kui
JF-Expert Member
- Mar 2, 2009
- 6,467
- 6,499
Nakubaliana na ushauri wako kwa Law Masha lakini kwa maoni yangu sio sahihi sana kuwaweka kwenye mizani moja na vigezo (parameters) vile vile Wenje na Law Masha kwa sababu moja au mbili kuu; Masha ni product ya political patronage na mfumo ule ule uliotufikisha hapa tulipo; sina uhakika kama wewe unapaona ni pazuri sana!! hata hao anaowaita wafadhili wa miradi aliyojinasibu nayo; tuna hakika gani kama sio Fedha ya umma iliyotokana na mradi tata wa vitambulisho vya uraia ambavyo mpaka wa leo havija-materialise ukiondoa uzinduzi tu?!
Wenje ni kama mpigania uhuru; hana nafasi na resources wala fursa alizokuwa nazo Law Masha kumuwezesha kufanya maendeleo msingi kama anayojinasibu nayo Law Masha; vyama vya upinzani havitambuliki na wala havikubaliki; bado mfumo uliopo umejaa watawala recycled wenye full hangover ya one party system!!
Self glorification na mbwembwe nyingi za Law Masha alipokuwa madarakani ni baadhi ya character flaws za Law Masha zilizokuwa zikiwakera wananchi na kuwafanya watumie haki yao kumkumbusha kwamba wao ndio waajiri wake and not vice versa!! behaving like a spoilt child or a yankee New yorker havikumsaidia hata kidogo na matokeo yake akabwagwa na mtoto mdogo akitokea chuo kikuu, a pure political novice or rookie kama wamarekani wanavosema! sasa hivi he is crying foul over spilt milk and embarking on a blame game which is unhelpful.
Hivi supporters wa Law Masha mmewahi kumuuliza kama aliwahi kukaa chini akafanya tathmini objective kabisa sababu za kuanguka kwake mpaka akapandisha jazba akaenda kustrip ofisi ya mbunge samani zote?!
Kwa hiyo kwa sasa kazi ya Wenje na wanamapinduzi wengine wa "nji hii" ni kujenga self awareness; wanachi kujitambua na kukataa udhalimu, unyonyaji, ukandamizwaji, rushwa na ufisadi wa raslimali zao ili kuelekea kupata mfumo mpya wa uongozi ambao ni people centered, a government of the people, by the people and for the people.
Tukifika hapo ndio tunaweza kuwauliza kina Wenje na wenzake; Wapi maendeleo mliyotuahaidi; nini tofauti yenu na watawala waliopita?!! and thus hold them to account.
You sound like someone I know!