World Cup Qatar 21 November, 2022 nani atabeba kombe?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Ndio ni hiyo jana tumeshuhudia upangaji wa makundi kwa nchi zinazoshiriki Kombe la Dunia hapo badaye mwezi wa November 022 kule Qatar.

Japo kuna baadhi ya mechi bado hazijachezwa, je kwa maono yako nani anaenda kuibuka kidedea na kulichukua kombe kutoka mikononi wa weusi wenzetu Ufaransa Je Ufaransa atalitetea tena?

I my self nategemea upinzani kutoka kwa timu zote mpaka kwa sasa ukiniuliza nani anaenda kubeba hilo Kombe la Kidunia sina majibu kombe la dunia ni zaidi ya kula na wachezaji wenye majina makubwa na sio ajabu mwaka huu ukawa mwaka wa miujiza timu wababe wote wakatolewa mapema au kuishia robo fainali.

Brazil chini ya Tite bado timu haijakaa vizuri wakikutana na timu Ulaya watapata shida timu haichezi kama timu bali wanategemea mchezo mmoja mmoja lile Samba lao limepotea siku hizi wameiga Mpira kwa Amerika ya Kusini kabisa nguvu nyingi akili kidogo wakikutana na timu kama Denmark wanaoutumia akili nyingi wanacheza soka la kitabuni usishangae ukawa mwisho wao kama watakutana robo fainali au Nusu fainali.

Timu za Kiafrika at least Senegal wanaweza kutoa upinzani wa kweli, Cameroon wapo na talented players ila bado naona shida ipo kwenye benchi lao la ufundi hakuna kocha mzoefu pale hawa wengine waliobaki wapige matizi sana.

Je wewe kwa upande wako unatwambia tutegemea nchi gani kuwa bingwa wa kombe la dunia 2022?
 
Germany
Netherlands



[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Wakimwita Mkude na Mfungaji Bora wa muda wote Boko na Ngasa lazima turudi na kikombe kile.
 
Germany
Netherlands



[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Ujerumani siwapi nafasi sana same same to Uholanzi Ujerumani na Uholanzi wamepitia kwenye Vipindi vigumu sana miaka ya karibuni kwenye Soka

Labda kama Van gaal na Hans Flick watakuja na Udambwi mwingine.
 
Ujerumani siwapi nafasi sana same same to Uholanzi Ujerumani na Uholanzi wamepitia kwenye Vipindi vigumu sana miaka ya karibuni kwenye Soka

Labda kama Van gaal na Hans Flick watakuja na Udambwi mwingine.
Wajeruman wapambanaji, sio kizembe yan wale watu
Pia watu wanao, damu changa

Uholanzi ina kikosi kipana, talented
 
Wajeruman wapambanaji, sio kizembe yan wale watu
Pia watu wanao, damu changa

Uholanzi ina kikosi kipana, talented
Ukiangalia Kombe lililopita waliboronga sana China ya kocha Joachim Low labda Hans Flick anaweza kuja na kitu kipya manake anaamini katika soka la kushambulia.

Hawa kina Depay hawaminiki sana yaa wapo na talented wachezaji ila nikikumbuka kina Frank de Boer, Edga David, Seedorf, kluvet Patrick walishindwa kunyanyua kombe lolote na vipaji vyote nakata tamaa.
 
Kwa upande hawa jamaa siwapi nafasi sana wametoka kwenye misingi ya soka lao nao wanatembeza buti balaa ukutane na Casemiro pale kati aisee ni kiatu kiatu
 
Sijui kwanini nimejikuta naiamini Portugal watafanya vizuri kwenye hili kombe,ngoja nisimame nayo Kama vile moyo unavyotaka...pia naiona senegali wakifika mbali Kama watarekebisha udhaifu wao uleeee.
 
1. Argentina.
World cup ni mechi kadhaa tu ambazo ukiachilia kuwa na timu nzuri, basi kigezo cha muhimu kinachoamua ushindi ni morali ya timu. Recently, Argentina morali yao iko juu sana, wametoka kushinda Copa America na wanaamini wanaweza kushinda World Cup pia. Hawana majina makubwa makubwa, ila shughuli ngumu wanaiweza. Sitashangaa Leonel Messi akibeba world cup yake ya kwanza and probably ya mwisho!

2. Brazil.
Huwa siwaamini mabishoo. Ila hawa jamaa kipindi hiki ni tishio. Team yao imerudi japo sio kwa asilimia mia moja. Wako na kikosi kipana sana, na kuna vipaji vya uhakika kwenye kila eneo. Shida ni kwamba huwa hawawezi shughuli chafu. Ukikutana na majitu kama Ubelgiji, bila kucheza mpira mchafu yanaweza kukutoa roho. Otherwise, nawapa nafasi ya kufanya vizuri.

3. Ufaransa.
Bingwa mtetezi kama kawaida yake, amejaza majina makubwa makubwa mpaka anaogopesha. Ukitajiwa kikosi cha ufaransa, unajua kabisa unaingia uwanjani ukiwa umeshafungwa goli moja kabla ya mpira kuanza. Shida ni kwamba, kuna tofauti kati ya kua na timu, na kuwa na mwachezaji wenye majina makubwa. Kama kocha wao atafanya vizuri kwenye kuiunganisha timu, basi hawa jamaa wataondoka na ndoo!

WENGINE;
- Spain. Vile vitoto vilifika nusu fainali Euros, na vikafika fainali Olympic. Watu wazima wasipokaa sawa, vinaweza kuwashangaza.

- Portugal. Hawa jamaa pia wako na majina makubwa, ila team haina muunganiko. Wanategemea maajabu ya mchezaji mmoja mmoja. Pamoja na hayo, wako na watu wanaoweza kuamua matokeo muda wowote. Ikitokea wakafika hatua ya robo fainali, basi lolote laweza kutokea.


NB: Baada ya kuangalia AFCON, sidhani kama kuna team ya Africa itafanya maajabu. Mpira wetu bado uko na safari ndefu. Tunatishana tukicheza sisi kwa sisi, lakini kwa huko duniani sisi bado sana. Sioni wa kufurukuta mbele ya Denmark, achilia mbali big boys. Nadhani tukijitahidi sana, robo fainali ndio patakua mwisho wetu!
 
A
Argentina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…