Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Kupitia mtandao wa kijamii wa facebook dorothy Gwajima amechapisha akileza kuwa wewe binti ambaye, fikra zako zinakutuma uwe mvivu mvivu kusoma au kujishughulisha na masuala ya maendeleo na kuwekeza kwenye harakati za yuko ambaye, Mungu alishamwandaa kwa ajili ya maisha yangu mimi, atanipa kila kitu.
Wosia wangu; zama zimebadilika, inuka, pambania maisha yako kwa elimu na shughuli za kiuchumi kwanza na mengine yatafuata yakiwa na baraka za Mungu.
Kwa nini nimesema haya?; vilio vya waliokuwa na mawazo kama hayo, vinavyonifikia kwa sms, ni vya majuto na vya kusikitisha mno. Ni kweli, wanaume nao wapo wanaopitia manyanyaso ila kwa namba, wanawake ni wengi mno na kisa mojawapo ni pale walipoacha kupambania ndoto zao za maendeleo yao kwanza, wakaanza kupambania ndoto za yuko aliyeandaliwa kwa ajili yangu.
Nasikia mengi, naona mengi, moyo wangu umeniambia, nitoe hii elimu ya ukumbusho kwenu jamii na hasa mabinti.
Hitimisho; maisha yapo, wanaume wapo, mahusiano yapo tu tangu enzi za Adamu na Hawa, cha msingi, hebu jiandae kwanza na maisha yako kwa kuweka bidii yako kwenye maendeleo ya baraka alizokupa Mungu.
Nani kanielewa? Nani hajaelewa? Kila mmoja abebe mzigo wake sasa, tukutane maishani.