World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Sio utani mechi kati ya Deutscheland na Brasil iliuma mno mno mpaka nikazima TV baada ya goli la tano kufungwa. Tokea kuanza mechi hizo sijapata kufedheheka kaisi hicho hata zile mechi za wasakatonge wa Cameroon sikujisikia vibaya vile. Je wewe mwenzangu ni mechi gani iliyokupelekea kuzima TV kabla haijaisha sababu ya timu uipendayo kupoteza tumaini la ushindi?
 
Vipi waarabu waliopo Tanzania nao hakuna mwenye hobby ya soccer?Kwa kauli hiyo tunajuaje kama watu weusi wa Argentina wanapenda soccer,maana michezo ni mingi

we umeambiwa argentina walipeleka frontline wafrika kwenye vita wakafa unaongelea hobby ya warabu. Tanzania nayo imewaua warabu vitani.

issue ni kwamba kila mtu anachoice ya mchezo wake huwezi kulazimisha kula mtu akawa mchezaji wa soka
 
Hivi kwani timu ya nchi kutokuwa na watu weusi kwenye kikosi chake ni ubaguzi?

Mimi nadhani kuwaza hivyo au kuangalia mahsusi ili kuona kama kuna watu weusi sehemu, ndo hisia za ubaguzi hizo.
 

Sawa....Ila nilisema toka mwanzo hili kombe lazima libaki Amerika ya Kusini...

#Team Argentina hoyeeeee
 
Last edited by a moderator:
van Gaal Kasema kuna wachezaji wawili wamegoma kupiga Penalt mwanzo ndio Beki akajitolea najaribu kujiuliza ni nani?sababu Penalt mwanzo anapewa mpigaji wanaowazoea wazuri wa kupiga ile za mwanzo alipiga Van a Parsie mwanzo then Robben Then Dirk Kuyt ila safari hii Parsie hakuwepo, inaonyesha waliogopa wanaweza Kuwa Robben au Kuyt wamekimbia Presha, Penalt wengi tunaona rahisi ila kutoka kati mpaka kwenda kupiga sio kitu rahisi sasa hivi ni #TeamArgentina
 
siku Klose alipovunja rekodi ya Ronaldo De lima. Ata hivyo kwangu Ronaldo ni best of the best.
 
Fresh tu...mimi mpira jana sikuangalia kabisa...ila nasikia subs zake jana hazikuwa poa sana..

Ebana bora Kombe liishe turudi katika klabu zetu. Can't wait for post Sunday...
 
Kama ni ubaguzi Germany ni viongozi kwa Western Europe. Hapa tushabikie Kile ukipendacho Kumbe lishe tusubiri 2018 Kama tutakuwa hai. #teamargentina #teammessi
Hata sisi watanzania tunaongoza kwa ubaguzi,unakumbuka yule miss Tanzania mwenye asili ya india?Hoyce Temu alitoa machozi.mpira ni kuhave fun,tukianza mambo ya ubaguzi,binadamu wote ni wabaguzi
 

Mkuu jiulize hivi hata kama weusi wapo argentina ni mweusi yupi ambae ulishawai kumsikia duniani raia wa argentina kanyimwa kuitwa kwenye timu yao ya taifa.?inawezakana yupo iila je mi mweusi yupi tusema ulishawai kusikia anauweza kuliko messi,maschelano,higuain ama yoyote yule kaachwa kisa ni rangi yake.?tavez mwenyew tu haya mashindano anayaangalizia kwenye t.v.waafrica hua tunatabia za kujibagua sijui kwanini.!!juzi hapa timu za africa angalau mbili ziingia hatua ya mtoano lakini watu hawakuisha kulalama kua fifa haiwapendi mara mungu katulaani,mambo kibao wakasahau kua wa asia wao awakupitisha hata timu moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…