SoC01 Wote wanastahili Kuheshimiwa

SoC01 Wote wanastahili Kuheshimiwa

Stories of Change - 2021 Competition

Ntiyakama

Member
Joined
Sep 19, 2021
Posts
32
Reaction score
37
Nikiwa nazungumza na Mama mmoja aliyekuwa akijushughurisha na usafi nilipokuwapo, (Mama huyu nilimkuta mahala hapo nilipo ripoti mwaka wa kwanza: nilikuwa mwaka wanne katika eneo hilo wakati namuuliza swali hili) nilimuuliza;

“umekuwepo hapa kabla yangu, si muda mrefu nitaondoka pengine nitakuacha hapa; nini kimekuwa kikikustaajabisha sana katika muda wote uliokuwepo hapa?”

Mama aliinama kidogo, alipoinuka; alianza kusema kwa huzuni sana; namna ambavyo tumekuwa tukidhauriwa na vijana wadogo (baadhi) kuliko hata watoto wetu wa kuwazaa…!

Sawa, salamu si lazima sana; inasikitisha hata unapomwelekeza jambo – kijana; hatufanyi hivyo, hupaswi kunawia hapo, hapa si pahala pa kutupa taka (za namna hii), nivumilie kidogo nisafishe uendelee…

…wapo wanaojifanya kutosikia na kupuuza, bora hao - wapo wasioweza hata kukaa kimya au kujibu kwa busara, hujibu chochote wanachojiskia kujibu, wengine huenda mbali zaidi na kusema;

‘usinikarahishe; kwani mko hapa kwaajiri ya nini?!...usafi ni kazi yenu, naweza kuchafua sehemu yeyote na mtawajibika kusafisha, ndio kumewaweka mjini….’

Hawaishii hapo wapo wanao amua mpaka kutukana kabisaa…! Lakini; wapo pia ambao wanajiheshimu, wanajari na kuona kama kila mtu anathamani; wachache wa namna hiyo, wanafanya tuendelee kuwa na ari pia faraja katika kazi

Maneno hayo yalinikumbusha hadithi ya kijana mmoja aliyekuwa akifanya kazi kiwanda cha nyama, aliyefungiwa ndani ya chumba cha baridi (kwabahati mbaya), akasaidiwa na Mlizi, akiwa karibu kufa kwa baridi ya kunzia nyama

Mlinzi alizoe kila mara kijana yule alipotoka kazini, lazima alipita kumsalimu na kumuaga; lakini hakumuona siku hiyo, akaona shaka huenda hajatoka, akuamua kwenda kumtafuta ndayi ya kiwanda

“Mtendee yeyote unayehisi kumzidi nafasi, cheo, elimu, fedha, n.k, kwa heshima sawa na umpayo Bosi wako; hakuna atakaye pendezwa na namna uwatendeavyo kwa dharau uliowazidi, bali kila mtu atakujari kama utamtendea kwa heshima.”

Ni mama zetu, ni baba zetu, ni kaka na dada zetu na wengine ni wadogo zetu, tofauti huenda ikawa tu kwamba, wapo katika mazingira tofauti na sisi, hatukufahamiana nao kabla, wanafanya kazi tunazo zibedha ingawa bado zinatusaidia na nimuhimu sana katika maisha yetu ya kila siku.

Hakuna tofauti nyingine yeyote inayoweza kututofautisha nawao katika misingi na maana halisi ya utu.
Usimfanyie yeyote ambacho mwenyewe hautamani mwingine akufanyie wewe, heshimu na thamini wengine.

Hatakama katika mtazamo wako wandani umefikiri kuwa huyo aliyekukaribia hastahili hata kidogo heshima kutoka kwako, angalau msikileze ajaribupo kukuambia jambo na kama kutukana ndilo jibu pekee utakayoona anastahili, jaribu kukaa kimya angalau, kuepusha maumivu unayoweza kumpatia kwa maneno yadhalilishayo na pengine kuumiza, kutoka kinywani mwako.

“kama kutukana ndilo jibu pekee ulilonalo, kumjibu aliyekuuliza jambo: jaribu kukaa kimya angalau, kuepusha maumivu unayoweza kumpatia kwa maneno yadhalilishayo na pengine kuumiza, kutoka kinywani mwako.”

Kuheshimiwa ni jambo ambalo kila binadamu analihitaji, analitamani na analionea thamani. Hauitaji kiasi kikubwa cha fedha wala mali nyingi kununua heshima; jambo moja tu unahitaji nalo ni kujihemu na kuwaheshimu wengine.

Heshima itaiongeza thamani yako; ni thamani yako ndio itakayoamua aina gani ya maisha utayaishi; taaluma, cheo, fedha, familia, marafiki, mali vinaweza visifae chochote kama wewe kama binadamu, thamani yako imeshuka, umekosa heshima.

Watu wanaweza kukunafikia kuwa wanakujali/kukupenda kwasababu tu ya nafasi, fedha au nguvu ulizonazo; na ndani mwao wakiwa na uhalisia kuwa wewe ni mtu asiyefaa jambo linaloweza kuwa hatari zaidi kwako, utakapokujia wakati ambapo uhalisi utajidhihilisha.

Wote wanastahili kuheshimiwa.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom