World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

andybird314 nimekutafuta sana!
pole sana mkuu!
unakumbuka kauli yangu?

Naikumbuka sana yaani nahisi kama ni gundu fulani vile. Ila ndio mpira ukiweka mategemeo sana unaanguka kwa aibu. Brazil wamenifanya hata kazini wanaanza nisumbua na sijaenda hadi sasa
 
Last edited by a moderator:
kwa sasa sina, timu yeyote atakayechukua kombe kati ya walioingia hatua hii poa tu.

Adui mwombee njaa: Ujerumani apigwe tu ametufedhehesha sana.

Nashauri Brazil wasipeleke timu uwanjani katika mechi ya mshindi wa tatu, huenda tukakutana na kipigo kingine kibaya kutoka kwa Uholanzi au Argentina. Wafanye kama Yanga tulivyomkacha Mnyama kwenye mechi kama hivyo kwenye mashindano ya CECAFA, ni afadhali kufungiwa kuliko kukutana na kipigo cha aibu. Brazil waiombe FIFA wasipeleke timu uwanjani kwa madai kuwa wachezaji wamepata 'BRAIN CONCURSION' baada ya kipigo cha milenia kutoka kwa Ujerumani.
 
Tukisema ukweli wale wachezaji wameathirikia kisaikolojia. Mashabiki walilia sana na sidhani kama wataisahau hii siku

Ukiona mtu mzima analia ujue kuna ... Nahisi kuna kipigo kingine kibaya kinatungoja kwenye mshindi wa tatu, chonde chonde wasipeleke timu uwanjani kwa gharama yoyote hata kama ni kufungiwa.
 
Tukisema ukweli wale wachezaji wameathirikia kisaikolojia. Mashabiki walilia sana na sidhani kama wataisahau hii siku

Sisi tu tulioangalia kwenye screen tulihuzunika, Wajerumani wenyewe walivyoona zinafika6 walihuzunika ijapokuwa yule sub aliyefunga goli la 6 na la 7 alitakiwa awaonee huruma! Kibinafsi, mimi naona ni matokeo ya kisaikolojia zaidi.

Moja kwamba Neymar hayupo, hiyo kisaikolojia iliwaathiri.
Pili Thiago Silver, nahodha na mtu muhimu hayupo, ikawatoa kabisa kwenye mstari

Na tatu, kimuhemuhe cha kucheza nyumbani huku ukiwa na Wananchi wakiwatazama unakosa amani. Huwezi kuamini ile mechi ingechezwa nje ya Brasil, hata kama wangefungwa ingekuwa pungufu ya goli7, tuseme pungufu ya goli5!
 

Endelea kuota mchana mama yangu.
 
Neymar asinge hata itwa kwenye team ya Brazil ya mwaka 1998-2006!Pato angesimamiwa angefanya mambo zaidi ya Neymar

Kikosi cha kwanza kama mchezaji Gustavo asingeitwa hata Brazil under 19!Lkn leo Gustavo eti ndiyo mido panga pangua wa Brazil

Neymar ameonesha kiwango kikibwa kwenye WC 2014 kilichoiangusha brasil ni wenzake kina fred na hulk wanatoa msaada mdogo kwenye timu, ila kwa kiwango alichokua nacho sasa ana uwezo wa kupata namba katika taifa lolote hapa duniani
 
Uliskia maneno ya Luiz? aliongea mpaka akatia huruma sana,ukipata ile script embu irushe hapa.

“We wanted to make the people happy but we couldn't do it. Sorry to all Brazilians,” he told reporters after the game.

“Everyone knew how important this was... to see all of Brazil happy.

“They were better than us. It's a day of great sadness. We can only apologise. We are so sorry.

“It’s the end of a dream, and not in the way we wanted. But I will learn from this moment. I'll never give up.”
 
Pia mkuu kumbuka tulibishana sana wewe na wenzako mlikuwa mnamtetea DAVID LUIZ, ..sasa yametimia, karibu kule nyumbani CHELSEA FC THREAD tuendelee na mjadala.:wacko:
Tukisema ukweli wale wachezaji wameathirikia kisaikolojia. Mashabiki walilia sana na sidhani kama wataisahau hii siku
 
Neymar ameonesha kiwango kikibwa kwenye WC 2014 kilichoiangusha brasil ni wenzake kina fred na hulk wanatoa msaada mdogo kwenye timu, ila kwa kiwango alichokua nacho sasa ana uwezo wa kupata namba katika taifa lolote hapa duniani

Mtafutie namba Germany huyu Neymar!Je unajua kama Reus asingeumia ndiyo anaanza Germany pamoja na Muller ambapo akina Klose,Kroos,Gotze,Schurrle na yule mshambuliaji anachezea Arsenal wote wanasubiri benchi!!Hapo dimba ya nyuma kuna mtu anaitwa Gundagan nae kaumia ambapo akiwepo Howdes anasubiri~!!

Hapo Badstubber bado anaumwa!Acha kabisa mkuu Neymar hata reserve hawekwi Germany
 
Acha ushabiki wako neymar ana kiwango kikubwa tu

Uko sahihi ndg..Neymar ni classic sana na hata Oscar mzur pia tatizo lililopo ni beki haikuwa makini katika kukaba hasa beki za pembeni na dante..
 
kwa sasa sina, timu yeyote atakayechukua kombe kati ya walioingia hatua hii poa tu.

Duh!!! Asante sana Katavi,angalau tutashindwa kujua nani atashinda,na wala usiseme hata unapenda nani ashinde,wewe leo kuwa mtazamaji tu,hatukunyanyapai ila tunakupenda sana,umekuwa kama mtabiri humu jamvini.
 
Last edited by a moderator:
yule mshambuliaji anachezea Arsenal wote wanasubiri benchi
Usiumeume maneno...ni Lukas Podolski.

Na kwa taarifa mechi ya jana dhidi ya Brazil haikuwa hadhi yake kucheza! Utamwona siku ya Fainali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…