WLF Tanzania
Member
- Oct 9, 2014
- 38
- 22
Serikali ya mkoa wa Kigoma na WLF wazindua Kampeni ya Redio na Uhamasishaji Jamii kuwahimiza akina mama wajawazito wajifungue katika Vituo Vya Huduma za Afya.
Serikali ya mkoa wa Kigoma na World Lung Foundation (WLF) leo wamezindua kampeni ya Thamini Uhai ambayo ni kampeni ya redio, mabango, simu za mkononi na uhamasishaji jamii ikilenga kuongeza huduma za kiafya kwa mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Kujifungua katika huduma salama za kiafya ni njia nzuri na ya uhakika kwa afya ya mama na mtoto. Hii ni kweli si tu kwa akina mama wenye matatizo ya ujauzito lakini kwa wanawake wote, kwa sababu matatizo ya dharura wakati wa ujauzito yaweza kutokea katika hatua yoyote wakati wa kujifungua.
Wanawake wachache -chini ya asilimia 50% - mkoani Kigoma hujifungua katika vituo vya huduma za afya na utumiaji huu mdogo wa huduma za afya ni sababu tosha inayopelekea idadi kubwa ya vifo vya mama wajawazito mkoani Kigoma. Uwiano wa vifo vya wajawazito nchini ni vifo 410 kwa 100,000.
Kampeni ya Thamini Uhai imebuniwa kuainisha sababu za kitamaduni na tabia ambazo zinapelekea matumizi madogo ya vituo vya huduma za afya wakati wa ujauzito. Hii inajumuisha fikra potofu kuhusiana na usalama wa kujifungua nyumbani, ukosefu wa mpango binafsi wa kujifungua, kujua umbali mrefu na suala la usafiri ambalo akina mama wengi wanakabiliana nalo katika kufikia vituo vya huduma za afya. Wakati mwingine, inajumuisha uwezo mdogo na uangalizi duni katika vituo vya afya. Kampeni imedhamiria kupunguza vifo vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi wakati wa kujifungua
Kampeni hii ilibuniwa ikilenga wanawake na wanaume wa mkoa wa Kigoma, kuhakikisha ujumbe wa kampeni unafanya kazi ipasavyo. Kampeni imelenga jumbe kuu tatu (3) katika matangazo matano ya redio: Ujumbe mmoja umelenga katika umuhimu wa kuwa na mpango wa kujifungua; ujumbe mwingine ni umuhimu wa kujifungua katika kituo cha huduma za afya na ujumbe wa tatu ni kutambua dalili za hatari wakati wa ujauzito.
Matokeo ya majaribio ya kampeni yameonyesha kwamba matangazo yanasababisha watu kuona hatari ya kutokutumia huduma za afya wakati wa kujifungua, na yanaibua mijadala kwa makundi ya walengwa na kuunda tabia chanya kwa wanaume kuwasaidia mama wajawazito. Kampeni ya Thamini Uhai pia itawasilishwa kwa njia ya uchoraji wa kuta, mabango , vipeperushi, simu za mkononi na uhamasishaji wa jamii kwa kushirikisha viongozi wa kijamii kama mabalozi.
WLF ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na CDC Foundation itajumuisha huduma ya ujumbe wa simu za mkononi katika kampeni hii. Huduma hii, inayotolewa kupitia mHealth Tanzania ni ubia wa serikali na sekta binafsi inawafikia akina mama wajawazito na waliojifungua kupitia ujumbe wa simu za mkononi. Inafikisha taarifa muhimu na kukumbusha muda wa kliniki kwa lugha ya Kiswahili, kwa bure, akina mama wajawazito na wenye watoto wachanga chini ya wiki 16, wasaidizi wao (wenza, ndugu na rafiki) pamoja na wadau wengine.
Ujumbe unaotumwa huandikwa kwa kutegemeana na taarifa iliyotolewa na mama mhusika ambaye anaainisha wakati wa usajili wiki au miezi ya mimba yake (au umri wa mtoto wake). Hii inawasaidia akina mama kupata ujumbe mahsusi na taarifa inayowahusu moja kwa moja. Matangazo ya "Thamini Uhai " yatarushwa kupitia TBC radio na Radio Kwizera na itawahamasisha akina wanawake kujisajili kwa huduma hii bure kwa kutuma neno ‘MTOTO' kwenda namba 15001.
Kampeni ya Thamini Uhai ni sehemu ya mpango wa WLF wa afya ya mama mjamzito, ambao unatafuta kuainisha changamoto maalum ikidhamiria juhudi za kupunguza vifo vya wajawazito nchini Tanzania. Changamoto hizi ni kubwa zaidi maeneo ya Kigoma vijijini, ambapo kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi (waganga wasaidizi, manesi wenye ujuzi), vitendea kazi vichache, na akina mama kuchelewa kufika katika vituo vilivyopo. Kigoma imekuwa ni shabaha kuu katika juhudi za mradi wa afya ya mama mjamzito wa WLF kwa miaka mitano sasa kupitia ufadhili wa kipekee kutoka Bloomberg Philanthropies.
WLF wamesaidia kuboresha na kujenga vituo vya afya 15 katika mikoa ya Kigoma, Morogoro na Pwani na imetoa mafunzo ya huduma mtambuka wa dharura ya uzazi na watoto wachanga (Comprehensive Emergency Obstetric and Newborn Care (CEmONC)) na nusu kaputi kwa wafanyakazi wa afya 106 ambao ni waganga wasaidizi, wakunga na maafisa afya nchini. Katika wilaya tano za Kigoma, WLF imesaidia kuboresha taasisi tisa (9) za afya , ikiwemo vituo sita (6) vya afya kwa kuwajengea uwezo wa kutoa huduma mtambuka wa dharura ya uzazi. Taasisi hizi ni pamoja na vituo vya afya vya Ujiji, Nguruka, Kakonko, Mabamba, Nyenge, Buhingu na hospitali tatu (3) ambazo ni: Maweni, Kibondo na Kasulu.
Kampeni imewezeshwa kwa ufadhili kutoka mfuko wa Swedish International Development Cooperation Agency (SIDA), ukilenga kusaidia mradi wa afya ya mama mjamzito Tanzania na wafadhili wengine wa mradi ni Bloomberg Philanthropies na H&B Agerup Foundation.
World Lung Foundation ilianzishwa kama sehemu ya kupambana na tatizo la kimataifa la maradhi ya mapafu inayoua watu milioni 10 kila mwaka. Shirika pia linafanya kazi katika miradi ya kupunguza vifo vya akina mama na watoto. WLF inaboresha afya kimataifa kwa kuboresha uwezo katika jamii husika, kwa kutoa msaada katika utafiti wa utendaji, kuendeleza sera husika na kwa kutoa elimu kwa umma. Maeneo yanayotiliwa mkazo na shirika ni kupunguza matumizi ya tumbaku, kuzuia vifo vya akina mama na watoto, kifua kikuu, Ukimwi/VVU, pumu na afya ya mapafu ya mtoto. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti worldlungfoundation.org
Kigoma Regional Commissioner, Lt Colonel(Retired) Hon. Issa Machibya shaking hands with WLF's Project Director(third left) after successfully launching The 'Thamini Uhai Campaign' in Kigoma.

World Lung Foundation's staffs and some of the Kigoma maternal health care providers marching towards Mwananchi grounds to mark inauguration of the Thamini Uhai Campaign in Kigoma.

The guess of Honour, Lt Colonel(Ritired) Issa Machibya(third left) clamping and other high table members clapping their hands after a successfull launch of the Thamini Uhai Campaign in Kigoma.