Hili suala la internet tunaliongelea kishabiki wakati ni suala la kiuchumi ambalo inatakiwa tutumie data sahihi badala ya ushabiki wa nani bora kati ya simba na yanga. Ukishabikia kitu cha kiuchumi utaishia kuliwa na hatimaye utashangaa mbona kila mwaka mambo yangu hayabadiliki? Sasa tuangalie yafuatayo.
Internet ya nyumbani au ofisini: Nyumba au ofisi havihami na asilimia themanini ya muda ama tuko nyumbani au ofisini. Asilimia kama kumi ya muda tuko kwenye vyombo vya usafiri au tuko kwa marafiki au kwenye starehe (kwa wastani wa watu wengi). Asilimia chache sana ya muda tuko nje ya ofisi au nyumbani na tuko kazini hivyo; FIXED INTERNET NI CHEAPEST NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA ZAIDI WA KUITUMIA. HATA KAMA KUNA VI-USUMBUFU VYA HAPA NA PALE, FIXED INTERNET NI BEST. DUNIANI KOTE.
Sasa kwa Tanzania, TTCL wanauza 1GB for Tshs 30,000.00, 2GB kwa Shiling 60,000.00, na unlimited 256Kbps kwa Tshs 45,000 kwa mwezi. Sijaona rates za chini kuliko hizi. Mwenye kujua rates za chini zaidi hapa jamvini.
Kwa Matumizi ya ofisi angalia rates hizi, 4GB kwa 100,000.00, 10GB kwa 200,000; 20GB kwa 360,000 na mwisho wa zote 40GB kwa 450,000 na 100GB kwa 1m (yaani hapa unazungumzia shilingi 10 kwa 1MB). Wenye rates za chini zaidi katika soko wazilete hapa jamvini ili tujiridhishe.
Ni kweli at times utahitaji kutumia internet ukiwa mbali na nyumbani au ofisini, kwa hiyo you need an alternative means. Hapa utahitaji kuwa na second alternative ambayo kusema kweli lazima tuwe makini. Mobile rates hazitofautiani kama tunavyozungumza hapa. Zantel wanacharge Tshs 120 kwa MB na wana bundles kama ambavyo tumeshaziona hapa. TTCL wanacharge Tshs 160.00 kwa MB na wana bundles kama ambavyo tumeona vile vile. Tofauti ya TTCL na Zantel kwenye Mobile ni shilingi 40. Vodacom ni Tshs 264 kwa MB moja na Zain ni kama Tshs 300 kwa MB.
TTCL Mobile inapatikana makao makuu ya mikoa yote hapa nchini; Zantel ni kwa baadhi ya mikoa tu hata hapa dar kuna rafiki yangu anakaa maeneo ya Mbezi Makabe Zantel hakuna.
Ikiwa ninasafiri safiri mara kwa mara je naenda zaidi mikoa ipi? Vipi nikienda milkoa ile ambako Zantel haipatikani, what is the cost of missing my connection? Inawezekana kweli ile tofauti ya Tshs 40.00 kati ya TTCL na Zantel ikakufanya uingie gharama kubwa zaidi kwani ukienda mahali ambko zantel haipo, ama you miss kabisa au ununue second device which is additional expenses.
Kwa hiyo, mimi Nyumbani na ofisini natumia TTCL Broadband and it is cheaper. Nasafiri mara nyingi katika mikoa yote. Yaani sijui kama mwezi ujao nitakuwa mtwara au Sumbawanga au Mwanza. Mwanzoni nilikuwa na Vodacom 3G, siku moja nikasafiri nikatumia wiki mbili Mtwara. Niliporudi nikanunua Zantel. All was well, nikasafiri kwenda Sumbawanga wiki tatu. I had to buy TTCL mobile.
Sasa angalia; nilijikuta nimenunua devices tatu. Devices hizo ninazitumia ninapokuwa nimesafiri tu. Nimegundua I spent too much. Ningenunua TTCL mobile in the first place, nisingehitaji kununua Voda au Zantel tena. Ni vibaya sana kufanya maamuzi kwa kuangalia kitu kimoja tu eti mobility. Watu wengi tuna end-up spending too much kwa service ambazo kusema kweli hazihitaji mobility. Ikiwa asilimia themanini ya muda natumia internet nikiwa sehemu ile ile kwa nini nitumie hata shilingi zaidi kununua service ya mobile wakati ya landline ambayo ni bora na gharama nafuu zaidi ipo? Tuwe wachumi.
Ukitaka kujua watu wanaoangalia sana uchumi na ambao siku zote wako mbele nenda mitaa ya uhindini. Lazima utamkuta mtu analandline na ina Broadband. Hizi mobile na laptop wengi tunanunua for show off ambazo mara nyingi zinatuumiza zaidi kuliko kutusaidia.
Kumalizia, wisdom duniani kote ni kuwa 3G ni expensive.