World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Hata kushangilia hawajashangilia,da kwa kweli ajabu na kweli
 
Defence yao ni mbovu sana nadhani kuliko timu yoyote ile katika mashindano haya. Ujerumani hawakucheza mpira wa kutisha ila nafasi zote walizozipata leo wamezitumia vizuri.

Na siamini hiki kisago ni kwa ajili Neymar Jr na Thiago Silva kutokuwepo.

Kwa jinsi walivyocheza defense leo hata wangekuwa na Pele, Zico, Romario, na Ronaldo....wangefungwa tu.
 
Jamanii Huu si Udhalilishajii sasa 7-1
Hamna haki za binadamu hapa...
 
Kila timu nayoshangilia inafungwa WorldCup hii bora kesho niwe Argentina ili Holland ipite.

hahahaha mkuu juzi ulisema upo ujerumani imekuwaje ukabadili kukimbilia Brazil?
 
Brazil walifanya makosa wakajichanganya mapema sana, hawa wauaji kina Hitler wakatenda yao. Wameogopa hata kushangilia
 
Naomba ufafanuzi inakuwaje mechi ya robofainali timu ichapwe 7 kwa 1,ina mana mpaka imefika robo ilibebwa au
 
David luiz kapga goti na kumshukuru kwa kuwanusuru na aibu ya magoli 10
 
Oscar anaifungia Brazil bao lake la 11 tangu aanze kuichezea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…