Kama hawa wabunge wanaoitwa COVID -19 ni haramu ni kwa nini Chama kinapokea (kama kinapokea) ruzuku inayotokana na watu haramu wanaovunja ibara ya 78(e) ya Katiba ya JMT inayotabanaisha kuwa ili mtu awe mbunge ni lazima atokane na chama cha siasa?
Bila shaka hii ni danadana tu ilihali akina Mh. Freeman Aikael Mbowe na timu yake wanafahamu ukweli wa jambo lenyewe ila wameamua kuwazuga akina mama/ wanawake wa CHADEMA na kwa kutokufahamu akina mama hawa wameanza kupiga yowe wasilofahamu chanzo chake ni nini!
Pamoja na mapungufu ya kibinadamu, nimemsikia Mh. Job Ndugai - Spika wa bunge la JMT akiomba vielelezo rasmi ili aweze kuwatimua wale watu wanaoitwa COVID - 19 mle bungeni.
Ni kwa nini CHADEMA wasipeleke hivi vielelezo (Muhtasari wa kikao kilichoaziamia kuwavua uanachama, katiba ya chama (kifungu cha kumfukuza mwanachama) na maamuzi ya kamati/baraza kuu la chama) ili kuthibitisha kuvuliwa uanachama kwa hao watu na ivo kupoteza sifa ya kuitwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Muda ni mwalimu mzuri, ama Mbowe anawazuga wanachama wake au Spika Job Ndugai ameamua kuwakingia kifua watu haramu huku akifahamu kufanya hivyo ni kwenda kinyume ibara ya 78(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.