Ujisomee kwanza kwa undani zaidi kidogo, kaka. Huyu aliongoza jeshi la Waarabu katika Syria dhidi ya Wabizanti, lakini hakushinda Milki ya Bizanti. Bizanti (bila Syria) iliendelea kwa karne nyingi baada ya Khalid ibn Walid. Vilevile hakushinda Uajemi (Persia). Alianzisha mashambulio kadhaa dhidi ya vituo ya Uajemi katika Iraki. Lakini shambulio kubwa dhdi ya Uajemi lilitokea baada yake.
alitambuliwa kama kiongozi muhimu wa Waislamu katika miaka yao baada ya Muhamad. Mwishoni Khalifa Umar alimfukuza kwa mashtaki ya kugawa na kujigawia mwindo wa vita dhidi ya utaratibu.
Tendo la kukamata Yerusalemu halikuwa jambo kubwa kwa macho ya kijeshi.
Inaelekea umeisoma historia ya Waarabu, Waislamu nusu nusu.
Vita ni mchakato, Khalid Bin Walid alipigana na Majeshi ya dola ya Uajemi katika Vita kubwa tano na mara zote alishinda aliwachapa kwenye vita ya kwanza inayoitwa battle of the river, battle of Wallaja, Battle of Ullais, Battle of Hira.
Vita mojawapo ambayo Khalid bin Walid aliingia ndani kabisa ya dola ya Uajemi ni vita ya Battle of the Chains, katika jimbo la Hommuz ambayo ni Iran ya leo, Khalid bin Walida akiwa kamanda pia alishinda hiyo vita
Hizo siyo vita ndogo, ni vita zilizoinvolve makumi elfu ya Wanajeshi huku Waislamu wakiwa outnumbered katika ratio ya 2:1 sometimes.
Ushindi wa Khalid bin Walid ulipave njia ya Waislamu kuingia ndani ya Moyo wa dola ya Uajemi na kuitwaa once and for all
Baada ya Khallid bin Walid kuwachapa Waajemi Khalifa Abubakar alimtuma kwenda kuwachapa Wabyzantine (East Roman Empire) huko pia alitembeza kichapo, Utawala wa Omar ulipoingia madarakani baada ya Abubakar kufa kule kwenye battle front Syria Khalid bin Walid aliendelea kutembeza kichapo katika series ya battle nyingi tu dhidi ya East Roman Empire (Byzantine), Na battle iliyokuwa decisive ilikuwa ni battle ya Yarmouk, hii ilikuwa ni mwaka 636.
Omar alimtoa Khalid Bin Walid ukamanda siyo kwa sababu ya misconduct, bali alifanya hivyo kwa sababu reputation ya Khalid bin Walid ilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba akaanza kuhofu watu kujisahau kuwa Ushindi hutoka kwa Mungu na si binadamu. Hilo ndo lilimsukuma Omar kumbadilisha.
Kuhusu allegation za misconduct ya funds, Tukio lilikuwa ni baada ya mtu mmoja kuimba shairi kumsifu Khalid bin Walid na Khalid bin Wallid akamtunza yule muimbaji kwa fedha nyingi, Omar ambaye alikuwa ni Caliph hakupenda matumizi ya hizo fedha kwa sababu Omar alikuwa hapendi extravagancy, lakini hiyo siyo sababu ya Omar kumtoa kwenye Command ya majeshi ya waislamu.
Hata Khalid alipoondolewa kutoka kwenye Kucommand majeshi bado alikuwa mtoa msaada mkubwa wa Strategy za ushindi, kiasi kwamba kamanda mpya alikuwa akimwamini Khalid bin Wallid atake responsibility za uongozi katika mapambano katika ile kampeni ya Kuiangusha dola ya Urumi ya Mashariki (Byzantine)
Kuanguka kwa Jerusalem kijeshi ilikuwa ni kitu kikubwa sana kwa sababu strategy mojawapo ya Dola ya Byzantine ilikuwa ni kuilinda Jerusalem kwa udi na uvumba. Hata situation ilivyo leo hii huko Jerusalem, sababu mojawapo ya hali kuwa hivyo ni kutokana na waislamu kushinda hiyo vita ya mwaka 636. Mfano wa legacy ya huko, ni Waislamu kushikilia funguo za nyumba za Ibada za Wakiristo na Wayahaudi (Temple mount na makanisa ysliyomo huko), Baada ya Omar kwenda Jerusalem kukagua ushindi, Wazee, Makasisi wa Kikiristo wa huko walimpa funguo za makanisa yao kama ishara ya kumkabidhi funguo mtawala mpya, Na Omar akachagua familia moja huko Israel kuwa ni watunzaji wa hizo funguo, mpaka leo hii hiyo familia ndo watunzaji wa hiyo funguo
Kiufupi Kama hujui historia ya Khalid bin Wallid huwezi kumuelewa huyu mwamba, Huyu hajawahi poteza pambano hata moja naAlishiriki kikamilifu kuzipiga dola mbili ya Rumi Mashariki na Uajemi.
Dola ya Byzantine iliendelea kubaki maeneo kama Uturuki, cyprus na Ugiriki tu ikiwa haina makali ya awali, lakini baadae ilikuwa kuangushwa na Ottoman Empire katika Karne ya 15, pale majeshi ya Waislamu ya Ottoman yalipouiteka Constantinople (Istanbul) na kuligeuza lile ksnisa maarufu Hagia Sofia kuwa msikiti.
Kaka Khalid bin Wallid achana nae, yule ni jenerali hana mfano
Hebu cheki kidogo hapa kuhusu stratergy ya vita ya Yarmouk uuone ugenius wa Khalid bin Walid, These videos are a must watch kwa mtu yeyote anayetaka kujua sanaa ya mapigano
PART 1
PART 2