Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya leo.
View attachment 2629490View attachment 2629492
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huwa na swali, likifuatiwa na hoja, kisha jibu utalitoa wewe mwenyewe.
Swali la mada hii ni Je
Wosia mzito wa William Malecela (Le Mutuz) kwa CCM, Wapinzani, Serikali na kwa JamiiForums uzingatiwe na kutekelezwa ili tuendelee kumuishi, au baada ya kufa,anakuwa ndio mwisho wake na kila kitu chake?.
Wiki iliyopita kwenye safu hii niliandika Buriani ya Benard Membe, na Wiki hii ni Buriani nyingine, hii ni buriani ya mtu wa kawaida tuu ambaye sio kiongozi wa CCM, wala sio kiongozi wa serikali, ni mtu tuu wa kawaida aliyefahamika na wengi, hivyo maneno ya mtu wa wengi ni maneno ya wengi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hii ni makala ya kuitaka CCM, serikali, wapinzani kuzingatia sana wosia wa mtu huyu!.
Huyu ni William Malecela, ambaye anajulikana sana kwa jina maarufu la Le Mutuz, kutokana na kuendesha ukurasa wake wa Le Mutuz Super Brand kwenye mitandao ya kijamii, hivyo kuna wengi wanaomfahamu zaidi William kutokana na umaarufu wake wa kwenye mitandao ya kijamii kama Le Mutuz, hivyo sifa zake kama William Malecela, kujikuta zimeishia Jamiiforums pekee. William Malecela alifariki ghafla wiki iyopita na kuzikwa kijijini kwao Mvumi Dodoma siku ya Jumatano iliyopita.
Wosia.
Wosia ni maneno ya mwisho ya marehemu anayoyaacha kuzungumzia jambo fulani, wosia huo unaweza kuwa wa maneno ya kuambiwa au kuandikwa. Wosia huu wa William Malecela kwa CCM serikali, ni wosia wa maneno ya kuzungumza, ambapo aliyasema bila kupanga, ni tulikutana tuu viwanja vya Saba Saba, nikamfanyia mahojiano impromptu, na kwavile sasa tuko kwenye dunia ya kimtandao, wosia huu nimeurekodi kwenye video na kuutupia kwenye mtandao wa YouTube, baada ya kupokea taarifa ya kifo chake, nilipoyasikiliza tena "Mahojioano William Malecela na Pasco Mayalla" ndio sasa nimegundua kumbe huu ni wosia anaihusia serikali, CCM, na wapinzani.
Poleni Sana Wafiwa Wakiongozwa na The Malecelas.
Kunapotokea msiba wowote, wafiwa wakuu wa kwanza ni familia yake, hivyo kwanza nitoe pole zangu kwa familia yake, mkewe na watoto wake, pole kwa familia ya Mzee John Samwel Malecela, pole kwa familia yake ya JF, pole kwa wanamitandao kumpoteza mwanamtandao mwenzao, pole kwa CCM kumpoteza mwanachama wake ambaye ni mmoja wa wana CCM Wazalendo na wakweli kabisa toka ndani ya nafsi zao, na pole kwa Watanzania wote kumpoteza Mtanzania mwenzetu, haijalishi alikuwa nani, thamani ya mtu ni utu, hivyo binadamu yoyote akitangulia pole ni stahiki.
Mimi ni mtu wa mastori mastori, hivyo sasa nakuja kwenye mastori story ya Pasco, kama wewe sio mtu wa mastori story, jump to conclusions.
Mastori ya Pasco, Mimi na Malecelas
William Malecela, A Man With A Heart of Gold
Kuna watu wengi ni watu wenye roho mbaya, akiona kuna mchongo fulani, hakupi connection, William alikuwa ni mtu mwenye roho nzuri. Ni William Malecela, Le Mutuz ndie aliyenitambulisha mimi kwenye mtandao wa YouTube channel, na video yangu ya kwanza kwenye YouTube ni video ya mahojioano na William Malecela ambayo video hii ndio usia ambao William Malecela ametuachia milele, nataka wana CCM wote haswa viongozi, watu wa serikali na sisi wana jf, tusikilize kwa makini wosia huu na ikiwezeka tuuishi.
William Malecela Kada Mtiifu na Mkweli Daima wa CCM, at Heat!, He Was Born and Breed CCM!, Amekufa CCM!
Chama cha Mapinduzi CCM, kina taratibu zake za ukosoaji kufanywa na wanachama wake, kinataka ukosoaji wowote wa CCM, ukifanywa na mwana CCM, ukosoaji huo ufanyike kwenye vikao vya ndani. William alikuwa hakopeshi!.
William Malecela Aliipenda CCM na Kuitetea CCM, Lakini Hakuwa Chawa!
Siku hizi kupitia mitandao ya kijamii, kumeibuka vikundi vya kusifia wakiijiita machawa. William Malecela ni mwana CCM, aliyeipenda CCM kwa dhati ya moyo wake na kiitetea CCM kwa nguvu zake zote ila hakuwa chawa kwasababu pia aliikosoa CCM, wazi wazi na sio kupitia vikao vya ndani.
Ni katika mahojiano haya William Malecela alitoa usia mzito kwa Chama chake CCM, na serikali yake, kwa wapinzani na kwa wana JF. Je William Malecela alitoa wosia gani kwa serikali, CCM, wapinzani na kwa Jf?.
Kwa wenye uwezo to listen in between the words, karibu hapa
Kwa wasio na uwezo to read in between the lines and to listen in between the words, juma lijalo nitawamegea wosia huu tits and bits nitawatafunia, nyie kazi yenu itabakia ni kumeza tuu!.
Wasalaam
Paskali