaka Tanzania inyimwe.
Saa chache zilizopita Benki ya Dunia kupitia Bodi ya Wakurugenzi Watendaji ya Chama cha Maendeleo ya Kimataifa (IDA) imefanya maamuzi ya kihistoria ya kuruhusu mkopo wa Dola za Marekani Milioni 500 utolewe kwa Tanzania kwa ajili ya kusaidia kuboresha elimu ya Sekondari baada ya mjadala mrefu uliochukua miezi zaidi ya mitatu.
Uamuzi wa Benki ya Dunia umezima kampeni ya kidhalimu iliyofanywa na Mwanasiasa mpuuzi Zitto Kabwe aliyeandika barua kwenda benki hiyo akitumia nembo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka Tanzania inyimwe mkopo huo bila kujali athari zake kwa wananchi hasa wanyonge na maskini.
Zitto Kabwe akishirikiana na mabeberu wanaomfadhili alifanya uharamia kwa kuchochea uongo kuwa Tanzania inakandamiza wanafunzi wa kike kwa kuwanyima fursa ya kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito ilihali anajua kuwa sio kweli na kuna utaratibu ulio wazi wa watoto hao kupata elimu kupitia programu mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima, Mpango wa Elimu kwa walioikosa na vyuo mbalimbali.
Hili ni pigo jingine baya sana kwa Zitto Kabwe na washirika wake ambao wamekuwa wakiichonganisha na kuichafua Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Kitamaifa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa bila kujali athari ambazo wananchi wanazipata kutokana na kuinanga Tanzania ama kukwamisha miradi mikubwa na washirika wa maendeleo.
Katika safari ndefu ya mjadala ambao ulianza tangu Januari mwaka huu wa 2020, Benki ya Dunia imepiga chini msimamo wa mabeberu waliotaka Tanzania inyimwe fedha hizo baada ya kuingizwa mkenge na Zitto Kabwe.
Watu wengi wanaweza kujiuliza kwa nini Zitto Kabwe na wafadhili wake walikuwa wanashupalia Tanzania inyimwe fedha hizo? Ukweli ni kwamba Zitto na wadhalimu wenzake hawakuzuia fedha hizo kwa sababu ya kupigania wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shule kama wanavyodai, bali walishupalia Tanzania isipewe fedha hizo baada ya msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano kukataa kukopeshwa fedha ambazo zingeingizwa nchi kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na miradi ambayo haina matokeo kwa wananchi ili baadaye zitumike kwa maslahi ya siasa za upinzani na sio wananchi.
Kwenye hili, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Jemedali Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli inastahili pongezi za dhati kwa msimamo thabiti usiyoyumba na ushindi mkubwa dhidi ya kibaraka Zitto Kabwe na washirika wake ambao wamekuwa wakipiga tripu kwenda mabeberu hao kufanya kampeni ya kuiangamiza Tanzania eti wakitaka kuiondoa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.
Kongole Rais Magufuli, hongera Watanzania wote kwa ushindi huu mkubwa. Zitto Kabwe na washirika wake washindwe na walegee.
Sasa Tanzania itapata Dola za Marekani Milioni 500 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 135 kwa ajili ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu ya Sekondari, kuboresha mazingira ya elimu kwa wasichana na kuinua ubora wa elimu kwa wasichana na wavulana.
Mkopo huu ni wa gharama nafuu na sio fedha za bure. Watanzania watazilipa, lakini sasa watalipa fedha ambazo zinakopwa na kuelekezwa kuwasaidia mamilioni ya Watoto wa Tanzania na sio kwenda kwenye NGO na miradi ya kupitisha fedha zinazokwenda kwa wachumia tumbo akina Zitto Kabwe na washirika wake.
Tunaamini Serikali ya Tanzania itatoa mchanganuo wa fedha hizi zinakwenda wapi na zitawanufaishaje Wanzania.
Kila la kheri Watanzania na pole sana Zitto Kabwe kwa kuangukia pua katika mchazo huu mchafu. Tambua kuwa Mwenyezi Mungu husimama na wenye haki na katika hili amesimama na Watanzania wenye haki na Rais wao mpendwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
Taarifa hii haina uhusiano na siku ya Wajinga Duniani. Ni ukweli mtupu na inapatikana katika tovuti mbalimbali za Kimataifa. Waweza kuisoma hapa kwenye tovuti ya Benki ya Dunia yenyewe
New Financing to Make Secondary Education Safer, Better, and More Accessible for Tanzanian Girls and Boys
Mwl. Damas Masele MPJ
Mkufunzi Mstaafu.
31 Machi, 2020.
Sent using
Jamii Forums mobile app