World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

haa haaa mweeeh !!!
 
Last edited by a moderator:
Imetosha Mkuu kwa leo, wacha tusubiri mchapo mwingine in few hours, natumai huo utakuwa patashika nguo kuchanika kwa dakika 90/120 na labda kwenye matuta.

Nawakumbusha maneno yao tu Mkuu
 
Naona uoga umetoka wote, yaani kama wachezaji wao wameweza kuvumilia dakika 90 ngoja na mie nivumilie. Ila wanajua kabisa wananchi watalipuka
 
Reactions: BAK
Ntashangaa sana kama Dante na Fred hawajapelekwa mahakamani leo

Wale watu ni wauaji kabisa. Ila atakuwa amelipwa na Bayern kuharibu mechi jana mi nilishauri wachomwe moto
 
...Wanatamani wasogeze 2018 iwe mwaka kesho 🙂🙂 lakini ndiyo hivyo tena, sasa ni kutafakari kwa kina wapi walipokosea na kuanza upya kuisuka timu ya 2018.

Defence yao majina makubwa tu haina kitu pale yaani hata mie ningewafunga
 
Reactions: BAK
nilisema humu !
Brazili kimpira haifik fainali
ila kiftna itafika!
sasa wamefanya fitna weeeee kwa wier ist futbal wamechemsha!
Andybird231 sijui yu wapi yaillahi

Dah wewe acha tu, niliumia goli la kwanza ila la pili lilipoingia nikawa nachat hapa mara magoli 5 nikasema hii ni PS bana sio real football. Mie nasubiri Brazil acheze maana kombe la dunia halijaanza.
Hali ilikuwa mbaya sana. Kama ningelala na kukuta matokeo ni haya nadhani ningedondoka
 
Last edited by a moderator:
Hawana jinsi zaidi ya kuanza kulia

Jana ilikuwa mauaji ya Hitler dhidi ya Jews, hawa watu sio wazuri. Unajua mkubwa mwenzako huwezi mpiga vile mbele za watu hata kama kalala na mkeo
 
Nimehamia rasmi Argentina sasa....

Messi legoooooooooooooooo

Nataka sana kombe libaki Americas

Kweli Bora libakie huko America hata liwapoze maana likienda mbali zaidi ya hapo ni hatare, ila Messi akichukua itakuwa balaa sana aisee. Robben mmmh, German mmmmmmmmh
 

Mabeki wale na kocha wao wamechangia kiasi kikubwa kushindwa kwaonna ikitokea fujo basi wachezaji wapelekwe mahakamani pamoja na CBF
 
Mie kuna mtu wangu ni mpenzi sana wa Brazil, basi mechi inaanza akanitumia text kufurahia game na kudai ushindi ni kama kawa nami nikafanya hivyo baada ya goli la tatu nikamtumia text kumwambia sielewi nini kinaendelea hakujibu, halftime nikamtumia text kimya nikaamua kumpigia simu kimya, hii si kawaida yake nikaanza kuingiwa na wasi wasi mpira ulivyoisha nikampigia simu kimya. Ndiyo nimempata sasa hivi anadai baada ya goli la nne akaamua kulala, kaamka kakuta text messages 200 zikimpa pole kwa kipigo, na missed calls 120. Nafurahi kwamba yuko poa kabisa.

Naona uoga umetoka wote, yaani kama wachezaji wao wameweza kuvumilia dakika 90 ngoja na mie nivumilie. Ila wanajua kabisa wananchi watalipuka
 
Ceasar hajacheza mechi yyt ya maana kwa mwaka na nusu leo anafanywa keeper wa kwanza wa Brazil!Kipa huyu hana hata team ya maana anayoidakia

Yaani mtu alikuwa anachezea QPR ikashuka daraja ndio anadakia Timu Ya Taifa. Mazoea ni mabaya sana, basi yeye alijijengea sifa kwenye penalties
 
Scolari aliichagua team yake miaka 3 iliyopita na wala hakujali viwango vipya!Kocha ajaye amlete Miranda wa Atletico acheze na Silva na Fernandihno!Fukuza Dante na Paulihno lkn muache Luiz kama reserve

Mazoea ni mabaya sana na kujitakia kadinkwa Silva kunawala sana ile sehemu ilikuwa wazi sana na pia kuhusu kujipanga naona inauma sana kuandaa kutumia hela, mashabiki wengi afu mshindwe
 
Neymar na Oscar waitwe kama mido za pembeni na sio kama eti ndiyo unawategemea!Msimamie Pato afanye mazoezi awe striker wa Brazil maana umri bado sana!Then msimamie Dihno apunguze unene asimame na Pato

Kocha mpya ataekuja atapata wakati mgumu sana kwani hawa wachezaji watakuwa wanakumbuka kilichotokea jana
 

Ndugu we mwambie tu kuwa Brazil walipewa faini ya 6 goals kwa kumpiga refa
 
Last edited by a moderator:
Yaani kiukweli hata ingekuwa mie Brazilian jana lazima ningeungana kunukisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…