Wote waliomtukana Shaffih Dauda kuhusu suala la Mo wamuombe radhi haraka sana

Wote waliomtukana Shaffih Dauda kuhusu suala la Mo wamuombe radhi haraka sana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Uungwana ni vitendo , Tunawajua wote mliotoa lugha chafu baada ya Shaffih Dauda ( Mzee wa under dog ) kuanika ukweli wa Mgogoro wa Simba , Kabla sijawataja majina yenu mnatakiwa kumuomba radhi haraka sana .

Shaffih kama mwandishi wa habari za michezo anayo haki ya kuripoti taarifa yoyote ya kweli hata kama inaumiza , huo ndio uanamichezo , mpaka dk hii taarifa ile bado imesimama wima mno! hakuna uongo wala uzushi wowote ule .
 
Wanakuja mkuu ngoja tuwasubiri hapa
 
Nao wakapiga kelele, wakaziba masiko yao wasitake kusikia alichokisema yule farisayo aliye mwandishi hata saa ilipofika nayo kweli ikachomoza kama miale ya nuru ichomozayo magharibi, ndipo mbumbumbu wote wakapoteana.
Kiromoni 3:9

Na hili ndilo neno la usiku huu
Bwana awe naaaaaaaanyiiiii
 
Ipo siku yake tu,anakujazieni wachezaji wenye mishahara mikubwa kwanza ili akitoka mnyooke
Kuwalipa watalipwa tu japo itakuwa kwa tabu mimi kama mwanachama wa Simba sports uwezo wa kuwalipa wachezaji wote wale kama tutakuwa na matokeo mazuri viwanjani tunao.

Msimu uliopita mechi za Simba zilikuwa zinaingiza kuanzia million 300+, hili jambo la Mo ni story tu tunawapikia mambo vyura mjisahau
 
Kwa hiyo unataka tuombe msamaha kwa jambo ambalo halijatokea, ulifikilia kweli kabla ya kuandika
Uungwana ni vitendo , Tunawajua wote mliotoa lugha chafu baada ya Shaffih Dauda ( Mzee wa under dog ) kuanika ukweli wa Mgogoro wa Simba , Kabla sijawataja majina yenu mnatakiwa kumuomba radhi haraka sana .

Shaffih kama mwandishi wa habari za michezo anayo haki ya kuripoti taarifa yoyote ya kweli hata kama inaumiza , huo ndio uanamichezo , mpaka dk hii taarifa ile bado imesimama wima mno! hakuna uongo wala uzushi wowote ule .
 
Tunamkasirikia kwa kuandika kwa "kushabikia habari zenye mlengo mbaya tu za Simba Sport Club na ze nye kuikejeri klabu yetu pendwa" kwa nia ya kuifedhehesha kitaifa au kimataifa.
Ukimwona huyo mwandishi akiisema Simba basi katika kuikejeri kuiponda na kuikatisha tamaa.
Ukimwona anaandika kuihusu Simba basi kwa habari mbaya tu za kuukuza mgogoro fulani au tatizo flani kwa nia ya kuuchochea mgogoro huo.
Kamwe hatujamsikia akiipongeza Simba au kuitia moyo au kuisema kimafanikio flani.
Yeye "ni kama Shetani wa Simba Sports Club"
 
Back
Top Bottom