Byzantine haikuwa Syria tu. Hivyo kama alishinda vikosi vya Syria haina maana kuwa aliwashinda warumi. Hakuna mtu mwenye ubavu wa kuwashinda warumi
Mkuu, dola la Rumi katika miaka yake zaidi ya 2000 halijawahi kufanikiwa kuwapiga waajemi hata siku moja. Baada ya dola la Karthago (Carthage) nadhani madola ya Uajemi (The Parthian Empire and The Sassanian Empire) ndiyo yalikuwa maadui wakubwa wa Roma ambao Roma alishindwa kuwashinda. Hizi nyingine za kusema Roma hawezi kushindwa nadhani ni propaganda za kidini ambazo inabidi zitazamwe upya. Haya hebu zingatia vita zifuatazo:
The Battle of Carrhae: Hii vita ilipiganwa mwaka 53 BC, kule eneo la Carrhae ambako ni Uturuki ya leo, ambapo mwanajeshi wa Roma mwenye uwezo wa kipekee kabisa na aliyewahi kushinda vita (
Imperator)
Marcus Lucianus Crassus. Huyu alivamia dola la kiajemi la Parthia na wanajeshi 4,3000. Hawa wanajeshi walikuwa ni wazoefu wa vita (Battle Hardened) maana kabla ya hii vita walikuwa wametoka kupigana na jeshi la watumwa lilikuwa chini ya Spartacus na Crixus (The Third Servile Wars) na kushinda. Walikuwa na jeshi la wavaa vyuma vizito (Legionaries/Heavy Infantry) wasiopungua 35,000, huku adui wao kiongozi wa jeshi la Parthia,
Rustem Surena alikuwa na wanajeshi 10,000.
Hao wanajeshi 10,000 waligawanywa katika makundi mawili ambayo ni wapanda farasi wenye mishale 9,000 (Mounted Archers) na Jeshi la wapanda farasi wenye vyuma 1,000 (Heavy Cavalry/Cataphracts). Jeshi la Roma lilizidiwa na maelfu ya Warumi waliuwawa huku watu zaidi ya 10,000 wakichukuliwa mateka. Silaha kubwa ya waajemi ilikuwa ni mishale (The Scythian Composite Bow) ambao uliletwa na mfalme Koreshi miaka mingi nyuma. Wanahistoria wanasema waajemi waliwazunguka Waroma huku wakiwa wananyesha mvua ya mishale kwa masaa mengi bila kusimama. Fuatilia utaona......
The Battle of Nisibis: Hii vita ilipiganwa mwaka 217 AD, kule Nisibis ambako nako ni Uturuki ya leo. Hii vita ilianza kwa ugomvi mkubwa ambapo Kaisari wa Roma Caracalla alivunja mkata alioingia na mfalme wa Uajemi (Parthian Empire), Artabanus IV kwa kuvamia Uajemi na kuua raia wasio na hatia. Waajemi walipanamba na Waroma kwa siku tatu mfululizo, ambako maelfu yao walikufa. Kaisari wa Roma baada ya kuona atauwawa ikabidi akubali kushindwa na kumlipa mfalme wa Uajemi fidia kubwa mno ya pesa pamoja na kurudisha mateka wa kijeshi.
Halafu ukumbuke kipindi hiki dola la Kiparsi ndiyo lilikuwa linaelekea kuanguka , maana walikuwa wanapigana vita vya wao kwa wao (Civil War) kugombania madaraka. Wafalme wa Roma waliona hii ndiyo nafasi kuvamia Uajemi, lakini waliangukia pua vibaya mno.
The Battle of Edessa: Hii vita ilipiganwa mwaka 260 A.D kule Edessa, ambako ni Uturuki ya leo. Nadhani hii ni moja ya vita mbaya zaidi kuwahi kuikuta Roma ukizitoa vita kama zile za Vita ya Cannae (The Battle of Cannae) na vita ya ziwa Trasime (The Battle of Lake Trasimene) ambazo majeshi ya Roma yalichinjwa vibaya sana na vikosi vya mwanajeshi wa Karthago, Hannibal Barca. Hii vita ya Edessa ilikuwa ni mbaya sana hadi kupelekea Kaisari wa Roma
Publius Lucianus Valerianus pamoja na wanajeshi 70,000 walitandikwa vibaya na kuchukuliwa mateka na mfalme
Shapur I wa dola la Kiajemi la Sassani (The Sassanian Empire). Kaisari wa Roma alifia Uajemi na nchi ikaingia kwenye taharuki kubwa mno. Hichi ni kitu ambacho wengi hatufundishwi kwenye vitabu vilivyojaa propaganda za kidini na kizungu. Fuatilia utaona.......
Wababe wengi wa Roma kama Mfalme
Trajan ,walipambana na Uajemi hadi kufika mji mkuu Ctesiphon na kuupiga lakini hawakufanikiwa kuwashinda waajemi. Sasa hebu fikiria, mtu kama Trajan alishindwa kuwatawala waajemi unadhani walikuwa ni watu wa aina gani hawa. Mfalme
Heraclius naye alijaribu na kushindwa vibaya mno hadi kufanya makubaliano ya amani.
NB: Dola la Mrumi kuanzia mji wa
Rome hadi
Constantinople walikuwa wanapigika sana. Wafalme kama
Attila The Hun,
Theodoric The Great,
Khosrow na majeshi yao walifanikiwa kufika sehemu za ndani kabisa za Roma huku
Sultani Mehmed II (The Conqueror) akifanikiwa kuwaangusha kabisa Waroma na kuutwaa mji mkuu wa Constantinople huku akijipa jina la Kaisari.
NO BODY IS INVINCIBLE............