World Cup 2010 SA: Match updates (From June 11)

Lakini hii Brazil ya mwaka ni sifuri hawatoki wakikutana na wajerumani hawa
 
Hii mechi ikiisha hivi gang chomba atakuwa vindicated......
 
Du dakika ya 20, no goal jamaa wamekaza, sijui watakomaa hadi mwisho!
 
Brazil ya mwaka huu nayo inaonyesha udhaifu, haiwezekani mcheze na timu mbovu kama hii mpaka sasa hamjafunga hata goli moja, kama ni hv watapata tabu kwa ivory coast na ureno
 
Jamani jamani wamo hawa.... Ona hayo mashuti! Utafikiri urefu wao haugawanywi mara ya tatu ya ule wa Hasheem Thabit lol...
 
Nimempenda mkorea alokuwa analia akiimba wimbo wa taifa 🙂

Umeona eh! Kuna wengine huwa wanaguswa sana na nyimbo zao za Taifa mpaka huangusha mchozi.
 
n.korea wanacheza 5-4-1 formation........brazil wana kazi leo........inabidi watumie very quick passes and movements
 
n.korea wanacheza 5-4-1 formation........brazil wana kazi leo........inabidi watumie very quick passes and movements
Wanawanyima nafasi lakini hii style mara nyingi mabeki wanaishiaga kuchoka kwa vile inaleta mashambulizi mengi,baada hapo wakichoka ndio mvua inaanza sasa ya magoili manake wakiachia kimoja watalizika na wao kupanda.
 
I believe!...
brazil kuganda golin kwa n.korea kutazaa goli mana always mgagaa na upwa hali wali mkavu!...but pia naamin N.korea waweza kufunga kwa counter attack...nimeliona hili pia!
 
Robinho anapiga vyenga tu no malengo. Ila jamaa hawa nao wafupi sana kona na mipira ya juu wanasumbuka sana
 
mie nahisi alikuwa anakumbuka tu matatizo ya nchini kwao.

Basi huyu yuko emotional sana,au mara ya kwanza anacheza WC nini..sijawahi kulia nikiimba wimbo wa taifa..
BTW,yani mpaka sasa Brazil hawajafunga goli ina mana hawa N.Korea ni wakali hivyo?!..ha ha
 
kama kawaida unaweza kusubiri basi saa nzima lisije ila likija yanakuja matatu.....brazil wakifunga moja itafuata mvua ya magoli....
 
40mins gone 0-0.......C'MON KOREA............GO KOREA GO...........
 
Ila kubutua nako wanabutua! Toka hii mech imeanza! Sanaaaa cjui kwa kuwa kujaribu si kushindwa!! Haaa! Yani goli liko kati butuo linapaa juu tena pembani yagoli kulia/kushoto...duuu..
 
Brazil bila kujaribu mikwaju ya nje watanasa.pale golini wanapotaka kulazimisha kuingia kumejaa wa korea kinoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…