World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Namuonea huruma leo baada ya kufungwa watambebesha lawama zote yeye

Leo atawaonyesha wabaguzi wa Italy na jamii yote ya kiitaliano duniani kuwa yeye ndo Striker aliyebaki wa kutegemewa na Azzuri. Waache ubaguzi wakubali kuwa dunia imebadilika waangalie jinsi France, Holland, Belgium, England, Portugal, Germany, Spain walivyofaidika na wachezaji weusi.
 
USA Jumatatu anamchapa Ghana!Siziamini kabisa team zetu za Afrika maana sisi tuna amini sana manguvu kuliko kutumia akili!

Mkuu Malafyale unashangilia chama la wajukuu wa Washington?
 

Kama una chuki na wataliano ni haki yako lakini acha kubwebweja porojo zako hapa, Balloteli ni mzungu?

Haya maneno yako mwenyewe yanaonesha wewe pia ni mbaguzi, kwa maneno ya Nyerere, "Kaburu mweusi"
 
Hivi saa nne ni nani anacheza kati ya costarica na uruguay au Italy na na England? au England na Italy ndo itakuwa hiyo saa saba za usiku? maana sielew elewi hapa

Mods wetu nao sijui wanafikiri wote tuko vizuri kwenye jiografi! Kuna mdau mmoja aliweka ratiba hapa yani full lakini walikoipeleka wanajua wenyewe badala ya kuiweka mwanzo.
 
Kifaa cha Arsenal kinaonyesha macheche hapa, kitawaliza watu EPL msimu ujao
 
Kama una chuki na wataliano ni haki yako lakini acha kubwebweja porojo zako hapa, Balloteli ni mzungu?

Haya maneno yako mwenyewe yanaonesha wewe pia ni mbaguzi, kwa maneno ya Nyerere, "Kaburu mweusi"

Nadhani umenielewa vibaya nazungumzia na kuwapinga wataliano wanaombagua na wasiotaka Baloteli asichezee Italy kwa sababu ni mweusi. Nilichosema ni kitu dhahiri wala sio fikra zangu, wewe mwenyewe unajua jinsi baadhi ya wataliano wenzake wasivyomtaka awe katika timu ya taifa.
 
Japo Italy na England zote sizipendi ila England ndio siipi nafasi kabisa.
 
Uruguay wanapewa penati na kufunga, ni penati ya uhalali kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…