Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ujisomee kwanza kwa undani zaidi kidogo, kaka. Huyu aliongoza jeshi la Waarabu katika Syria dhidi ya Wabizanti, lakini hakushinda Milki ya Bizanti. Bizanti (bila Syria) iliendelea kwa karne nyingi baada ya Khalid ibn Walid. Vilevile hakushinda Uajemi (Persia). Alianzisha mashambulio kadhaa dhidi ya vituo ya Uajemi katika Iraki. Lakini shambulio kubwa dhdi ya Uajemi lilitokea baada yake.Hakuna Jenerali katika Historia anayemfikia Khalid bin Walid.
Ukisikia Conquests zote walizofanya Waislamu hadi kuikamata Jerusalem kutoka kwa Byzantine empire na kisha kuitawala kwa karne nyingi, Khalid bin walid alikuwa kamanda
alipigana vita zaidi ya 100 hajawahi kupoteza pambano
Ujisomee kwanza kwa undani zaidi kidogo, kaka. Huyu aliongoza jeshi la Waarabu katika Syria dhidi ya Wabizanti, lakini hakushinda Milki ya Bizanti. Bizanti (bila Syria) iliendelea kwa karne nyingi baada ya Khalid ibn Walid. Vilevile hakushinda Uajemi (Persia). Alianzisha mashambulio kadhaa dhidi ya vituo ya Uajemi katika Iraki. Lakini shambulio kubwa dhdi ya Uajemi lilitokea baada yake.
alitambuliwa kama kiongozi muhimu wa Waislamu katika miaka yao baada ya Muhamad. Mwishoni Khalifa Umar alimfukuza kwa mashtaki ya kugawa na kujigawia mwindo wa vita dhidi ya utaratibu.
Tendo la kukamata Yerusalemu halikuwa jambo kubwa kwa macho ya kijeshi.
Sipinga alifaulu katika kampeni. Lakini ulimpigia debe bila kiasi.Inaelekea umeisoma historia ya Waarabu, Waislamu nusu nusu.
Vita ni mchakato, Khalid Bin Walid alipigana na Majeshi ya dola ya Uajemi katika Vita kubwa tano na mara zote alishinda aliwachapa kwenye vita ya kwanza inayoitwa battle of the river, battle of Wallaja, Battle of Ullais, Battle of Hira.
Vita mojawapo ambayo Khalid bin Walid aliingia ndani kabisa ya dola ya Uajemi ni vita ya Battle of the Chains, katika jimbo la Hommuz ambayo ni Iran ya leo, Khalid bin Walida akiwa kamanda pia alishinda hiyo vita
Hizo siyo vita ndogo, ni vita zilizoinvolve makumi elfu ya Wanajeshi huku Waislamu wakiwa outnumbered katika ratio ya 2:1 sometimes.
Ushindi wa Khalid bin Walid ulipave njia ya Waislamu kuingia ndani ya Moyo wa dola ya Uajemi na kuitwaa once and for all
Baada ya Khallid bin Walid kuwachapa Waajemi Khalifa Abubakar alimtuma kwenda kuwachapa Wabyzantine (East Roman Empire) huko pia alitembeza kichapo, Utawala wa Omar ulipoingia madarakani baada ya Abubakar kufa kule kwenye battle front Syria Khalid bin Walid aliendelea kutembeza kichapo katika series ya battle nyingi tu dhidi ya East Roman Empire (Byzantine), Na battle iliyokuwa decisive ilikuwa ni battle ya Yarmouk, hii ilikuwa ni mwaka 636.
Omar alimtoa Khalid Bin Walid ukamanda siyo kwa sababu ya misconduct, bali alifanya hivyo kwa sababu reputation ya Khalid bin Walid ilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba akaanza kuhofu watu kujisahau kuwa Ushindi hutoka kwa Mungu na si binadamu. Hilo ndo lilimsukuma Omar kumbadilisha.
Kuhusu allegation za misconduct ya funds, Tukio lilikuwa ni bwada ya mtu mmoja kuimba shairi kumsifu Khalid bin Walid na Khalid bin Wallid akamtunza yule muimbaji kwa fedha nyingi, Omar ambaye alikuwa ni Caliph hakupenda matumizi ya hizo fedha kwa sababu Omar alikuwa hapendi extravagancy, lakini hiyo siyo sababu ya Omar kumtoa kwenye Command ya majeshi ya waislamu.
Hata Khalid alipoondolewa kutoka kwenye Kucommand majeshi bado alikuwa mtoa msaada mkubwa wa Strategy za ushindi, kiasi kwamba kamanda mpya alikuwa akimwamini Khalid bin Wallid atake responsibility za uongozi katika mapambano katika ile kampeni ya Kuiangusha dola ya Urumi ya Mashariki (Byzantine)
Kuanguka kwa Jerusalem kijeshi ilikuwa ni kitu kikubwa sana kwa sababu strategy mojawapo ya Dola ya Byzantine ilikuwa ni kuilinda Jerusalem kwa udi na uvumba. Hata situation ilivyo leo hii huko Jerusalem, sababu mojawapo ya hali kuwa hivyo ni kutokana na waislamu kushinda hiyo vita ya mwaka 636. Mfano wa legacy ya huko, ni Waislamu kushikilia funguo za nyumba za Ibada za Wakiristo na Wayahaudi (Temple mount na makanisa ysliyomo huko), Baada ya Omar kwenda Jerusalem kukagua ushindi, Wazee, Makasisi wa Kikiristo wa huko walimpa funguo za makanisa yao kama ishara ya kumkabidhi funguo mtawala mpya, Na Omar akachagua familia moja huko Israel kuwa ni watunzaji wa hizo funguo, mpaka leo hii hiyo familia ndo watunzaji wa hiyo funguo
Kiufupi Kama hujui historia ya Khalid bin Wallid huwezi kumuelewa huyu mwamba, Huyu hajawahi poteza pambano hata moja naAlishiriki kikamilifu kuzipiga dola mbili ya Rumi Mashariki na Uajemi.
Dola ya Byzantine iliendelea kubaki maeneo kama Uturuki, cyprus na Ugiriki tu ikiwa haina makali ya awali, lakini baadae ilikuwa kuangushwa na Ottoman Empire katika Karne ya 15, pale majeshi ya Waislamu ya Ottoman yalipouiteka Constantinople (Istanbul) na kuligeuza lile ksnisa maarufu Hagia Sofia kuwa msikiti.
Sipinga alifaulu katika kampeni. Lakini ulimpigia debe bila kiasi.
1. hakushinda Bizanti, alikamata Syria. Bizanti iliendelea kwa miaka 700. Hii siiti "kushinda Bizanti". Waliweza kuimarisha hali yao kiasi hakuna Mwarabu aliyeweza kuwashinda tena.
2. Kuhusu Uajemi: alifanya kempeni moja pale Iraki, akipita tu kusini ya mto Frati katika Iraki. Hakuvuka mto, hakukaribia miji muhimu ya Waajemi. Alipita katika maeneo ya Walakhmiya (Lakhmids / Lakhmiyun) na kuwashinda. Hakukupigana na jeshi la Waajemi wenyewe.
Katika Yerusalemu Khalid hakufaulu kitu. Jeshi la Waarabu lilishindwa kuteka mji, shauri la ukuta mkubwa. Wakati ule walikosa bado elimu na uwezo kushinda ngome iliyo imara. Walizuia tu vyakula kuingia ndani. Baada ya mapigano ya Yarmouk mji ulikuwa bila njia ya kupata msaada kutoka nje. Askofu wa Yerusalemu alisimamia utetezi wa mji hatimaye alikubali kusalimisha amri kwa mashariti khalifa aje mwenyewe ili amaliza mapatano naye. Khalid hakuongoza jeshi la kiarabu pale Yerusalemu. Waarabu hawakutaka kumsubiri khalifa, walijaribu udanganyifu walituma halid ibn Walid afika kama khalifa lakini watetezi walimtambua walisema watasalimu amri pekee mbele ya jkkhalifa mwenyewe. Basi khalifa Umar alipofika walimkabidhi mji kwa masharti, yaliyokubaliwa na Waarabu. Si Khalid aliyeshinda Yerusalemu.
Swali kama alikuwa jenerali kushinda wote - basi uzuri wa binti uko machoni mwa mtazamaji. Hawezi kunivuta.
Kumbe umeshaanza kushuka chini kutoka mnara ulipopanda awali. Kuhusu Khalid kuwashinda Wabizanti katika Syria, hakuna neno.Hizi taarifa potofu unazipata wapi wewe?
Nimekwambia Jeshi aliloliongoza Walid lilipigana na Waajemi katika Battle Tano na alishinda Zote, kabla yake hakujawahi kuwepo Mwarabu hata mmoja sliyewahi kushinda vita yoyote na Mwajemi. Tena hizi battle siyo battle ndogo, ni battle kubwa kabisa kabisa zenye kuinvolve maelfu ya wapiganaji.
Nimekueleza Khalid Bin Wallid aliongoza Vita kati ya Waislamu na Waajemi ndani ya Mji wa Hommuz, ndani kabisa ya moyo wa Uajemi, na akamchallenge Governor wa huo mji katika battle ya Man to Man (Duel), Khalid akamchapa na Pia jeshi alilokuwa analiongoza Likawachapa Hao waajemi.
Kuhusu Jerusalem, Vita ni mbinu, Kukata Supply ya vyakula ni mbinu mojawapo, Hata akina Genghiskhan baadae walikuwa wakitumia mbinu hiyo. Siyo kukata supply ya vyakula tu bali walikuwa pia wakichoma vijiji na hifadhi za Chakula vya adui.
Militarily Jerusalem ilishaanguka, Haikuwa na power yoyote ya Kustand off tena. Tayari majeshi ya Wallid yalishawachapa Wabyzantine wenye kutawala mji wa Jerusalem wakati huo na mji ulikuwa defenseless kijeshi, it was the matter of time kabla haujaanguka.
Wao kumtaka Khalifa aende ndo watoe funguo kwa mtawala mpya ilikuwa ni political, au kiucha Mungu rather than military action, maana Militarily walikuwa wameshachapwa, wameshakuwa out manuevred. Hata kwa mfano Khalid angemgomea Askofu wa Jerusalem kuwa si lazima Khalifa aje, Tayari Wallid angeweza kuutwaa ule mji, Lakini kutoka na heshima kwa Khalifa, na kutokana na heshima ambayo waislamu walikuwa nayo juu ya viongozi wa dini ya watu wa Kitabu (Wakiristo), Khalid na wenzie wakaona wakubali propsal ya Askofu. La sivyo isingependeza Waislamu wautie njaa mji. mzima watu wote wafe, hilo hata kidini wangetenda dhambi, maana maagizo ya mtume katika vita yako wazi, mosi usidhuru wanawake, pili usidhuru watoto, usiharibu nyumba za ibada etc.
Sasa nakushangaa hitambui kuanguka kwa Jerusalem kama feat ya kijeshi, hii ni ajabu sana. Jerusalem ilikuwa ni mji chini ya ufalme wa Byzantine chini ya mfalme Heraclius, Ni baada ya Majeshi ya Byzantine kupigwa na Waislamu kutoka katika Syria, Palestine ndipo Jerusalem ilipoanguka, Ni ajabu unavyodhani Jerusalem iligawa funguo kwa Khalifa kwa kupenda bila kuwa militarily defeated!. Vita siyo bunduki na mapanga peke yake, Vita ni pamoja na kumfanya adui Assurende hata kwa kumminya asipate msosi.
Kuhusu Byzantibe kuendelea kuwepo kwa miaka 700 (Kama muendelezo wa Roman Empire), Hii siyo hoja, Hoja ni kwamba Roman Empire ilipigwa na kufurumushwa na Waislamu huko Levant (Syria, Palestine na baadhi ya sehemu za Iraki). East Roman Empire kupoteza mji mtakatifu wa Jerusalem na nchi takatifu ni pigo kubwa mno kwao na hawakuacha kufikiria namna gani watairudisha hiyo himaya yao yenye mji mtakatifu, ni mpaka miaka 500 baadae kupitia Crusades Jerusalem iliwatoka waislamu lakini baadae ikarudishwa mikononi mwao karne chache baadae kupitia kwa Jenerali Salahu-din (Wazungu wanamuita Saladin).
Kuhusu Lakhmids, pengine hujui kuwa Uajemi wakati huo ilikuwa ni dola kubwa inayochukua sehemu za Iraki, Iran, Tajikstan n. k.
Nimekueleza Khallid ameshafanya Battle ndani ya Hommuz, Moja ya Jimbo mubimu sana ndani ya Uajemi na Kutembeza kichapo cha nguvu!.
Khalid ni commander bora kabisa kuwahi kutokea!
Kumbe umeshaanza kushuka chini kutoka mnara ulipopanda awali. Kuhusu Khalid kuwashinda Wabizanti katika Syria, hakuna neno.
Mimi nilijibu madai yako pale juu ulipoandika
" Empires mbil kubwa za Wakati wake Byzantine na Persia zilianguka huku yeye akiwa ni Commander wa majeshi yaliyoziangusha! "
Milki hizo hazikuangushwa na Khalid. Bizanti haikuangushwa kabisa na Waarabu, ili kupungukiwa. Na Uajemi ilianguka baada ya Khalid.
Kuhusu Yerusalemu: naona umeshakumbuka kuwa Khalid hakuongoza Waarabu pale Yerusalemu. Alikuwa mmojawapo wa viongozi chini ya Abu Ubaidah . Hakuwa na kazi nyingi maana hapakuwa na mapigano.
Kuhusu madai yako "Khalid Bin Wallid aliongoza Vita kati ya Waislamu na Waajemi ndani ya Mji wa Hommuz, ndani kabisa ya moyo wa Uajemi,"
Je kweli hujui kusoma ramani? "Moyo wa Uajemi"???? Moyo hii ilikuwa bado mbali. Hiyo safari ya Khalid katika Iraki ilikuwa kabisa upande wa kusini wa Mto Frati; yaani alipita mpaka wa kusini wa Milki ya Uajemi na hapa alishinda vikosi vya Waarabu walioshikamana na Uajemi na pia vikosi vya Waajemi vilivyokuwepo pale.
Hujaeleza kitu, maana umechanganya "mji wa Hommuz" (hakuna mji wa Hommuz) na jina la kiongozi mmoja Hormuz upande wa Waajemi. Nahisi unamaanisha "mapigano ya nyororo" ( معركة ذات السلاسل ) ambako Hormuz aliwaongoza Waajemi.
Kaka ninakupongeza maana umejitahid kujisomea, tofauti na wengi wanaochangia hapa. Madharinyuma yako katika historia kwa jumla bado ina mapengo mengi ("moyo wa Uajemi"!!) lakini usikate tamaa, endelea kujielimisha!
Na ukimpenda Khalid vile - nilivyosema juu, uzuri unapatikana machoni mwa mtazamaji.
Khalid Bin Walid (The Sword of Islam), alikuwa ni mwanajeshi mwenye akili ya kipeke yake sana. Historia huwa haiwazungumzii vizuri hawa wanajeshi wa kiarabu. Nadhani pia unapunguza makali ya hii hoja yako unaposema neno BYZANTINE EMPIRE kwasababu lile lilikuwa ni DOLA LA MRUMI (THE EASTERN ROMAN EMPIRE). Tena hatari zaidi ni kwamba Kaisari wa kipindi hicho alikuwa ni Heraclius ( A Military Genius), ambaye alikuwa na uzoefu mkubwa wa vita baada ya kupambana muda mrefu na waajemi (SASSANIAN EMPIRE).Hakuna Jenerali katika Historia anayemfikia Khalid bin Walid.
Ukisikia Conquests zote walizofanya Waislamu hadi kuikamata Jerusalem kutoka kwa Byzantine empire na kisha kuitawala kwa karne nyingi, Khalid bin walid alikuwa kamanda
alipigana vita zaidi ya 100 hajawahi kupoteza pambano
Mkuu, hoja yako haipingwi: Khalid Ibin Walid alikuwa ni mwanajeshi mwenye uwezo wa kipekee. Japo nadhani kule Uajemi alipambana vita moja kubwa kwenye mji wa Kazima (The Battle of Chains) ambako leo hii ni Kuwait. Mchezo aliokuwa anautumia ni ule ule (Razzia Tactics) , anakuzungukia kwa nyuma anakuchosha halafu anatokea mbele yako. Japo, nadhani katika majenerali wa jeshi la waarabu (The Rashidun Caliphate) ambaye anahitaji kupewa sifa zake kwa kuiangusha Uajemi ni Saad Ibin Waqqas maana yeye ndiyo alipambana na Rostam kule Qadisiyyah (The Battle of Qadisiyyah) hadi kufika mji mkuu wa Ctesiphon na kumkimbiza mfalme Yezdegerd III.2. Abu Ubayda Japo alikuwa ni mkuu wa Vikosi baada ya Khalid kuwa demoted na Calif Omar kwa sababu Khalif hakutaka watu wanuabudu Khalid kutokana na umaarufu wake wa kushinda vita, Lakini techinically operation nzima ya Syria hadi kuanguka kwa Jerusalem ilikuwa inaendeshwa kwa Stratergy za Khalid bin Walid, Hata kwenye mapambano hayo, mara kadhaa Abu Ubayda alimpa majukumu Khalid kuongoza vita katika kampeni hizo
Huyo alikuwa na vifaru bora kuliko vifaru vyote ktk ile vitaMbona hamumtaji jenerali Erwin Rommel wa Ujerumani shujaa wa kweli wa World war two
Licha ya kutumia silaha duni za kiitaliano ila mataifa kama manne (USA,UK,FRANCE And CO ) walikuwa hawauwezi mziki wa Rommel
Companero...1. Saladin
2. Shaka
3. Napoleon Bonaparte
4. Attila the Hun
5. Genseric the Vandal
6. Alexander the Great
7. Charlemagne
8. John Okello
9. Chris Hani
10. Hannibal
11....
AS Abri,Mbona hamumtaji jenerali Erwin Rommel wa Ujerumani shujaa wa kweli wa World war two
Licha ya kutumia silaha duni za kiitaliano ila mataifa kama manne (USA,UK,FRANCE And CO ) walikuwa hawauwezi mziki wa Rommel
Byzantine haikuwa Syria tu. Hivyo kama alishinda vikosi vya Syria haina maana kuwa aliwashinda warumi. Hakuna mtu mwenye ubavu wa kuwashinda warumiInaelekea umeisoma historia ya Waarabu, Waislamu nusu nusu.
Vita ni mchakato, Khalid Bin Walid alipigana na Majeshi ya dola ya Uajemi katika Vita kubwa tano na mara zote alishinda aliwachapa kwenye vita ya kwanza inayoitwa battle of the river, battle of Wallaja, Battle of Ullais, Battle of Hira.
Vita mojawapo ambayo Khalid bin Walid aliingia ndani kabisa ya dola ya Uajemi ni vita ya Battle of the Chains, katika jimbo la Hommuz ambayo ni Iran ya leo, Khalid bin Walida akiwa kamanda pia alishinda hiyo vita
Hizo siyo vita ndogo, ni vita zilizoinvolve makumi elfu ya Wanajeshi huku Waislamu wakiwa outnumbered katika ratio ya 2:1 sometimes.
Ushindi wa Khalid bin Walid ulipave njia ya Waislamu kuingia ndani ya Moyo wa dola ya Uajemi na kuitwaa once and for all
Baada ya Khallid bin Walid kuwachapa Waajemi Khalifa Abubakar alimtuma kwenda kuwachapa Wabyzantine (East Roman Empire) huko pia alitembeza kichapo, Utawala wa Omar ulipoingia madarakani baada ya Abubakar kufa kule kwenye battle front Syria Khalid bin Walid aliendelea kutembeza kichapo katika series ya battle nyingi tu dhidi ya East Roman Empire (Byzantine), Na battle iliyokuwa decisive ilikuwa ni battle ya Yarmouk, hii ilikuwa ni mwaka 636.
Omar alimtoa Khalid Bin Walid ukamanda siyo kwa sababu ya misconduct, bali alifanya hivyo kwa sababu reputation ya Khalid bin Walid ilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba akaanza kuhofu watu kujisahau kuwa Ushindi hutoka kwa Mungu na si binadamu. Hilo ndo lilimsukuma Omar kumbadilisha.
Kuhusu allegation za misconduct ya funds, Tukio lilikuwa ni baada ya mtu mmoja kuimba shairi kumsifu Khalid bin Walid na Khalid bin Wallid akamtunza yule muimbaji kwa fedha nyingi, Omar ambaye alikuwa ni Caliph hakupenda matumizi ya hizo fedha kwa sababu Omar alikuwa hapendi extravagancy, lakini hiyo siyo sababu ya Omar kumtoa kwenye Command ya majeshi ya waislamu.
Hata Khalid alipoondolewa kutoka kwenye Kucommand majeshi bado alikuwa mtoa msaada mkubwa wa Strategy za ushindi, kiasi kwamba kamanda mpya alikuwa akimwamini Khalid bin Wallid atake responsibility za uongozi katika mapambano katika ile kampeni ya Kuiangusha dola ya Urumi ya Mashariki (Byzantine)
Kuanguka kwa Jerusalem kijeshi ilikuwa ni kitu kikubwa sana kwa sababu strategy mojawapo ya Dola ya Byzantine ilikuwa ni kuilinda Jerusalem kwa udi na uvumba. Hata situation ilivyo leo hii huko Jerusalem, sababu mojawapo ya hali kuwa hivyo ni kutokana na waislamu kushinda hiyo vita ya mwaka 636. Mfano wa legacy ya huko, ni Waislamu kushikilia funguo za nyumba za Ibada za Wakiristo na Wayahaudi (Temple mount na makanisa ysliyomo huko), Baada ya Omar kwenda Jerusalem kukagua ushindi, Wazee, Makasisi wa Kikiristo wa huko walimpa funguo za makanisa yao kama ishara ya kumkabidhi funguo mtawala mpya, Na Omar akachagua familia moja huko Israel kuwa ni watunzaji wa hizo funguo, mpaka leo hii hiyo familia ndo watunzaji wa hiyo funguo
Kiufupi Kama hujui historia ya Khalid bin Wallid huwezi kumuelewa huyu mwamba, Huyu hajawahi poteza pambano hata moja naAlishiriki kikamilifu kuzipiga dola mbili ya Rumi Mashariki na Uajemi.
Dola ya Byzantine iliendelea kubaki maeneo kama Uturuki, cyprus na Ugiriki tu ikiwa haina makali ya awali, lakini baadae ilikuwa kuangushwa na Ottoman Empire katika Karne ya 15, pale majeshi ya Waislamu ya Ottoman yalipouiteka Constantinople (Istanbul) na kuligeuza lile ksnisa maarufu Hagia Sofia kuwa msikiti.
Kaka Khalid bin Wallid achana nae, yule ni jenerali hana mfano
Hebu cheki kidogo hapa kuhusu stratergy ya vita ya Yarmouk uuone ugenius wa Khalid bin Walid, These videos are a must watch kwa mtu yeyote anayetaka kujua sanaa ya mapigano
PART 1
PART 2
Well tufanye basi Byzantine ilishinda vita zote, na haikupigwa, na Jerusalem haikuangukaByzantine haikuwa Syria tu. Hivyo kama alishinda vikosi vya Syria haina maana kuwa aliwashinda warumi. Hakuna mtu mwenye ubavu wa kuwashinda warumi
Wako wengi kama watatajwa hapaAS Abri,
Ahsante kwa kumleta Erwin Rommel ''The Desert Fox.''
Nilikuwa naitazama hiyo orodha halafu nikawa nimeshughulishwa na John Okella na nikawa nacheka peke yangu.
Nikaikagua tena orodha sikumuona Rommel wala Umar Mukhatar wala Khalid bin Walid.
Tatizo kubwa nilionalo siku hizi ni kuwa watu hawasomi vitabu na matokeo yake ndiyo haya.
Mambo mengi ni ya kubabiababia.
Duh, yaani kwenye list yako umemuweka John Okello? Kwenye list yako hayupo Khalid ibn Walid, 'Amr ibn al-'As, S'ad ibn Abi Waqqas, Tariq ibn Ziyad, Genghis Khan, Muhammad al-Fatih, Aurangzeb, George Washington, Erwin Rommel, George Patton na Douglas McArthur!!1. Saladin
2. Shaka
3. Napoleon Bonaparte
4. Attila the Hun
5. Genseric the Vandal
6. Alexander the Great
7. Charlemagne
8. John Okello
9. Chris Hani
10. Hannibal
11....